Mahakama ya Mafisadi kumfunga nani?

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,244
7,970
Waswalihi waliwahi kunena" Nani kumfunga paka kengele?" Hii mahakama kama ni kweli itakuwepo itashughulika na akina nani? Mahakimu na majaji ni hawa hawa wa kwetu au watatoka nchi nyingine?

Wakuu nimeuliza haya kwa kutazama mwendelezo wa kesi mbambali kubwa tena zenye kulitia taifa hasara kubwa za mabilioni, Juzi hapa Kuna aliyekua mkurugenzi wa TANESCO alikutwa hana hatia na kesi kuishia hapo,kuna waheshimiwa flani wako jela kwa hukumu ya miaka single digit juu ya kesi kubwa ya kulisababishia taifa hasa za mabilioni,Wengine leo nasikia kua wameanza kufutiwa mashtaka kwa madai eti shitaka halina uzito wowote, jamani!

Kinachonipa shida ni kwamba kama taifa lilipata hasara ya mabilioni, tunaambiwa mtu hana hata, pesa zimepotea, sasa nani alikula hizo pesa?zilupotelea kwenye mikono ya nani? Nani wa kurudisha hayo mabilioni kama mshukiwa tunaambiwa hahusiki.

Afisa mmoja wa TAKUKURU alisika akilia kwa kusema Mahakama flani imejaa uozo,Sasa swali langu ni kwamba nani atakua msimamizi wa Mahakama ya mafisadi?

Tanzania Tanzania nchi yangu.
 
Ushahidi usio na mashaka. Mimi nadhani wanasheria wa serikali sio wajanja sana (kuna kesi ya mauaji Ilikuwa na miaka 10) ukilinganisha na mawakili wa kujitegemea ambao nia yao kuu ni kushinda kesi. Bora kumpata mtu kwa kidogo chenye ushahidi thabiti kuliko kwa makubwa ambayo utashindwa kuyatetea. Sio tu mahakimu wanaoweza kununuliwa hata mashahidi na waendesha mashitaka nk.

Ninavyohisi mahakama hizo zitasimamiwa na wanaojua sheria zinazohusu ufisadi, rushwa na uhujumu uchumi vizuri. Pengine kuna wanaonolewa sasa hivi. Naona bunge hili litatilia mkazo uboreshwaji wa jela.

Kuhusu kurejeshwa kwa pesa itategemea huyo mtu aliinvest wapi. Kuna wale ambao wanadaiwa Bil. 18, property zao zilizoshikwa ni Bil 6 na baada ya mnada inawezekana kabisa hata hiyo 6 isipatikane. Utaratibu wa account na property za nje ya nchi siufahamu.
 
Nani alisema kuwa wao sio mafisadi? Nina maana baadhi ya majaji. Mbona kashfa ya ESCROW baadhi wamo? Mahakama hii haitakuwa muarobaini bali huenda ikatumika kisiasa zaidi!!!!
 
Hivi Kitilya, Sioi na yule mwenzao wako wapi? Bila kumsahau Masamaki, Kabwe na wenzao?

Hiyo inatowa majibu kwa kichwa cha habari, ujumbe sijausoma.
 
kila kitu ni siasa mtu alishapata mtaji wa kura yupo magogoni anakwambia atajenga mahakama za kifisad ajabu na yeye anahusika ktk tairi hilo hilo.
 
Waswalihi waliwahi kunena" Nani kumfunga paka kengele?" Hii mahakama kama ni kweli itakuwepo itashughulika na akina nani? Mahakimu na majaji ni hawa hawa wa kwetu au watatoka nchi nyingine?

Wakuu nimeuliza haya kwa kutazama mwendelezo wa kesi mbambali kubwa tena zenye kulitia taifa hasara kubwa za mabilioni, Juzi hapa Kuna aliyekua mkurugenzi wa TANESCO alikutwa hana hatia na kesi kuishia hapo,kuna waheshimiwa flani wako jela kwa hukumu ya miaka single digit juu ya kesi kubwa ya kulisababishia taifa hasa za mabilioni,Wengine leo nasikia kua wameanza kufutiwa mashtaka kwa madai eti shitaka halina uzito wowote, jamani!

Kinachonipa shida ni kwamba kama taifa lilipata hasara ya mabilioni, tunaambiwa mtu hana hata, pesa zimepotea, sasa nani alikula hizo pesa?zilupotelea kwenye mikono ya nani? Nani wa kurudisha hayo mabilioni kama mshukiwa tunaambiwa hahusiki?

Afisa mmoja wa TAKUKURU alisika akilia kwa kusema Mahakama flani imejaa uozo,Sasa swali langu ni kwamba nani atakua msimamizi wa Mahakama ya mafisadi?

Tanzania Tanzania nchi yangu.
kama mwanasheria mkuu wa serikali anafukuzwa kazi kwa kushiriki ufisadi pamoja na majaju wakuu kwa kweli hali ni tete kwenye hiyo sector,,espirato santus,,mungu uwalinde maskini
 
Nchi hii cjui usanii utaisha lini ...maana hiyo yote ni kuwatengenezea watu ulaji tu na si vinginevyo
 
Hivi Kitilya, Sioi na kile kihawara chao wako wapi? Bila kumsahau Masamaki, Kabwe na wenzao?

Hiyo inatowa majibu kwa kichwa cha habari, utumbo sijausoma.
Nashangaa sana hii mijitu sijui uifanyie nini iwe satisfied, kuweni na subira muone, I bet the former DPP Jaji Dkt Feleshi aongoze jopo la hiyo mahakama tuone watahonga wapi, kuna majaji wako Iringa wanapikwa mpaka hivi sasa tunavyozungumza.
 
Kila siku wanaandamana kwenda mjengoni;
hiyo mahakama itakuwa ya kufunga waendesha bodaboda na akina mama lishe.
 
Mahakama haijaanza mshaanza kuweweseka subiri ije then uje na maswali yako mkuu
 
Back
Top Bottom