Uchaguzi 2020 Mahakama yajipanga kwa kesi za Uchaguzi

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma, amesema mahakama imejipanga kushughulikia kesi za uchaguzi, endapo zitafunguliwa baada ya uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 28, mwaka huu.

Kadhalika, alisema Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA) Lushoto, kimeshatoa mafunzo kwa majaji wa Tanzania Bara na wa Mahakama Kuu Zanzibar pamoja na Mahakimu Wafawidhi namna ya kushughulikia kesi za uchaguzi na kuandika hukumu.

Kauli hii aliitoa jana jijini Dar es Salaam, wakati akifungua mafunzo kwa wajumbe wapya wa Baraza la Chuo cha Uongozi wa Mahakama yaliyoandaliwa na IJA.

“Maofisa waliopatiwa mafunzo ya kushughulikia kesi za uchaguzi ujao ni pamoja na Majaji wa Mahakama ya Rufani, Jaji Mkuu wa Zanzibar, Majaji wa Mahakama Kuu Tanzania na Zanzibar, Wasajili na Warajisi kutoka Mahakama ya Zanzibar, Mahakimu Wakazi Wafawidhi kutoka Mahakama za Hakimu Mkazi na Wilaya," alisema Jaji Prof. Juma.

Alisema mafunzo hayo yameiweka mahakama ya Tanzania katika utayari wa kuendesha kesi za uchaguzi.

"Kama kutafunguliwa mashauri mbalimbali ya uchaguzi basi, mahakama imejipanga kukabiliana nayo kwani pamoja na mafunzo ya kuendesha mashauri hayo, lakini majaji na mahakimu wamefundishwa namna bora ya uandishi wa hukumu," alisema.

Aidha, alisema chuo hicho kinashiriki vyema katika kuleta mabadiliko makubwa ya kiutendaji yaliyokusudiwa kwenye mahakama kupitia Mpango Mkakati wa Mahakama wa miaka mitano na programu ya maboresho, ili kutimiza dira ya haki sawa kwa wote na kwa wakati.

Jaji Profesa Juma alisema licha ya uwekezaji mkubwa uliofanywa na mahakama katika matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika utoaji haki, bado matumizi yamekuwa madogo kuliko ilivyotegemewa.

"Ingawa uongozi wa mahakama kwa takribani miaka mitatu sasa iliamua matumizi ya TEHAMA kuwa si hiari, lakini kwa bahati mbaya bado matumizi yake ni madogo kulinganisha na uwekezaji mkubwa uliofanywa. Huu ni wakati wa chuo kujiimarisha, ili kitoe mafunzo kwa watumishi wa mahakama kwenye eneo la utoaji haki mtandao," alielezea.

Naye Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Jaji Paul Kihwelo, alisema mafunzo hayo yatafanyika kwa siku mbili na yanalenga kuwajengea wajumbe hao uwezo wa kutekeleza majukumu yao ikiwamo kusimamia utendaji wa chuo.
 
Mahakama gani hizo za CCM, huyo mteule wa jiwe nani atamuamini? safari hii haki itapatikana hapo hapo uwanjani wapinzani wasijidanganye kusubiri haki kwenye hizi mahakama za jiwe.

Unless Lissu ndie awe Rais.
 
Nakuhakikishia atayetaka kupewa hakiyake kwenye kituo cha kupigia kura na si mahakamani atapewa hapohapo bila kusita, jeshi la polisi ndio lenye haki ya kutoa haki kwa wale wanao fikiri mahakama zinachelewa kutoa haki.
 
Kesi nyingi zingeepushwa kama mahakama isingekubali kuwarudisha wakurugenzi kama wasimamizi Kwa kigezo kwamba wamekula kiapo. Lakini uwepo wa kesi ndio neema Kwa mahakama anyway
 
Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma, amesema mahakama imejipanga kushughulikia kesi za uchaguzi, endapo zitafunguliwa baada ya uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 28, mwaka huu.

Kadhalika, alisema Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA) Lushoto, kimeshatoa mafunzo kwa majaji wa Tanzania Bara na wa Mahakama Kuu Zanzibar pamoja na Mahakimu Wafawidhi namna ya kushughulikia kesi za uchaguzi na kuandika hukumu.

Kauli hii aliitoa jana jijini Dar es Salaam, wakati akifungua mafunzo kwa wajumbe wapya wa Baraza la Chuo cha Uongozi wa Mahakama yaliyoandaliwa na IJA.

“Maofisa waliopatiwa mafunzo ya kushughulikia kesi za uchaguzi ujao ni pamoja na Majaji wa Mahakama ya Rufani, Jaji Mkuu wa Zanzibar, Majaji wa Mahakama Kuu Tanzania na Zanzibar, Wasajili na Warajisi kutoka Mahakama ya Zanzibar, Mahakimu Wakazi Wafawidhi kutoka Mahakama za Hakimu Mkazi na Wilaya," alisema Jaji Prof. Juma.

Alisema mafunzo hayo yameiweka mahakama ya Tanzania katika utayari wa kuendesha kesi za uchaguzi.

"Kama kutafunguliwa mashauri mbalimbali ya uchaguzi basi, mahakama imejipanga kukabiliana nayo kwani pamoja na mafunzo ya kuendesha mashauri hayo, lakini majaji na mahakimu wamefundishwa namna bora ya uandishi wa hukumu," alisema.

Aidha, alisema chuo hicho kinashiriki vyema katika kuleta mabadiliko makubwa ya kiutendaji yaliyokusudiwa kwenye mahakama kupitia Mpango Mkakati wa Mahakama wa miaka mitano na programu ya maboresho, ili kutimiza dira ya haki sawa kwa wote na kwa wakati.

Jaji Profesa Juma alisema licha ya uwekezaji mkubwa uliofanywa na mahakama katika matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika utoaji haki, bado matumizi yamekuwa madogo kuliko ilivyotegemewa.

"Ingawa uongozi wa mahakama kwa takribani miaka mitatu sasa iliamua matumizi ya TEHAMA kuwa si hiari, lakini kwa bahati mbaya bado matumizi yake ni madogo kulinganisha na uwekezaji mkubwa uliofanywa. Huu ni wakati wa chuo kujiimarisha, ili kitoe mafunzo kwa watumishi wa mahakama kwenye eneo la utoaji haki mtandao," alielezea.

Naye Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto, Jaji Paul Kihwelo, alisema mafunzo hayo yatafanyika kwa siku mbili na yanalenga kuwajengea wajumbe hao uwezo wa kutekeleza majukumu yao ikiwamo kusimamia utendaji wa chuo.
Huyu jaji si lolote si chochote. Kwa uwoga wake, amelazimishwa kuwa kada mwaminifu wa CCM. Huyu kama alivyo mahela, anashiriki vikao vya siri vya ccm. Bashiru hukutana mara kwa mara na huyu bwana kwaajili ya mikakati ya kuhujumu haki za watu kupitia uchochoro wa mahakama. Huyu ndiye aliyeharibu mamlaka ya mhimili wa mahakama.

Lililo jema ni kuwa jamii ya kimataifa inafahamu vizuri sana alivyouvuruga mhimili wa mahakama kwa matakwa ya chama na serikali. Kuna siku atajibu.

Kwa hali ya sasa, mahakama sahihi, ya haki na ya kweli ni umma wenyewe. Wananchi wasiwasikilize hawa makada wa ccm wanaitumia mifumo mbalimbali iliyostahili kuwa huru, kuinufaisha CCM.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna kujipanga, anayepanga ni Jiwe na siyo Ibrahim! Hukumu zote zinatolewa na Jiwe kama atakuwa ndiye Rais. Kama atakuwa Lisu, basi Mahakama itatoa hukumu na si Lisu
😄😄😄😄 Siasa bwana.
 
Eti jaji anafundisha namna ya kuandika uhukumu!!! Alikuwaje jaji sasa kama hajui kuandika hukumu? Hizo si kozi za mahakimu vijana? Tanzania bwanaaa…!
 
Back
Top Bottom