Mahakimu wanafunzi (Intern Magistrate) Waamua Kesi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahakimu wanafunzi (Intern Magistrate) Waamua Kesi

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Kichakoro, Oct 1, 2012.

 1. K

  Kichakoro JF-Expert Member

  #1
  Oct 1, 2012
  Joined: Sep 10, 2008
  Messages: 1,556
  Likes Received: 1,322
  Trophy Points: 280
  katika pita pita yangu nimekutana ni issue ya mahakimu wanafunzi (interns) wakiwa wanasikiliza Kessy
  na hata kuitolea maamuzi (hukumu) baada ya kuisikiliza. mawali ninayojiuliza bila majibu


  1. Je ni sahihi kwa hakimu mwanafunzi kusikiliza kesy na kuifanyia maamuzi? Kama jibu ni Ndio nenda swali la pili na kama ni hapana nenda number 3
  2. Je wamekula kiapo?
  3. Je maamuzi waliofanya (hata kama ni chini ya usimamizi wa hakimu) je yana uhalali kisheria?
  4. Kama hawajaapishwa kisheria, je uhalali huo wameupata wapi?
  5. Wakati wanaendesha kesi, je watuhumiwa ama mlalamikaji atamuaddress kama hakimu (ieleweke bado ni mwanafunzi)?
  6. Je, kuna sheria yeyote inayowapa nguvu ama mamlaka kufanya ivyo? kama ipo ni ipi?
  7. Kama wafanyayo ni batili (null and Void) je kesi zilizoamuliwa na watu hawa zinaguvu kisheria?
  Maswali ni mengi hivyo naomba ufafanuzi wa wataalaam wa sheria. Ieleweke sina utaalam wa taaluma hii ndio maana napenda kujifunza
   
 2. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #2
  Oct 1, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Kama wanafanya chini ya usimamizi wa hakimu kuna shida gani? - mwisho wa siku si ni hakimu husika ndio anatoa maamuzi na kubeba dhamana ya maamuzi yaliyotolewa. Naona kama ni utaratibu wa kawaidia kwa fani/taaluma mbalimbali (udaktari, uhasibu, engineering etc).
   
 3. b

  ba nso JF-Expert Member

  #3
  Oct 1, 2012
  Joined: Aug 21, 2012
  Messages: 640
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  Hakuna kitu kama "intern Magistrates" Tanzania, maana uhakimu hausomewi chuo chochote, tofauti na udaktari. kwasasa hakimu anaye ajiriwa sifa kubwa ya msingi ni awe amemaliza shahada ya sheria. Naomba ufanye utafiti wako upya.
   
 4. K

  Kichakoro JF-Expert Member

  #4
  Oct 1, 2012
  Joined: Sep 10, 2008
  Messages: 1,556
  Likes Received: 1,322
  Trophy Points: 280
  SMU,

  Aliyeandaa na kusoma hukumu sio msimamizi bali hakimu mwanafunzi suala hapa sio utaratibu bali ni kujua huu utaratibu una nguvu kisheria?
   
 5. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #5
  Oct 1, 2012
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  Interns are not allowed to hear undermine cases. If they do it's illegal
   
 6. K

  Kichakoro JF-Expert Member

  #6
  Oct 1, 2012
  Joined: Sep 10, 2008
  Messages: 1,556
  Likes Received: 1,322
  Trophy Points: 280
  Mkuu chuo cha sheria Lushoto wanasoma kina nani? Najua kuna mabadiliko yanafanyika kama ulivyonesha hapo juu

  lakini Mwaka wa pili walikua field (practical) n.k Yote tunaita mafunzo kwa vitendo. sasa napenda kufahamu tu kisheria na taratibu zake wanaruhusiwa
   
 7. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #7
  Oct 1, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Kama ni hivyo basi kuna walakini!
   
 8. v

  valid statement JF-Expert Member

  #8
  Oct 1, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 2,737
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Mbona mahospitalini, intern doctors huwepogo. Na hatulalamikir?
  Na huwa hawana lesen za udokta, hawana tabu hao mahakimu...
  Hata ivo hayo ni maoni yangu,sina uelewa wa mambo ya sheria
   
 9. M

  Mbalamwezi JF-Expert Member

  #9
  Oct 1, 2012
  Joined: Sep 30, 2007
  Messages: 803
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Mkuu Kichakoro,
  kwanza omba kufahamu kama wanayosikiliza ni Kessy au kitu kingine. Inawezekana kabisa mnazungumzia kitu kingine.

  lakini kwa maana ya mwenendo wa shauri lililopo mahakamani, au KESI, huhumu haiwezi kutolewa na mwanafunzi. Anachoweza kufanya ni kuandika, kwa mujibu wa sheria, (ambazo ni zile zile ambazo angetumia hakimu) halafu, hakimu, am kwa hapa tumwite msimamizi wa huyo mwanafunzi, ataifuatilia kama iko sahihi na kuikubali kama ambavyo angeifanya yeye. Baada ya hapo ataimiliki yeye, kwa maana kama ni uwajibikaji itakuwa ni yeye. Atahukumu.
   
 10. b

  ba nso JF-Expert Member

  #10
  Oct 1, 2012
  Joined: Aug 21, 2012
  Messages: 640
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  Kile ni chuo cha uongozi wa mahakama, wanaosoma hufanya kazi mbali mbali za kimahakama si lazima wawe mahakimu na pale wanasoma diploma, kwa hiyo kwasasa hakuna hakimu atatoka hapo baada ya kuhitimu mpaka wakasome tena miaka 4 shahada na mwaka 1 ikibidi law school.

  kuhusu jinsi ya kuandaa hukumu na kusikiliza kesi ni sehemu ya mafunzo ya wanafunzi wa sheria, sheria iko wazi kuwa hukumu yoyote ni lazima iwekwe sahihi na hakimu husika kwa maana hiyo basi hao wanafunzi hawana uwezo wa kusikiliza kesi peke yake na kuandika hukumu,

  ni lazima awepo hakimu na kama ameandaa "mfano wa hukumu" anampatia hakimu asahihishe (the magistrates marks the template for accademic purpose which at the end of the field practice the marks are submitted to the university via field supervisor).

  Na kama hakimu ameridhika kuwa kaandika vizuri kabisa hufanya marekebisho muhimu na kuifanya kua ndio hukumu mwisho wa kesi.
   
 11. K

  Kichakoro JF-Expert Member

  #11
  Oct 1, 2012
  Joined: Sep 10, 2008
  Messages: 1,556
  Likes Received: 1,322
  Trophy Points: 280
  Wakuu nashukuru kwa maelezo. Pia naomba tufuatilie yanayoendelea kwenye mahakama zetu
  mtakua suprised sana maaana kuna ukiukwaji mkubwa wa taratibu.

  sitopenda kuitaja mahakama lakini hapa hapa dar es Salaam wilaya za kinondoni na Ilala yanatokea.

  Fuatilieni kwa karibu
   
 12. M

  Mbalamwezi JF-Expert Member

  #12
  Oct 2, 2012
  Joined: Sep 30, 2007
  Messages: 803
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  Mkuu, huo niliopigia mstari ni udhaifu mkubwa kama kweli hupendi yanayotokea kwenye mahakama zetu. Hupendi kutaja majina ili kiwe nini? Na kwa nini basi tufuatilie ikiwa hata wewe umefuatilia na hupendi kutaja majina? Kila mtu afuatilie na ibaki kuwa siri yake? Namna bora kabisa ya kuwajibika kila mtu pale alipo ni kusema ukweli kwa yale ambayo tunaona yanaharibu jitihada za kuleta maendeleo. Huduma za mahakama ni muhimu sana katika kusimamia haki kwa wakati, na tunawajibika kutoa maoni kwa kusema ukweli pale tunapoona mambo hayaendi sawa.

  Sasa mtu kama wewe akija na kusema kuna tatizo mahali, na hataki kutaja ni wapi, basi unajipunguzia mwenyewe heshima ya kusikilizwa na kuaminiwa. Sasa kama unashindwa kutaja hapa jamvini, tena pa wazi na huru, utataja wapi, kwenye mkutano wa wazi wa Chadema au CCM?
   
 13. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #13
  Oct 2, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  ni bora afunguke mapema ili tujue nini kinatakiwa kufanyika kama tatizo kama hilo ukikutana nalo..
   
 14. K

  Kichakoro JF-Expert Member

  #14
  Oct 2, 2012
  Joined: Sep 10, 2008
  Messages: 1,556
  Likes Received: 1,322
  Trophy Points: 280
  Nashukuru kwa comment

  sijafanya ivo kwa sababu aliyenipa hizi taarifa ni mmojawapo wa intern kwenye mahakama
  husika yeye mwenyewe hajafurahia ndio maana sijaitaja mkuu.
   
 15. s

  semba masondole New Member

  #15
  Oct 5, 2012
  Joined: Oct 5, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sheria aina mbwembwe kaka! Wanakwenda kiutaratibu
   
 16. don-oba

  don-oba JF-Expert Member

  #16
  Oct 6, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 1,384
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  kwa sheria zetu, hata mwenyekiti wa kijiji, diwani au mtu mzima mwenye hekima anaruhusiwa kutoa hukumu katika mahakama za mwanzo! Sasa kama hawa wanaruhusiwa hao watashindwaje? Pili ukiwa na shahada ya LL.B haihitaji uwe na tiketi ya school of law kuwa mwanasheria.
   
 17. v

  victor lee Member

  #17
  Oct 9, 2012
  Joined: Jul 14, 2012
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pengne una ongelea MOOT COURT ,au kati ya mahakimu 300 walio ajiriwa juz juz ambao kabla ya kuripot kazn walipewa semina na mbinu pale HC kama ni wa dzain hyo waliapishwa kwanza af semina ndo zikaanza. kama issu ni kuapa basi waliapishwa kam ni validity ya decsn yao bas da issue wil be wether or nat they were entertaining da case u/supervision ov a competent magistrate or judge with extended jurisdictin over such matter in qn at da materiat date.
   
 18. K

  KANAN Senior Member

  #18
  Oct 13, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 124
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  inawezekana wao wamerise issues na kuzijibu na kuandika hukum, then hakiu uhusika akaipitia na kama akiiona ipo sawa anachofanya ni kuisaini tu....kwa hiyo aliyeiandika ni yule aliye saini, kwangu mimi hakuna shida.
   
Loading...