Mahakama ya Mafisadi kumfunga nani?

Mahakama ya Mafisadi kumfunga nani?

Ushahidi usio na mashaka. Mimi nadhani wanasheria wa serikali sio wajanja sana (kuna kesi ya mauaji Ilikuwa na miaka 10) ukilinganisha na mawakili wa kujitegemea ambao nia yao kuu ni kushinda kesi. Bora kumpata mtu kwa kidogo chenye ushahidi thabiti kuliko kwa makubwa ambayo utashindwa kuyatetea. Sio tu mahakimu wanaoweza kununuliwa hata mashahidi na waendesha mashitaka nk.

Ninavyohisi mahakama hizo zitasimamiwa na wanaojua sheria zinazohusu ufisadi, rushwa na uhujumu uchumi vizuri. Pengine kuna wanaonolewa sasa hivi. Naona bunge hili litatilia mkazo uboreshwaji wa jela.

Kuhusu kurejeshwa kwa pesa itategemea huyo mtu aliinvest wapi. Kuna wale ambao wanadaiwa Bil. 18, property zao zilizoshikwa ni Bil 6 na baada ya mnada inawezekana kabisa hata hiyo 6 isipatikane. Utaratibu wa account na property za nje ya nchi siufahamu.
Rushwa katika nchi hii ni kila mahali. Wala tusijidanganye kwa kufikiri kwamba majaji wa serikali siyo wazuri kwa kuitetea serikali, hapa ni rushwa na inawezekana baadhi yao wanashiriki katika kuhakikisha wanashindwa ili wapate chochote na sijui kama kuna incentive yoyote wanapata kwa kushinda kesi zaidi ya mshahara ambao kimsingi ndo haki yao. Baadhi ya mawakili binafsi wanaweza kuwa wahongaji wakubwa, na kwa hivyo ni wazi lazima muda wote washinde. Saa ingine serikali ichukue baadhi ya kesi zake na izikabidhi kwa mawakili binafsi kwa makubaliano manono kidogo zaidi ya commission wanayopata toka kwa watu binafsi ili tuone matokeo yake. Lakini vile vile hao mawakili wa serikali wahusishwe kuanzia stage za awali hasa kwenye kesi zenye maslahi na taifa ili ziandaliwe katika mazingira rahisishi kuishinda. Lakini pia wanaweza kuwa assessed kila wakati ili kujua uwezo wao.
 
Mimi pia nahisi hamna jipya litalofanywa juu ya mafisadi wa nchi hii. Mahakama yenyewe ni very corrupt!

Nilichojifunza mpka sasa ni kuwa mtu akiiba pesa ndefu, hakuna wa kumgusa nchi hii. Ila ukiiba vihela vya kununulia Sayona utapelekwa ngome miaka 30 haraka sana kama yule mtumishi wa Ikwiriri.

Everyone has his/her price. Kila mtu ananunulika nchi hii. Kwa jinsi figisu zinavyofanywa nchi hii, the message ni kwamba piga mkwanja mrefu then Mahakama zetu zitakutetea vizuri tu, utafutiwa mashtaka ama utafungwa mwaka mmoja tu ili kuzuga.

Narudia, hamna jipya nchi hii kuweza kuyathibiti mafisadi!

Tanzania bado sana kuweza kutetea na kulinda maslahi ya umma. Mahakama, Police, na TAKUKURU ndo wanaotuangusha katika vita ya ufisadi.
 
Kama akina Masamaki, Kitilya, Sioi au siyo?

kwani hao wamefungwa? muhando kisha washa green light kesi ya utakatishaji ishaota mbawa kimoja komoja kinachomoka mwisho wa siku wapo mtaani kukurupuka na mizuka kubaya.
 
Serikali ya mazingaombwe wanatuzingua tu ninaamini kama kweli mahakama hiyo itafunguliwa na ikafanya vizuri basi 80% itabidi wafungwe mana serikali hii wengi ni vibaka
 
Ushahidi usio na mashaka. Mimi nadhani wanasheria wa serikali sio wajanja sana (kuna kesi ya mauaji Ilikuwa na miaka 10) ukilinganisha na mawakili wa kujitegemea ambao nia yao kuu ni kushinda kesi. Bora kumpata mtu kwa kidogo chenye ushahidi thabiti kuliko kwa makubwa ambayo utashindwa kuyatetea. Sio tu mahakimu wanaoweza kununuliwa hata mashahidi na waendesha mashitaka nk.

Ninavyohisi mahakama hizo zitasimamiwa na wanaojua sheria zinazohusu ufisadi, rushwa na uhujumu uchumi vizuri. Pengine kuna wanaonolewa sasa hivi. Naona bunge hili litatilia mkazo uboreshwaji wa jela.

Kuhusu kurejeshwa kwa pesa itategemea huyo mtu aliinvest wapi. Kuna wale ambao wanadaiwa Bil. 18, property zao zilizoshikwa ni Bil 6 na baada ya mnada inawezekana kabisa hata hiyo 6 isipatikane. Utaratibu wa account na property za nje ya nchi siufahamu.
Asante kwa hoja yako mkuu! Nimekuelea angalao na hiyo ndio hoja sio wajinga wajinga wasioju lolote zaidi ya mihemko isomaana.
 
Nashangaa sana hii mijitu sijui uifanyie nini iwe satisfied, kuweni na subira muone, I bet the former DPP Jaji Dkt Feleshi aongoze jopo la hiyo mahakama tuone watahonga wapi, kuna majaji wako Iringa wanapikwa mpaka hivi sasa tunavyozungumza.
Mkuu umeanza vibaya ukamalizia vizuri, ni bora mtu kusoma mada ukaelewa na kutoa jibu la hisia zako. Hivi hata kama ni wewe ukiangalia kina Mhando wameachiwa mpaka PCCB wanalalamikia mahakimu na Kina Kitilya wameanza kufutiwa mashtaka, tukae kimya tu? Changia tu hoja tueleweshane utaratibu na sio kuhemka tu.
 
Kama akina Masamaki, Kitilya, Sioi au siyo?
Mbona humtaji Madabida kwa ARVs fake? Wilson Kabwe yuko wapi? Kina mramba wana tumikia miaka mingapi na waliiba kiasi gani?
 
kwani hao wamefungwa? muhando kisha washa green light kesi ya utakatishaji ishaota mbawa kimoja komoja kinachomoka mwisho wa siku wapo mtaani kukurupuka na mizuka kubaya.

Dada hueleweki, mara unauliza wako wapi mara unasema karibuni watakuwa mitaani.

Mbona unajichanganya?
 
Mbona humtaji Madabida kwa ARVs fake? Wilson Kabwe yuko wapi? Kina mramba wana tumikia miaka mingapi na waliiba kiasi gani?

Kumbe unawajuwa contenders wa mahakama ya mafisadi.

Good, mfahamishe mleta mada.
 
kila kitu ni siasa mtu alishapata mtaji wa kura yupo magogoni anakwambia atajenga mahakama za kifisad ajabu na yeye anahusika ktk tairi hilo hilo.
teh teh. fish, ngarawa na nk
 
Waswalihi waliwahi kunena" Nani kumfunga paka kengele?" Hii mahakama kama ni kweli itakuwepo itashughulika na akina nani? Mahakimu na majaji ni hawa hawa wa kwetu au watatoka nchi nyingine?

Wakuu nimeuliza haya kwa kutazama mwendelezo wa kesi mbambali kubwa tena zenye kulitia taifa hasara kubwa za mabilioni, Juzi hapa Kuna aliyekua mkurugenzi wa TANESCO alikutwa hana hatia na kesi kuishia hapo,kuna waheshimiwa flani wako jela kwa hukumu ya miaka single digit juu ya kesi kubwa ya kulisababishia taifa hasa za mabilioni,Wengine leo nasikia kua wameanza kufutiwa mashtaka kwa madai eti shitaka halina uzito wowote, jamani!

Kinachonipa shida ni kwamba kama taifa lilipata hasara ya mabilioni, tunaambiwa mtu hana hata, pesa zimepotea, sasa nani alikula hizo pesa?zilupotelea kwenye mikono ya nani? Nani wa kurudisha hayo mabilioni kama mshukiwa tunaambiwa hahusiki.

Afisa mmoja wa TAKUKURU alisika akilia kwa kusema Mahakama flani imejaa uozo,Sasa swali langu ni kwamba nani atakua msimamizi wa Mahakama ya mafisadi?

Tanzania Tanzania nchi yangu.
Itamfunga Lowasa na mkwe wake. .
 
Dada hueleweki, mara unauliza wako wapi mara unasema karibuni watakuwa mitaani.

Mbona unajichanganya?

hukumu ishatoka? au ukishafika mahakamani ndo ushahukumiwa hapo ndo napata picha jinsi ambavyo mawakili wa serikali wanapo fail ktk kesi zao wanaamini mtu akishafika mahakamani bas kes imeisha kwa hii sampuli yako.
 
Dada hueleweki, mara unauliza wako wapi mara unasema karibuni watakuwa mitaani.

Mbona unajichanganya?

na kumbuka msingi mkubwa wa kesi ushapanguliwa utakatishaji fedha kuna nini hapo?
 
Back
Top Bottom