Mahakama yaita mashahidi katika kesi ya Ole Sabaya

Kinuju

JF-Expert Member
Mar 20, 2021
2,390
5,310
Gazeti la Nipashe la leo limeinukuu mahakama ikisema kwa sasa ipo tayari kupokea ushahidi kutoka kwa wote waliobakwa na kuteswa na Lengai Ole Sabaya alipokuwa mkuu wa wilaya ya Hai.
===

Hakimu wa Mahakama hiyo, Salome Mshasha, alitoa agizo hilo jana mahakamani huko baada ya kushindikana kusikilizwa kwa shauri hilo kutokana na Upande wa Jamhuri kushindwa kuwafikisha mahakamani mashahidi ili kutoa ushahidi.

“Hakuna haja ya kupoteza muda, kwa ufupi ninaagiza mashahidi waletwe na wafike mahakamani na tarehe ya kusikilizwa kwa shauri ipangwe bila ya kupoteza muda na tuache maneno mengi. Kwa kuwa ninyi ni wanasheria, mnafahamu sheria zinasemaje," Hakimu Salome aliagiza.

Akizungumza mahakamani huko, Wakili wa Serikali, Tarsila Gervas, alidai shauri hilo lilikuwa mbele ya mahakama hiyo jana kwa ajili ya kusikilizwa, lakini shahidi wa Upande wa Jamhuri alishindwa kufika mahakamani.

Kutokana na kutokuwapo kwa shahidi huyo, Wakili Gervas aliiomba mahakama kupanga tarehe nyingine ya kusikilizwa kwa shauri hilo la jinai namba 66.

Mawakili watano wa Upande wa Utetezi, Dankan Oola, Mosses Mahuna, Silvestar Kahunduga, Fredoline Gwemelo na Geston Justine, walidai wanataka waelezwe mahakamani idadi ya mashahidi ambao Upande wa Jamhuri umeandaa.

"Ikikupendeza Mheshimiwa Hakimu, kama tungeambiwa kuna mashahidi wawili au watatu siku ile ya kwanza, cha kushangaza sasa hivi mashahidi ndiyo wanatafutwa kwa njia ya kuiomba mahakama kuandikiwa barua ya wito wa kufika mahakamani kutoa ushaidi. Hii ina maana gani?

"Kwa kuwa kesi ilitakiwa kusikilizwa kwa madai kwamba shahidi amepata udhuru, ninaomba tusianze kupotezeana muda mapema hivi.

"Sisi tulijiandaa kwa ajili ya kusikilizwa kwa kesi lakini tunaambiwa shahidi tuliyemtegemea amepata udhuru, inawezekana mtu mmoja kuikwamisha mahakama hii isifanye kazi.

"Kwa hiyo tunaomba wakati mwingine kitu kama hiki kisitokee na watueleze mashahidi wapo wangapi na kama wana uthibitisho," alidai Wakili Oola.

Wakili wa Serikali, Gervas, alidai namna ya kuwafikisha mahakamani mashahidi ni jukumu lao wenyewe wenye kesi, hivyo hawawezi kuelekezwa siku ya kuwapeleka mahakamani.

"Nimesikiliza malalamiko na madukuduku ya mawakili wa upande wa utetezi kuhusu Jamhuri kushindwa kumleta shahidi mahakamani.

"Pia ninapenda kuiambia mahakama yako kuwa tumesikiliza hoja zao na wakati mwingine tutawaleta mashahidi hao, lakini namna gani ya kuwaleta ni jukumu letu kwa kuwa sisi ndiyo wenye kesi na hata tukiwa nao 20, hawawezi kutuelekeza tuwalete wote kwa siku ambayo wanataka wao kwa kuwa suala la haki ni la pande zote mbili," alidai Gervas.

Hakimu Salome baada ya kusikiliza hoja za pande mbili, aliahirisha shauri hilo hadi Julai 16, mwaka huu litakapokuja kwa ajili ya kusikilizwa kwa ushahidi wa Upande wa Jamhuri.

Katika hatua nyingine, mahakama hiyo ilisikiliza shauri la uhujumu uchumi linalomkabili Ole Sabaya na wenzake.

Katika kesi hiyo aliunganishwa na washtakiwa wengine wawili ambao ni mshtakiwa namba sita, Jackson Macha (29) na wa saba Nathan Msuya (31), wote wakazi wa Moshi mkoani Kilimanjaro.

Jana, ilikuwa mara ya tatu kwa Ole Sabaya na wenzake kupandishwa kizimbani wakikabiliwa na makosa matano ya uhujumu uchumi, rushwa, kuongoza genge la uhalifu, utakatishaji wa fedha na unyang’anyi wa kutumia silaha.

Mbali na Ole Sabaya, washtakiwa wengine ni pamoja na msaidizi wake wa karibu Silvester Stanslaus, Enock Togolani, John Odemba, Daniel Gabriel na Waston Mwakomange.
 
Makosa mengi ya Ole Sabaya ni ya kiutendaji. Mahakama ikiona vyema imfunge mwaka mmoja kifungo cha nje, maisha mengine yaendelee.
 
Kama uliibia watu watatu, ukaua wawili na kubaka wanne sehemu tofautitofauti lazima mashahidi wawe wengi kulingana na matukio yote hayo.

Pia hata kama mashtaka ni mawili kunaweza kuwa na mashahidi kumi
 
kimantiki inaruhusiwa mashahidi zaidi ya hapo? maana sjaelewa hawa wanajitokeza au wanaitwa..?
Hawa tayari walishatoa maelezo polisi....
Ili uqualify kama shahidi ni lazima utoe maelezo/ushahidi wako polisi kwanza....
huwezi kuitwa kama shahidi kama hukutoa maelezo polisi
Waendesha mashtaka ndio wanaamua nani wamuite nani wamuache wanaweza kuita idadi yoyote ile
 
Hawa tayari walishatoa maelezo polisi....
Ili uqualify kama shahidi ni lazima utoe maelezo/ushahidi wako polisi kwanza....
huwezi kuitwa kama shahidi kama hukutoa maelezo polisi
Waendesha mashtaka ndio wanaamua nani wamuite nani wamuache wanaweza kuita idadi yoyote ile
NA VIPI KAMA IDADI YA MASHAHID WALIOHOJIWA POLISI HAWAFIKI 3?
 
Hakimu huyo sabaya unasumbuka naye bure,muachie huru aingie mtaani ,Kama aliyemteua na kubariki uhuni wake aliondoka basi na yeye muda ukifika ataondoka.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom