Mahakama yaingilia Bunge kuzuia suala la Escrow lisijadiliwe!

Asubuhi niliwaeleza kuwa serikali ya CCM kupitia Mwanasheria mkuu na Waziri mkuu wapo kwenye mchakato mkubwa wakuzuia ripoti ya wizi wa Escrow isijadiliwe na bunge.

Sasa, jioni hii baada tu ya kuahirishwa bunge kiutatanishi, na kikao cha UKAWA kuisha, Katibu mkuu kiongozi Ombeni Sefue amewasilisha rasmi barua ya mahakama inayozuia mjadala wowote wa Esrow account katika bunge hili,

Ujio wa Sefue Bungeni na barua hii umetafsiriwa kuwa ofisi kuu nchini inatambua na kwa mamlaka iliyonayo imeinjinia kile kinachoitwa zuio la mahakama dhidi ya wizi huu unaotikisa nchi.



Sijui hii jeuri inatoka wapi eti zuio la mahakama.
Kama hili hapa chini ipo Kikatiba kwamba Mahakama haina meno/ mamlaka ya kumwadabisha Binadamu mmoja yaani mtendaji /ofisa wa Serikali mwenye kushindwa kutekeleza- articles 8 and 9 ya Katiba yetu ,leo hii uwezo na mamlaka ya Mahakama kusimamisha shughuli ya Bunge umetoka wapi?



However, it is important to note that both articles 8 and 9 are in Part II of Chapter One, headed ‘Fundamental objectives and directive principles of state policy’.

Article 7(2) of the Constitution specifically provides that the provisions of this Part are not enforceable by a court, and no court may determine whether any act or omission by any person complied with the provisions of this Part. The effect of this is that no one can be held to account for failure to comply with the founding

principles enunciated in Part II of Chapter One.







UPDATE:


- Zitto anasema kuwa Suala hili linachora mstari wa uvumilivu wa watanzania kwa Serikali
- Zitto anasema jambo hili (kuzuia Bunge lisifanye kazi yake) linaweza kutokea kwenye nchi isiyokuwa na Dola
- Zitto anasema umefanywa kila ubabe, kila aina ya maneno/matusi kuhakikisha suala hili halijadiliwi Bungeni lakini njia pekee ya kulimaliza hili ni kuwa na mjadala wa wazi Bungeni.

- Zitto anasema PAC ipo tayari wakati wowote watapohitajika kuwasilisha ripoti Bungeni watapohitajika. Anataka wanaotaka kupinga suala hili wasubiri ziletwe facts
- Waziri Mkuu, Mizengo Pinda anasema Mihimili Mitatu yote ipo kwa mujibu wa Katiba. Anasema ameogopa kuona Bunge likidai Mahakama inajaribu kuficha uozo
- Pinda anasema lazima busara kubwa itumike kuhakikisha maamuzi yanayofanywa na Bunge yasionekane kuingilia Mhimili mwingine (Mahakama) hivyo ni jukumu la Spika kutumia busara kila Mhimili unatekeleza jukumu lake inavyotakiwa (ANAZOMEWA)
- Ndugai anasema wao Wabunge kama viongozi hawawezi kuwa na umoja katika kutetea maovu. Anasema hekima itatumika
- Ndugai anasema haki itatendwa na Bunge, ushauri wa Pinda umepokelewa

Mhe. Zitto acheni kulalamika kama tunavyolalamika sisi wananchi tulioko huku Nje ya Bunge na mwisho wa siku mtakuwa kama wale wa Bukina Faso!
Kwa serikali kushindwa kutekeleza majukumu lake ni kosa la kiutendaji na namna Bora kwa Bunge ni kuzua hoja ya Kutokuwa na imani na Waziri Mkuu au hata Mkuu wa Nchi,kwa maana hiyo hakuna haja ya kulalamika chukueni hatua.

Kama Ikulu imediriki kutumia Mahakamani ni wazi haiko tayari kutimza majukumu yake na kwa maana hiyo inaingilia Uhuru wa mihimili nyingine-vigumu kwa namna yoyote ile kwa eti Bunge lisitimize majukumu yake eti Kisa hoja au suala husika liko mahakamani-kesho kichaa atafungua Kesi mahakamani kuaitaka lisitishe vikao vya Bunge au Ikulu sitishe kutimiza majukumu yake.

Waheshimiwa wabunge amkeni na chukueni hatua na hili linawezekana,na si kwa faida ya kisiasa bali kwa ustawi wa jamii kwa 50 yrs ijayo.

[h=3]Mfano upo;
zitto ataka saini za wabunge 70 kumng'oa,mawaziri watano ...
[/h]
 
Last edited by a moderator:
Pinda kazomewa na wabunge, baada ya swala la ESCROW kuwa la moto kwake....Hahahahaha na bado nasikia muda huu yuko kwenye gari analia
 
Roho inaniuma mm... ukizingatia watu huku tunateseka alaf wanajizolea mabilioni ya hela kwa lazima... wanazima hii issue wachukue hizo hela kimya kimya... wanazuiaje issue kama hii watu tulikua tunasubiri kwa hamu? Duuuh... R.I.P Tanzania...
 
Simiyu YetuMtazamo wangu mahakama wako sahihi kwamba jambo hili walikuwa wameliamua wao tena mahakama kuu iweje leo bunge wajadili maamuzi ya mahakama? Kama suala lipo mahakamani iweje hiyo pesa kwenye account ya escrow ikatolewa wakati kesi ya msingi ipo mahakamani?huoni kuna tatizo hapo?
 
Nashangaa kuna kipindi mlikuwa mnamtukana sana
Hapana sio kweli, ukifuatilia post zangu huyu jamaa nimeshawahi kumzungumzia mahali kuwa ni mtu anayefaa kwa kuwa anayo maamuzi. Aaamui kwa kuwa watu fulani wanataka nini, Ni kiongozi wa kweli.
 
Mahakama haina mamlaka ya kulizuia bunge kufanya shughuli zake ikiwa ni pamoja na kujadili report ya uchunguzi wa wizi wa Escrow. Isitoshe barua ya mahakama haiwezi kupelekwa na katibu mkuu kiongozi kwani si mtendaji wa mahakama wala mtumishi wa bunge. Kuna vitu havijakaa sawa kwenye taarifa yako kaka.

kilichoripotiwa na kaka ni kweli kabisa na yeye hajaongeza neno ndivyo hivyo ilivyo lakini kesho itaendelea kama mbinu hiyo ya kuzuia imefanikiwa au laah.... nawabunge wameishangaa mahakama kuingilia shughuli za bunge na mwisho ndugai akasema anamnukuu sitta wakati yupo kwenye kiti kwamba hatuwezi kuunda umoja kwenye uovu nabusura kubwa itatumika kuridhisha wote kuanzia wabunge hadi sisi raia.
 
Labda kazomewa babayako ila pm hatujaona wakati anazomewa au wewe ulikuwa unaangalia bunge gani.
 
Leo bunge limeonesha uhai mkubwa kuweza kushikamana katika suala, sante sana ndugai kwa kutumia hekma ya kiti kuwapa wabunge wachaingie hili suala. Lazma iletwe bungeni atajulikana tumbili ni nani.
 
UKAWA hawawezi kudeal na hii ishu kwa dhati kwa sababu kuna viongozi wawili wa upinzani wanahusishwa na ufisadi wa Escrow

Kwa hiyo UKAWA washawishike kwa kuwa hao viongozi wawili waliohusika na kashfa ya Escrow?
Labda unambie UKAWA ni hao wawili waliohusika na huo wizi, Otherwise UKAWA hawawezi kuwa wajinga kutetea watu wawili wakati jambo hilo litaiathiri UKAWA nzima.

Ni vema pia kama wapo hao viongozi wawili wa UKAWA waliopata huo mgao wawekwe wazi ili mwisho wa UKAWA ibaki safi.
 
Mtazamo wangu mahakama wako sahihi kwamba jambo hili walikuwa wameliamua wao tena mahakama kuu iweje leo bunge wajadili maamuzi ya mahakama?

Siku zote hizo mpaka report imekabidhiwa bunge mahakama ilikuwa wapi? haijasema? ndo mana tunasema Pinda na Warema walikuwa bizzy kuandaa mikakati namna gani watanusurika mana mahkama ndio kimbilio la ccm ukoo wa panya
 
Wengine tuliposikia jaji mkuu kaenda kumsalimu mgonjwa wa tezi dume tukaanza kujihoji kulikoni!
 
Back
Top Bottom