Mahari na ndoa

LOTH HEMA

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2015
Posts
29,917
Reaction score
47,554
Wajuba, kutokana na miaka hii maadili ya ndoa kuporomoka na ndoa hazidumu, kuna haja ya kutoa mahari na kufanya sherehe ya harusi kwa kutegemea michango ya watu? Mbona miaka ya nyuma michango haikuwepo na ndoa zilidumu mpaka kifo? Inakuaje unapanga kufanya sherehe ya mamilioni kwa kutegemea mifuko ya watu? Mbona zamani mtu alijibeba mwenyewe kufanya sherehe ya harusi kwa bajeti yake? Kuhusu mahari, inakuaje utoe mahari halafu ndoa haidumu? Kwingine ukiasi ndoa mahari inarudishwa. Kama tumependana tuoane tu, wazazi wako watapata zawadi kimtindo kutokana na hali zao kiuchumi
 
Kutoa mahali haihusiani na ndoa kuvunjika.
 
Kutoa mahali haihusiani na ndoa kuvunjika.
huoni kuwa ni hasara ndoa kuvunjika huku imetolewa mahari? Bora kuchukuana bure, zawadi zitatolewa baadaye sana, tena kwa kuangalia hali ya kiuchumi ya wazazi wa mke
 
Ndoa si makubaliano , mimi rafiki yangu aligoma na ikafanyika simple ..Ndoa simple tu wala hauna presha , unakuata mtu miezi zaidi ya 4 anapata tabu ya kufirikia ndoa ...Mimi nitaoa Mungu akipenda mwaka huu, itakuwa simple tu tena usiku .
 
huoni kuwa ni hasara ndoa kuvunjika huku imetolewa mahari? Bora kuchukuana bure, zawadi zitatolewa baadaye sana, tena kwa kuangalia hali ya kiuchumi ya wazazi wa mke
Siamini ya kuwa watu wanaoana ili baadaye waje kuachana. Ninyi wenye mindset ya "itakuwaje nimetoa mahali halafu tuachane" huwa ni pessimistic(watu wenye mtazamo hasi) hasa kuhusu mahali.
 
Toa mahali mkuu uoe, kisha leta uzi tukushauli
 
Wazee walinambia kuwa wao ilikuwa ukishalipia maharii na kufata taratibu zote na ndo harusi basi atachinjwa ng'ombe, mchele hakuna kwa kipindi hiko na walikuwa hawajauzoea kutokana na maeneo basi watapika ndizi za kutosha na nyama na supu na mbege safi watu wanakula

Sana sana watu wa karibu watatoa ndizi za kupika, ama wengine watakupikia mbege lakini kikubwa unatoa wewe,

Ila sio kama sasa sherehe million 20 na kuendelea na bado mnadaiwa
 
Yaani mpaka sherehe inaisha umechoka , hivi ukiomba michango ukapata ile pesa , then ukatumia kama 10% ya harusi simple na inayobaki ukaanzia maishi ni bora zaidi ...Kama mtu anataka kutoa zawadi ni kheri ..Ila sasa bwana harusi anaingia gharama na stress baada ya ndoa .
 
Watu wa haiba yako huwa ni wabinafsi sana...Ni ngumu sana kudumu kwenye hiyo ndoa unayoianzishia uzi humu.

Punguza tu ubinafsi kwanza.
 
Inawezkn kabisa ttzo ni wewe na kamati yako itakuelewa ?

Kingine wabongo tuna akili nimetoa laki moja basi tukifka ni kula kunywa na kubeba ndo ttzo Hilo mkuu
 
Inawezkn kabisa ttzo ni wewe na kamati yako itakuelewa ?

Kingine wabongo tuna akili nimetoa laki moja basi tukifka ni kula kunywa na kubeba ndo ttzo Hilo mkuu
Mtihani sana huu, watu wakitulia basi wanandoa wanapata kitu
 
Mkuu ni zamani zipi unazozungumzia? AU ni miaka ya nyuma ipi unayozungumzia?, Ambayo watu walikuwa hawachangii sherehe za harusi.

Nafikiri kilichobadilika ni aina ya michango inayotolewa, Zamani ilikuwa michango ya HALI na MALI, ila siku hizi ni MALI sana. Ukitaka kuchangia HALI unaonekana wewe hufai.
 
mambo yanabadilika na maisha yanabadilika pia gentleman,

mila, desturi, utamaduni na ustaarabu wa jamii mbalimbali nchini unabadilika kulingana na hali halisi ya mabadiliko ulimwenguni.

mahari ibaki tu ni jambo la jamii yako ndogo.
Lakini ndoa ni jambo la jumla la kistaarabu linalotambulika ulimwengu mzima.

sababu za kuvunjika kwa ndoa yako kunaweza kua tofauti kabisa na kuvunjika kwa ndoa ya mwingine.
kuvunjika kwa ndoa hakuna uhusiano wowote na mahari.

Technolojia, tamaa, pesa, elimu na ugumu wa maisha vimekua ni baadhi ya sababu muhimu sana za kuvunjika kwa ndoa nyingi nyakati hizi
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…