Mahari inaendaga wapi?

Mahari inaendaga wapi?

Heshima yenu wakuu! mwenzenu hilo swali hapo juu linasumbua akili yangu hivyo nataka kufahamu. Binti anapochumbiwa na kutolewa MAHARI(pesa) huwa inaenda WAPI? Je,anapewa yeye mwenyewe yote kwa mambo yake binafsi, au wazazi/walezi baba na mama wanagawana peke yao, au familia nzima huwa inagawana wakiwemo mashangazi cjui wajomba madada na makaka, au binti mwenyewe na wazazi wake pekee, au huwa inawekwa kwa ajili ya maandalizi ya vitu kama kitchenparty na sendoff?,ama inakuwaje? Au matumizi na mgawanyo huo hutofautiana kabila na kabila? Nijuzeni mwenzenu mana sikuhizi mahari imekuwa kama mtaji mtu anaoa hadi kwa millioni 2 utadhani ananunua kiwanja magwepande daah! That y vijana bado wapowapo wakifikiria hapa, siwalaumuu! Haya karibuni kwa discussion..... Nitarudi bdaye! Cc Heaven on earth christine ibrahim Lady doctor @Lara1 Nivea Smile miss strong DEMBA Kongosho Mamndenyi Mtambuzi watu8 Himidini HorsePower Mr Rocky Kaizer and OTHERS...

wanagawana wenye kujidai kwamba binti wamemzaa na kumtunza
 
Ya binti zangu ntakula peke yangu lol
hakuna cha mjomba wala shangazi
 
Dah usukumani watu wanatoaga ming'ombe mingi kiasi kwamba hata zikiuzwa thamani yake inakuwa kubwa kweli.
 
Heshima yenu wakuu! mwenzenu hilo swali hapo juu linasumbua akili yangu hivyo nataka kufahamu. Binti anapochumbiwa na kutolewa MAHARI(pesa) huwa inaenda WAPI? Je,anapewa yeye mwenyewe yote kwa mambo yake binafsi, au wazazi/walezi baba na mama wanagawana peke yao, au familia nzima huwa inagawana wakiwemo mashangazi cjui wajomba madada na makaka, au binti mwenyewe na wazazi wake pekee, au huwa inawekwa kwa ajili ya maandalizi ya vitu kama kitchenparty na sendoff?,ama inakuwaje? Au matumizi na mgawanyo huo hutofautiana kabila na kabila? Nijuzeni mwenzenu mana sikuhizi mahari imekuwa kama mtaji mtu anaoa hadi kwa millioni 2 utadhani ananunua kiwanja magwepande daah! That y vijana bado wapowapo wakifikiria hapa, siwalaumuu! Haya karibuni kwa discussion..... Nitarudi bdaye! Cc Heaven on earth christine ibrahim Lady doctor @Lara1 Nivea Smile miss strong DEMBA Kongosho Mamndenyi Mtambuzi watu8 Himidini HorsePower Mr Rocky Kaizer and OTHERS...

Kwa kawaida mahari inaenda kwa wazazi, hususan baba mzazi. Ila kwa kusikitisha, zile pesa baba mzazi huchukua na kwenda kuoa mke wa pili ama wa tatu bila mama mzazi kushirikishwa. In short, mahari imekuwa ruhusa ya ufuska kwa baba mzazi.
 
Mahari kama walivyotangulia kuchangia inategemea na mila za kabila lako. Kabila letu mahari ikitolewa kama ni ng'ombe wanauza ng'ombe unanunuliwa zawadi kadhaa, zinazobaki kama mna kijana wa kiume na yeye anatafutia mke na kwa kuwa zimepungua tayari baada ya kuuzwa hapo inabidi kijana asubiri either miaka miwili zizaliane ili zitoshe na yeye atoe mahari. Au mjomba anachukua jukumu la kununua hizo zawadi afu anapewa ng'ombe wawili.
 
Kwa mujibu wa taratibu na mafundisho ya kiislam, Mahari huwa ni stahiki ya binti.

Mengineyo ni tamaduni na mapenzi binafsi juu ya mgao.
.
Munkari pitia bandiko hili pia litakupa mwanga zaidi (kwa mujibu wa Uislam kama alivyosema Rock City)

Kwa kuongezea tu ni kwamba kiasi cha mahari hupangwa na binti muolewaji na kisha baada ya mchakato wa mahari kukamilika hukabidhiwa kiasi hicho cha mahari na yeye (kwa mapenzi yake) ataamua kuwagawia wazazi, walezi ama ndugu zake. Rock City utaongezea mengine kwa ufafanuzi zaidi.
 
Mahari kama walivyotangulia kuchangia inategemea na mila za kabila lako. Kabila letu mahari ikitolewa kama ni ng'ombe wanauza ng'ombe unanunuliwa zawadi kadhaa, zinazobaki kama mna kijana wa kiume na yeye anatafutia mke na kwa kuwa zimepungua tayari baada ya kuuzwa hapo inabidi kijana asubiri either miaka miwili zizaliane ili zitoshe na yeye atoe mahari. Au mjomba anachukua jukumu la kununua hizo zawadi afu anapewa ng'ombe wawili.

daah! Mila nyingine ngumu kweli yani kakangu asubiri miye niuzwe ndo nayeye akaolee dah c akatafute zake?nahisi kama ni uonevu flani hivi! Ila ndo utaratibu wenyewe huo tusiudharau!
 
Uchoyo huo mkuu.

sio uchoyo ni haki
siku hizi wanaume hawaoi binti asiye na kazi nzuri

na kazi nzuri mpaka binti asomeshwe shule nzuri na wazazi wake
mzazi unajinyima binti yako asome
halafu mtu akiona ana kazi nzuri analeta posa
sasa hapo unajilipa pensheni..lol
 
haahaha! Dah nnawaswas na wewe utakuwa wa kibosho!
 
Sie kwetu mahari hadi walioko vijijini hata kama ni watoto lazima wapewe chao haijalishi ni 200,300 lazima wapewe.
...duh kweli nyie noma......mi naona kwetu hata hizo mila hakuna maana ni full mchanaganyiko, so ambacho nilikiona kwa ndugu yangu ni hiyo mahali kupewa wajomba na wazazi wakagawana..vinhine hata cjui
 
Back
Top Bottom