Mahakimu wasambaratishwa Tanzania nzima

Mahakimu wasambaratishwa Tanzania nzima

AZUSA STREET

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2013
Posts
2,007
Reaction score
1,898
Nimeona leo mahakimu wakiwa mwamehamishwa hamishwa balaa, wametawanywa.

Hii ni nzuri, sio vizuri hakimu kukaa sehemu moja miaka mingi hadi anajenga kiota, anajenga undugu hivyo anaendesha kesi kwa kujuana etc.

Hapo nawapongeza. kilichobaki ni kwa Mawakili wa Serikali sasa, sijui lini watawasambaratisha na wao ili wasiendeshe kesi kwa mazoea na watu waliowazunguka na kuwazoea.
 
Huwezi kukomesha rushwa kwa kuwahamisha watumishi, rushwa itapungua kwa kuboresha maslahi yao
 
Huwezi kukomesha rushwa kwa kuwahamisha watumishi, rushwa itapungua kwa kuboresha maslahi yao
Nakubaliana na wewe partly ila naongezea kuwa rushwa ni tabia. Wapo watu hata uwape maslahi kiasi gani watakula rushwa tu.
 
Nakubaliana na wewe partly ila naongezea kuwa rushwa ni tabia. Wapo watu hata uwape maslahi kiasi gani watakula rushwa tu.
Hello ni jema sana kuwatawanya ha wa jamaa wkt mwingine nawachukia sana
 
wamewasambaratisha, wengine wamewapeleka mbali sana. kwenye ile list inazunguka mitandaoni wengine naona wametoka kusini wamepelekwa kaskazini, wengine kaskazini wamepelekwa kusini....binafsi naona wamefanya bora, kwasababu hakimu akikaa sehemu moja kwa muda mrefu anazoea eneo, anajenga vigenge na anashindwa kunyoosha mstari. hata kama tutasema rushwa ni tabia ya mtu sawa, lakini kuna wakati mwingine kama hakimu mnywaji wa pombe etc ana zoeana na watu hadi anashindwa kufanya kazi kwasababu anaokunywa nao, aliozoeana nao ndio haohao anatakiwa kuhukumu kesi ndio maana tunaweza kusema ameshindwa kuandika hukumu kumbe amehangaika kubumba na kupindisha ili kumuokoa mtu anayefahamiana naye kwa karibu.
 
Hawa mahakimu wetu kwakweli wanadumaza taaluma ya sheria, shule tunasoma kingereza wao wanatulazimisha kuzungumza kiswahili mahakamani...ajabu sana hii...ni kama vile wao walisoma sheria kwa kiswahili..
 
Nimeona leo mahakimu wakiwa mwamehamishwa hamishwa balaa, wametawanywa. hii ni nzuri, sio vizuri hakimu kukaa sehemu moja miaka mingi hadi anajenga kiota, anajenga undugu hivyo anaendesha kesi kwa kujuana etc. hapo nawapongeza. kilichobaki ni kwa Mawakili wa serikali sasa, sijui lini watawasambaratisha na wao ili wasiendeshe kesi kwa mazoea na watu waliowazunguka na kuwazoea.

Unaposema "hakimu unaendesha kesi kwa kujuana" wamaanisha nini? Unamaana huduma ya kesi mahakamani ni huduma ya jamii ya kila siku?
 
kina hakimu nimemkatia rufaa alikuwa ameahidiwa nusu ya hela nilizodaiwa, sijui kahama!
 
Unaposema "hakimu unaendesha kesi kwa kujuana" wamaanisha nini? Unamaana huduma ya kesi mahakamani ni huduma ya jamii ya kila siku?
Hapo Hakuna ukweli kwakua lazima atoe hukumu kwa mujibu wa sheriaa.
 
Hawa mahakimu wetu kwakweli wanadumaza taaluma ya sheria, shule tunasoma kingereza wao wanatulazimisha kuzungumza kiswahili mahakamani...ajabu sana hii...ni kama vile wao walisoma sheria kwa kiswahili..
kwa mujibu wa Taratibu wa mahakama za Tanzania,kiingereza kinatumika kuanzia mahakama kuu,hata hivyo kama una kesi mahakama za chini na hujui kiswahili,sheria inakutaka upatiwe mtaallam wa lugha unayoijua wewe ambayo itakua rahisi kwako kuendeshea kesi
 
The move behind? Katika udikiteita kila kinachofanyika ni kulinda oppressive regime!
 
Nimeona leo mahakimu wakiwa mwamehamishwa hamishwa balaa, wametawanywa.

Hii ni nzuri, sio vizuri hakimu kukaa sehemu moja miaka mingi hadi anajenga kiota, anajenga undugu hivyo anaendesha kesi kwa kujuana etc.

Hapo nawapongeza. kilichobaki ni kwa Mawakili wa Serikali sasa, sijui lini watawasambaratisha na wao ili wasiendeshe kesi kwa mazoea na watu waliowazunguka na kuwazoea.
Muwe mnawalipa pesa za kueleweka manake hao pia wana ndoa zao na watoto wanaosoma (wengine wanasoma private na wamelipa ada tayari)!
 
kwa mfumo wa ajira ya tanzania, matatizo ya ndoa katika kada hijyo na utoro kazini, na ongezeko la rushwa vinafuatia. mme/mke kahama kamwacha mwenza anaefanya jazi tofauti. kila mmoja anapata mwanya, visingizio kutofika kazini kumbe karudi kuiona familia.
 
Unaposema "hakimu unaendesha kesi kwa kujuana" wamaanisha nini? Unamaana huduma ya kesi mahakamani ni huduma ya jamii ya kila siku?
ndio ni huduma ya kila siku, hautalijua hilo hadi uwe na kesi mkuu hapo ndio utajua kama ni huduma au la. ni huduma tena kubwa na ya msingi mno na ni ya kiuchumi kwasababu ni sehem ya kupata au kukosa haki, ni sehemu ya kupata au kupoteza pesa etc.
 
kwa mujibu wa Taratibu wa mahakama za Tanzania,kiingereza kinatumika kuanzia mahakama kuu,hata hivyo kama una kesi mahakama za chini na hujui kiswahili,sheria inakutaka upatiwe mtaallam wa lugha unayoijua wewe ambayo itakua rahisi kwako kuendeshea kesi
hahaha, umeenda chaka sana mkuu. kiingereza ni kuanzia mahakama ya wilaya kwenda juu. hata ukiona umeongea kwa kiswahili jua hakimu/jaji kwenye jalada anarekodi kwa kimombo. huu ndio ukweli, mahakama ya mwanzo tu ndio lugha yake mama ni kiswahili.
 
Nimeona leo mahakimu wakiwa mwamehamishwa hamishwa balaa, wametawanywa.

Hii ni nzuri, sio vizuri hakimu kukaa sehemu moja miaka mingi hadi anajenga kiota, anajenga undugu hivyo anaendesha kesi kwa kujuana etc.

Hapo nawapongeza. kilichobaki ni kwa Mawakili wa Serikali sasa, sijui lini watawasambaratisha na wao ili wasiendeshe kesi kwa mazoea na watu waliowazunguka na kuwazoea.
yaani pamoja na na teknolojia yote hii ya utandawazi bado kuna watu wanaamini kuhamisha hamisha watu kunapunguza "networking"?

kweli janga la elimu is real!
 
kina hakimu nimemkatia rufaa alikuwa ameahidiwa nusu ya hela nilizodaiwa, sijui kahama!
hapo umeshinda kesi, ila wakumbuke tu ku assign reason kwenye record wanapohama wakati wa re-assignment. huwa na impact kubwa kwenye appeal.
 
yaani pamoja na na teknolojia yote hii ya utandawazi bado kuna watu wanaamini kuhamisha hamisha watu kunapunguza "networking"?

kweli janga la elimu is real!
nafikiri networking ya uso kwa uso na networking ya mtandao ni vitu viwili tofauti. hata kutongoza (kama umeoa) huwezi kuchumbia kwenye simu hadi mahali, mkionana ndio bond inakuwa kubwa ila kama mpo mbali ni ngumu. pia, communication ukiondoa ile ya uso kwa uso, ni hatari sana kwasababu simu zao nyingi zinaweza kupekuliwa sometimes where need be na hasa likitokea tatizo (no confirmation, inasemekana).
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom