Jodoki Kalimilo
JF-Expert Member
- Feb 12, 2012
- 12,671
- 11,338
Heri usukumani kuna mahari ya ng'ombe mnyama na ng'ombe fedha (ambayo kidogo ina unafuu kuliko kuambiwa kuleta ng'ombe original)Bei ya ngombe dume na mkaja wa mama vinapangwa na kwa kuangalia uwezo wa muoaji.
Binti ndio anajua uwezo wa mwanaume hivyo wanaweza kutaja hata 50,000-milioni kwa bei ya ng'ombe dume. Na mkaja inaweza kua 20,000-500,000 na hata zaidi.
Kimsingi masharti sio magumu sema hali ya kiuchumi imekuwa ngumu pia mabadiliko ya mila na desturi kutokana na maendeleo tunajikuta tunaenda kuoa kwenye community nyingine mfano mpare anaoa muha n.k. hivyo ukikutana na hayo mambo miguu inakuingia tumboni. Zamani iliwezekana watu walioa kwenye the same community hivyo hata kabla ya kuoa mtu anajiandaa na isitoshe jukumu la kulipa mahari lilikuwa ni la baba mzazi hivyo kama baba wengi wao walikuiwa wanajiandaa kwa kufuga mifugo miwili mitatu mpaka vijana wake watakapofika muda wa kuoa linatoka dume moja linakwenda kumaliza issue.Wanyakusya hawafai wana masharti magumu ya kuoa we acha kabisa halafu mabinti wenyewe wabishi na jeuri ukishawaweka ndani! Mke wangu ni mnyakyusa nilipoenda kuoa cha moto nilikiona. Kuna kitu wanaita mkaja wa mama, sijui kikingi, hela ya shangazi, vitenge, mablanketi, mashuka, ng'ombe 3 wawlli majike na dume moja, ukikaribishwa unalipia pale ulipokaa, wakileta msosi usidhani ni bure baada ya kula utaulipia. Mbona niliomba po at once nilijikuta km 2m zinakatika!
Ndagha Malafyale !
!
N'deke mwalangani na ilyopa lyake !
Habari Zenu Ndugu Zangu Wana MMU.Nilikuwa Sijawahi kuhudhuria tendo la kutoa posa kwa Wanyakyusa ila leo nimekuwa mmoja wapo wa kupeleka barua ya posa.
Swala la kupanga mahari limentoa macho kidogo huenda ni mimi kutokuwa na uzoefu.Kama ilivyo ada tumewasilisha barua vyema wakaipokea vizuri sana na baadaye tukapewa majibu kamaa ifuatavyo.
Mshenga upande wa binti kaanza kwa kusema sisi wanyakyusa huwa tunazo mahari mara mbili.(1).Mahari Ya Unyago ambayo ni non negotiable,ni kama ifuatavyo.
1.Ng'ombe Dume ambaye dhamani yake ni Tshs.500,000.Na hapa lazima utoe hela ng'ombe haitajiki.
2.Tshs.400,000 Za Mama Mzazi.
3.Blanketi 2 za wazazi.
4.Vitenge kulingana na idadi ya mashangazi.
(2)...Mahari Ya Pili ni negotiable:
1.Ng'ombe Wanne Majike.
2.Vitenge Vya Mashangazi.
Jamani nia yangu ya kuleta hili swala hapa ni kupata mtazamo wenu.
Je,Kwa Kijana wa kiume ambaye ametoka kwenye familia hohehahe ataweza kweli??
KARIBUNI MNIPE MTAZAMO WENU.
Na msingeenda na barua,mngepigwa faini!lakini huwa wanaangalia na waoaji wameendaje pale.kama mmeenda kitajiri basi mtalingana na mahari mtakayoambiwa.
Karibuni unyakyusani
Sent from my iPhone using JamiiForums
Kimsingi masharti sio magumu sema hali ya kiuchumi imekuwa ngumu pia mabadiliko ya mila na desturi kutokana na maendeleo tunajikuta tunaenda kuoa kwenye community nyingine mfano mpare anaoa muha n.k. hivyo ukikutana na hayo mambo miguu inakuingia tumboni. Zamani iliwezekana watu walioa kwenye the same community hivyo hata kabla ya kuoa mtu anajiandaa na isitoshe jukumu la kulipa mahari lilikuwa ni la baba mzazi hivyo kama baba wengi wao walikuiwa wanajiandaa kwa kufuga mifugo miwili mitatu mpaka vijana wake watakapofika muda wa kuoa linatoka dume moja linakwenda kumaliza issue.
Tatizo madingi wetu wametutosa siku hizi mahari unalipa wewe mwenyewe wakati yeye anaoa alilipiwa na mzee wake, pia kama hela ya sherehe asilimia kubwa utajitutumua mwenyewe though kwenye kikao cha kwanza yeye ndio anajifanya familia tuna kiwango hiki (uzoefu kwa wengi kimjinimjini except wachache)
Heri usukumani kuna mahari ya ng'ombe mnyama na ng'ombe fedha (ambayo kidogo ina unafuu kuliko kuambiwa kuleta ng'ombe original)
Mahali ndogo ivo unalalama,,,, huku watu tunaolewa kwa gharama fuso akiwa tajiri semi au bus
Mahali inaombwa au kutolewa kutokana uwezo wa familia ya kijana.
Ni jukumu la binti kuwaeleza wazazi wake uwezo wa mkwe wao mtarajiwa ili wakati wa kupanga mahari wajue mkwe wao ni mtu wa namna gani.
Sidhani kama kuna familia inaweza kumzuia binti yao kuolewa kwa kutoza mahari kubwa!
Bei ya ngombe dume na mkaja wa mama vinapangwa na kwa kuangalia uwezo wa muoaji.
Binti ndio anajua uwezo wa mwanaume hivyo wanaweza kutaja hata 50,000-milioni kwa bei ya ng'ombe dume. Na mkaja inaweza kua 20,000-500,000 na hata zaidi.