Mahakama za mwanzo kuboreshwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahakama za mwanzo kuboreshwa

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Rutashubanyuma, Dec 28, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 28, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  Mahakama za mwanzo kuboreshwa


  na Mwandishi wetu


  [​IMG] JAJI Mkuu mpya, Mohamed Othaman, amesema kazi kubwa iliyoko mbele yake ni kuhakikisha mahakama zinatoa haki kwa wananchi kwa wakati. Jaji Othman alisema hayo jana jijini Dar es Salaam muda mfupo baada ya kuapishwa na Rais Jakaya Kikwete kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania, Ikulu, Dar es Salaam.
  Alisema hata hivyo katika sekta hiyo kuna changamoto nyingi ambazo ni za muda mrefu na kutoa mfano kuwa mahakama za mwanzo ambazo zinahudumia wananchi wengi zinapaswa kuboreshwa ili ziwe na mawakili wa kutosha na wenye ujuzi.
  Kwa upande wake, Jaji Mkuu Mstaafu, Augustine Ramadhani, alisema katika uongozi wake amejitahidi kuvunja wigo uliokuwapo kati ya mihimili mitatu nchini ambayo ni serikali, Bunge na mahahama.
  “Nimejitahidi kuwepo kwa mafanikio kati ya mihimili hiyo, kwani kila siku ya sheria Rais na Spika wa Bunge wamekuwa wakihudhuria tofauti na enzi za Jaji Nyalali,” alisema.
  Alieleza mafanikio mengine kuwa ni kuanzishwa kwa mfumo wa teknohama, kupatikana kwa majaji wengi na mahakimu kuongezwa maslahi pamoja na paadhi ya kanuni kufanyiwa marekebisho.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Dec 28, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,748
  Likes Received: 416,592
  Trophy Points: 280
  Kero za mahakama kamwe hazitapatiwa ufumbuzi hadi pale katiba mpya itakapokuwa imepitishwa.......upo uhaja wa kuangalia upya uwajibikaji wa watoa haki unaunganishwa na wadai haki ambao ni raia...........mfumo uliopo unawafanya watoa haki kuwa na viburi na kufanya watakavyo na hivyo kuongeza mrundikano wa kesi kwenye mahakama zetu............................

  Watakapoanza kuwajibika kwa wadai haki kwa kupitia uwakilishi Bungeni sehemu kubwa ya matatizo ya utoaji haki yatapungua...................Hoja za kuborehsa masilahi na miundo mbinu pekee bila ya kuaanisha upya suala zima la uwajibikaji tutakuwa tunatwanga maji kwenye kinu............gharama zitaendelea kuwa kubwa bila ya mafanikio yoyote yale............
   
 3. akajasembamba

  akajasembamba Senior Member

  #3
  Jan 2, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 161
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kwa kweli tumeona mahakama zikiboreshwa kwa kuanzia na iliyopo CHALINZE!
   
Loading...