VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Wale Mahakimu Wakaazi 300 walioajiriwa na Serikali mnamo mwezi wa sita na kusambazwa mikoani wako njiani kugoma.Taarifa nilizozipata zinaonesha kuwa Mahakimu hao,tangu kuajiriwa kwao hawajalipwa mshahara wowote au hata fedha za kujikimu. Taarifa zinaonesha kuwa hali zao sasa ni mbaya na wanateseka vya kutosha.
Kwakuwa wote wanajuana vyema,Mahakimu hao Wakaazi ambao wamepelekwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama za Mwanzo wamepanga kugoma ili kudai maslahi yao kwa Serikali 'sikivu'. Ifahamike kuwa Mahakimu wakaazi ni wale wenye elimu ya ngazi ya Shahada na kuendelea na hawakuwahi kuwepo katika Mahakama za Mwanzo.Kupelekwa kwao,kutaruhusu Mawakili Wasomi kujitokeza Mahakama za Mwanzo.
Wanasema 'liwalo na liwe'....