Mahakama ya mafisadi kuanza leo

Mkuu unaposema fisadi mkuu unatuacha hewani kwani katika waliopelekwa mahakamani hatujaambiwa yupi ndio mkuu wao
kulingana na kamusi ya Lumumba,fisadi ni yule alietimukia CHADEMA mwaka jana,na kisha kupewa nafasi ya kugombea kiti cha uraisi 2015!
 
Mamvi naomba awe mshitakiwa wa kwanza kwenye hiyo mahakama, maana yeye ndiyo chanzo cha ufisadi wote.
Ndiyo, sababu yeye anahusika na Meremeta, iptl, escrow, fedha za STANBIC Bank, panton ya Bagamoyo, mabehewa feki, mgodi wa Kiwira..
Huyu ni maarufu kwa kuwa mahakama imeanzishwa kwa ajili yake.
 
Mahakama ya mafisadi IPO pale law school kwa Ku tafuta sifa kwa raisi Yale majengo tuliokua tunayatumia pale lawshool kwa ajili ya mootcourt wameyachukua na kuyabadilisha kuwa hiyo mahakama hii sio sahihi kwa mustakabari wa elimu yetu.
 
wakati wa kampeni za uchaguzi tulisikia habari za wakulima,wafugaji,wavuvi kuboreshewa mazingira yao. baada ya uchaguzi je ni kiasi gani wameboreshewa au angalau wanatajwa?
Walichofanikiwa kufanya ni kudumaza kilimo na biashara.
Mazao yameshuka bei kwa vile hawaruhusiwi kuuza nje ya nchi.
Kenya ni EAC sijui kwa nini tusiuze mchele, mbaazi na mahindi kwa jilani zet??
Wakulima wamedumazwa, wafanya biashara wamedumazwa.
Unategemea ni vipi utakuza uchumi wete??
 
Walichofanikiwa kufanya ni kudumaza kilimo na biashara.
Mazao yameshuka bei kwa vile hawaruhusiwi kuuza nje ya nchi.
Kenya ni EAC sijui kwa nini tusiuze mchele, mbaazi na mahindi kwa jilani zet??
Wakulima wamedumazwa, wafanya biashara wamedumazwa.
Unategemea ni vipi utakuza uchumi wete??

duhh! huku kwetu bakuri la mbaazi lilikuwa limefika kwenye sh2800 lakini majuzi tu baaada ya katazo linauzwa 700/800
 
Mm,kama Lowassa ni fisadi basi sisi CCM ni mafisadi papa.Hivi mbona huwa hatuna aibu ya macho.Ni nani asiyejua jinsi Chama kilivyoshirikiana na mafisadi kuifidi nchi.Mtu aliyetusaidia wakati tulipokuwa tumekabwa koo sasa tumemshupalia kwamba ni fisadi.Asingekubali kupakwa matope kwa niaba yetu si ajabu hata serikali na chama vingesambaratika.Tuwe na shukrani jamani.(QUOTE="Kitulo, post: 16700255, member: 104112"]Hicho ni kitengo kama kilivyo mahakama ya ardhi,biashara nk.
Wewe kaa tayari kusikia mafisadi papa wakianza kupelekwa kwenye mahakama ya mafisadi na wahujumu uchumi akiwemo baba wa ufisadi Tanzania mh.mgombea urais wa kudumu wa Chadema.[/QUOTE]
 
Hicho ni kitengo kama kilivyo mahakama ya ardhi,biashara nk.
Wewe kaa tayari kusikia mafisadi papa wakianza kupelekwa kwenye mahakama ya mafisadi na wahujumu uchumi akiwemo baba wa ufisadi Tanzania mh.mgombea urais wa kudumu wa Chadema.
Asante kwa kumuelewesha, nimesoma post yake kwa fikra zake anajua mahakama ya Mafisadi basi inaitaji jengo lake na iwe tofauti kabisa na judicial system iliyopo sasa. Ni suala la kuongeza kitengo kitakacho simamia kesi za ufisadi "grand corruption".
 
Hahahaha nchi ya kusadikika hii.

"Fairy Tale country"

Kituko zaidi subiri hao watuhumiwa watakaopelekwa, miniscule charges za kuiba vimilioni lakini watavyokuwa paraded kwenye magazeti na tv for publicity stunt.

Cha kushangaza waliotufikisha hapa kwa kuiba matrillioni hutakaa uwaone zaidi watazidi kuvyikwa vyeo.
Ni kweli mkuu naungana na wewe, hii nchi ni ya kipumbavu sana, kutoka kuwa visadi kuu hadi kupewa nafasi ya kugombea Urais, haya ni matusi makubwa sana kwa wahanga wa ufisadi
 
Bila shaka dhana ya "kujenga" inafahamika kwa kila mtu. Kipindi cha kampeni tuliaminishwa kuwa tukiwachagua watajenga mahakama ya mafisadi na kwa kila aliyesikia hili alijenga taswira mahususi kabisa kuwa mahakama hiyo itajengwa kweli na itakuwa tofauti na hizi mahakama tulizonazo kwa sasa.

Leo tunaambiwa mahakama hii itaanza kufanya kazi. Mimi kwa upande wangu sijui mahakama hii imeanza kujengwa na kumalizika lini, na ni wapi mahakama hii imejengwa?

Isijekuwa kesi za mafisadi tunaenda kuzisikilizia palepale kisutu kwenye mahakama tulizozoea kuona wanapelekwa akina Lissu
Wewe unavyosikia kujenga unajua lazima tofali na mchanga vihusike eti....kazi kwelikweli.!!
 
"Tutajenga mahakama ya mafisadi" lands haujui maana ya kujenga ndio maana unalopoka tu
Mkuu najua wewe ni mtaalam wa kiswahili unaweza kunisaidia pale wanasiasa ama viongozi wanapowaambia wananchi "Tujenge Nchi" wanamaanisha tujenge kwa kutumia matofali ya aina gani? ceramic, ya udongo ama cement?? ukiweza kuinjibu hili nitajua kuwa wewe si mnazi wa chama.
 
Back
Top Bottom