Papaa Mobimba
JF-Expert Member
- Jan 27, 2018
- 754
- 3,097
Wanasheria wa Mwandishi wa habari za Kichunguzi, Erick Kabendera wamewasilisha maombi maalum katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutaka mteja wao afikishwe Mahakamani ama Polisi imuachie leo
Mahakama hiyo imeridhia maombi hayo na kuitaka Polisi kama bado itakuwa ikimshikilia Mwandishi huyo aliyekamatwa tangu Julai 29, 2019 kumfikisha Mahakamani hapo kesho majira ya saa 3:00 asubuhi
Kabendera aliyekamatwa kwa nguvu na Polisi akiwa nyumbani kwake, anashikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Barabara ya Kilwa jijini Dar na amekuwa akihojiwa kuhusu uraia wake tangu hapo
UPDATE;
Idara ya Uhamiaji imetolea ufafanuzi suala la kukamatwa na kuhojiwa kwa Mwandishi wa habari za Kiuchunguzi, Erick Kabendera aliyekamatwa Julai 29, 2019
Wamebainisha kuwa wapo naye na Walimkamata kwa ushirikiano wa Polisi na kudai kuwa wanamuhoji na kuachiwa kwake itategemea na ushirikiano atakaoutoa kwao
Jana, Kamanda Mambosasa alisema wamemkamata Kabendera na kuwa wanamuhoji na wapo naye katika Kituo cha Polisi anachosimamia yeye
Leo asubuhi ndugu zake walipata wasaa wa kuweza kuonana naye akiwa katika Kituo cha Polisi cha Barabara ya Kilwa jijini Dar