Mahakama yaingilia Bunge kuzuia suala la Escrow lisijadiliwe!

Hii imo humuhumu ndani, Mahakamani hakuna kesi ya kuchotwa kwa mabilioni ya walipakodi wa nchi hii. Mahakamani hakuna kesi ya kwamba mabilioni husika yalichotwa kinyume cha sheria na taratibu za nchi hii. Mahakamani hakuna majina ya vigogo wa serikali na wengineo waliofaidika na mabilioni hayo haramu yaliyochotwa BOT.Mahakamani hakuna maazimio ya Bunge kufanywa ukaguzi kupitia CAG na TAKUKURU. Mahakamani hakuna PAC. Mahakamani hakuna Kamati ya Uongozi ya Bunge.Mahakamani hakuna kiti cha Spika.


Nb. kama umechukua hela ili upotoshe bora urudishe.

Mahakamani kuna kesi ya IPTL kumshtaki KAFULILA tu
 
Ni wazi sasa serikali imechanganyikiwa Na hii scandal.wakati waziri mkuu anaagiza mkaguzi pamoja Na pccb. Kufanya uchunguzi hakujua matokeo yake? Na je mahakama kuu walikuwa wapi wakati huo? Hapa wana tapatapa Tu.mwisho utajulikana .
 
CAG ndiye kachemka! Kabeba mambo yaliyoko kwenye mafaili mahakamani na kuyapeleka bungeni.

Walichotaka kujadili bungeni ni mambo ya mahakamani ambayo mmbeya mkubwa CAG kayabeba kwa kuyanyofoa kwenye mafaili ya mahakama na kupeleka bungeni.

Hata swala la kusema nani sijui kapewa anayeweza kuthibitisha ni mahakama sio CAG au bunge!

POLE SANA.Kuna methali inasema .............USILOLIJUA NI SAWA NA USIKU WA KIZA.CAG ana mandate ya kufanya INVESTIGATION na ndicho alichokifanya.Mtafute basi hata Internal Auditor wako akusaidie japo kidogo kukupa back ground ya kazi za CAG.
 
Hatujadili maamuzi ya mahakama hapana ila tunataka kujua pesa hizo usahihi wake ni upi na mbna tunajitia upofu
 
Mahakama haizuii bunge bali kujadili suala lililopo mahakamani ni kuingilia uhuru wa mahakama, na kuathiri utoaji wa haki katika suala hilo.
_Nchini hapa chombo cha haki ni Mahakama.wapo watu hupenda kutumia njia zinazowalinda au kuwapatia umaarufu.tuwaepuke.Mahakamani kila mmoja analazimika kusema ukweli.tutii mahakama zetu
 
Simiyu YetuMtazamo wangu mahakama wako sahihi kwamba jambo hili walikuwa wameliamua wao tena mahakama kuu iweje leo bunge wajadili maamuzi ya mahakama? Kama suala lipo mahakamani iweje hiyo pesa kwenye account ya escrow ikatolewa wakati kesi ya msingi ipo mahakamani?huoni kuna tatizo hapo?
Japo mi sio mwanasheria ila HII IMENIVUTIA SAAAN.YAAN KESI IKO MAHAKAMANI KUHUSU ACCOUNT AMBAYO ILISHAFUNGWA na hela hazimo? Kwa hiyo hiyo kesi ni kwa objective ipi?Na wanao taka kuhoji ziligawanywaje wanaingilia mahakama. pliz lawyers tell us sie layman imekaaje hii? Jamani sheria ngumu saaaana kwa ma leyman kama sisi.
 
Labda kazomewa babayako ila pm hatujaona wakati anazomewa au wewe ulikuwa unaangalia bunge gani.

Inaelekea unachangia huku ukiwa hujui unachokitetea, kama unakifahamu basi umeamua kutumia defence mechanism ya Fisi.Akikurupushwa cha Kwanza huachia UHARO! Ndicho unachokifanya!
 
Ninachofahamu ingawa si mtaalamu wa sheria, hii mihimili mikubwa mitatu katika nchi kila mmoja hujitegemea na haiingiliani, ni jambo la kushangaza na kutoeleweka mahakama kuandikia bunge barua kuzuia kujadili tukio la kashfa ya pesa za umma. Kama si kuchanganyikiwa sasa naona wanaenda nje ya taratibu za kisheria zinazoongoza mihimili muhimu nchini.
 
Tutarajie nini tena kama siyo kuvunjwa kwa baraza zima la mawaziri wa muungano ?
Yangu BAOBAO ni kutazama sinema hii !
 
Last edited by a moderator:
Tindu lisu mh naibu spika akuna kanuni yeyote inayozuiya bunge lako kujadili huu wizi wa escrow ccc, mh naibu spika katika sheria ninanozujua mm akuna sheria yeyeto inayokataza wizi huu kujadiliwa bungeni, labda sheria ambazo mimi sizijui, mh naibu spika ukifanya vizuru utakubukwa kwenye uongozi wako wa bunge na kuandikwa kwenye historia kama spika wa bunge la tisa samweli sitta kwenye wizi wa rich mond, usikubali kutumika kama toeti pepa ya kusafisha wizi wa pesa za watanzania
 
Kupitia hatua ya waziri mkuu na mwanasheria mkuu wa serikali kufanya jitihada za kuzuia kashfa ya Escrow isijaliwe na Bunge,kuna haja ya kupiga kura ya kutokuwa na imani na waziri mkuu. Naomba suala hili lianzie Bungeni then lihamie uraiani. Hatuwezi kuvumilia ushe..nzi na upuuzi wa namna hii. Haiwezekani pesa waibe halafu wakatae ripoti isijadiliwe.
 
Ccm bwana. Ukoo wa panya nimeshangaa sana asubuhi Pinda akijibu ,aswali ya papo kwa papo anasema hata yeye ni mwana sheria hivyo mahakama isiingiliwew. Kasahau kwamba hata bunge ni muhimili usiinghiliwe. Mahakama ina haki gani ya kuli pangia bunge kazi??? Pinda saa nyingine anafanana na jina lake. Watanzania tunataka kuaminishwa na hii ripoti kama kweli Mh Kafulila ni tumbili na Mh Zitto ni mpuuzi. Maneno ya Maswi na Warema. Au je ni kweli kwamba yale Mh Kafulila aliyoyasema ni vipeperushi vya kufungia maandazi kama rafiki yangu mtaalamu wa dharau Muhongo alivyo tuambia.

Tujiulize hivi hawa wanaotetea huu wizi wana maslahi gani kwenye hili??
 
Back
Top Bottom