beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,877
- 6,326
Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma, amesema mahakama imejipanga kushughulikia kesi za uchaguzi, endapo zitafunguliwa baada ya uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 28, mwaka huu.
Kadhalika, alisema Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA) Lushoto, kimeshatoa mafunzo kwa majaji wa Tanzania Bara na wa Mahakama Kuu Zanzibar pamoja na Mahakimu Wafawidhi namna ya kushughulikia kesi za uchaguzi na kuandika hukumu.
Kauli hii aliitoa jana jijini Dar es Salaam, wakati akifungua mafunzo kwa wajumbe wapya wa Baraza la Chuo cha Uongozi wa Mahakama yaliyoandaliwa na IJA.
“Maofisa waliopatiwa mafunzo ya kushughulikia kesi za uchaguzi ujao ni pamoja na Majaji wa Mahakama ya Rufani, Jaji Mkuu wa Zanzibar, Majaji wa Mahakama Kuu Tanzania na Zanzibar, Wasajili na Warajisi kutoka Mahakama ya Zanzibar, Mahakimu Wakazi Wafawidhi kutoka Mahakama za Hakimu Mkazi na Wilaya," alisema Jaji Prof. Juma.
Alisema mafunzo hayo yameiweka mahakama ya Tanzania katika utayari wa kuendesha kesi za uchaguzi.
"Kama kutafunguliwa mashauri mbalimbali ya uchaguzi basi, mahakama imejipanga kukabiliana nayo kwani pamoja na mafunzo ya kuendesha mashauri hayo, lakini majaji na mahakimu wamefundishwa namna bora ya uandishi wa hukumu," alisema.
Aidha, alisema chuo hicho kinashiriki vyema katika kuleta mabadiliko makubwa ya kiutendaji yaliyokusudiwa kwenye mahakama kupitia Mpango Mkakati wa Mahakama wa miaka mitano na programu ya maboresho, ili kutimiza dira ya haki sawa kwa wote na kwa wakati.
Jaji Profesa Juma alisema licha ya uwekezaji mkubwa uliofanywa na mahakama katika matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika utoaji haki, bado matumizi yamekuwa madogo kuliko ilivyotegemewa.
"Ingawa uongozi wa mahakama kwa takribani miaka mitatu sasa iliamua matumizi ya TEHAMA kuwa si hiari, lakini kwa bahati mbaya bado matumizi yake ni madogo kulinganisha na uwekezaji mkubwa uliofanywa. Huu ni wakati wa chuo kujiimarisha, ili kitoe mafunzo kwa watumishi wa mahakama kwenye eneo la utoaji haki mtandao," alielezea.
Naye Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Jaji Paul Kihwelo, alisema mafunzo hayo yatafanyika kwa siku mbili na yanalenga kuwajengea wajumbe hao uwezo wa kutekeleza majukumu yao ikiwamo kusimamia utendaji wa chuo.