Mahakama yazuia wakazi wa Kipawa kuhamishwa

Ng'wanza Madaso

JF-Expert Member
Oct 21, 2008
2,268
333
Na Hellen Mwango
20th November 2009

Mahakama ya Wilaya ya Ilala, Kitengo cha Ardhi, imetoa amri ya kuzuia kwa muda hatua yoyote ya kuwaondoa wakazi 22 waliolipwa fidia eneo la Kipawa jijini Dar es Salaam.

Hatua hiyo imekuja kutokana na Mamlaka ya Uwanja wa Ndege (TAA) kutoa siku 45 kwa wakazi hao wawe wamehama baada ya kulipwa, lakini wao wanasema hazitoshi kuwawezesha kuhamia katika viwanja walivyotengewa eneo la Pugu.

Wakazi hao pia wanasema kuwa sio rahisi kwao kuhama kwa kuwa baadhi yao hawajapokea hata hizo hundi zenyewe za malipo ya fidia.

Katika kufikia uamuzi wa kusitisha uhamishwaji kupitia maombi yao ya dharura, mahakama hiyo pia imezingatia kesi ya wakazi hao ambao wanapinga malipo yao kufanyiwa tathmini kwa mujibu wa sheria ya ardhi ya mwaka 1967 badala ya sheria ya sasa ya mwaka 1997.

Shauri hilo lilisikilizwa na Hakimu Mkazi, Laurian Hemed.

CHANZO: NIPASHE
 
fidia za kijinga nani anakubali wasihame tena wake na mahakama imefanya la maana
 
Huyo hakimu atapona kweli?
Ataundiwa mizengwe na kuhamishwa fasta!

PJ bora uundiwe zengwe uhamishwe, huyo atafutishwa hewa yenye sumu na kufa kifo chema.

All in all watanzania wa kipawa sasa simamieni haki yenu kidete hakuna mchezo hapa.

this govt is so mean, wao wangejenga nini na huto tusent?
 
Tanzania tuna semblance ya separation of powers, this is a plus.

On the negative side mipango ya maendeleo inachukua muda sana kwa sababu ya uzembe, kwa nini wengine hawajapata hizo hundi mpaka leo? Kwa nini watu ambao hawajapata hundi mnawapa siku 45 wahame?
 
Back
Top Bottom