Mahakama ya mafisadi kuanza leo

M

Mtarban

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2015
Messages
3,219
Likes
3,588
Points
280
M

Mtarban

JF-Expert Member
Joined Jan 14, 2015
3,219 3,588 280
Bila shaka dhana ya "kujenga" inafahamika kwa kila mtu. Kipindi cha kampeni tuliaminishwa kuwa tukiwachagua watajenga mahakama ya mafisadi na kwa kila aliyesikia hili alijenga taswira mahususi kabisa kuwa mahakama hiyo itajengwa kweli na itakuwa tofauti na hizi mahakama tulizonazo kwa sasa.

Leo tunaambiwa mahakama hii itaanza kufanya kazi. Mimi kwa upande wangu sijui mahakama hii imeanza kujengwa na kumalizika lini, na ni wapi mahakama hii imejengwa?

Isijekuwa kesi za mafisadi tunaenda kuzisikilizia palepale kisutu kwenye mahakama tulizozoea kuona wanapelekwa akina Lissu
 
Kitulo

Kitulo

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Messages
2,379
Likes
2,629
Points
280
Kitulo

Kitulo

JF-Expert Member
Joined Oct 5, 2012
2,379 2,629 280
Hicho ni kitengo kama kilivyo mahakama ya ardhi,biashara nk.
Wewe kaa tayari kusikia mafisadi papa wakianza kupelekwa kwenye mahakama ya mafisadi na wahujumu uchumi akiwemo baba wa ufisadi Tanzania mh.mgombea urais wa kudumu wa Chadema.
 
L

Levictus

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Messages
648
Likes
496
Points
80
L

Levictus

JF-Expert Member
Joined Aug 16, 2014
648 496 80
bila shaka dhana ya "kujenga" inafahamika kwa kila mtu. kipindi cha kampeni tuliaminishwa kuwa tukiwachagua watajenga mahakama ya mafisadi na kwa kila aliyesikia hili alijenga taswira mahususi kabisa kuwa mahakama hiyo itajengwa kweli na itakuwa tofauti na hizi mahakama tulizonazo kwa sasa. Leo tunaambiwa mahakama hii itaanza kufanya kazi. Mimi kwa upande wangu sijui mahakama hii imeanza kujengwa na kumalizika lini, na ni wapi mahakama hii imejengwa? isijekuwa kesi za mafisadi tunaenda kuzisikilizia palepale kisutu kwenye mahakama tulizozoea kuona wanapelekwa akina Lissu
You must be a layman
 
H

herzygovina mwangosi

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2013
Messages
908
Likes
384
Points
80
H

herzygovina mwangosi

JF-Expert Member
Joined Sep 26, 2013
908 384 80
bila shaka dhana ya "kujenga" inafahamika kwa kila mtu. kipindi cha kampeni tuliaminishwa kuwa tukiwachagua watajenga mahakama ya mafisadi na kwa kila aliyesikia hili alijenga taswira mahususi kabisa kuwa mahakama hiyo itajengwa kweli na itakuwa tofauti na hizi mahakama tulizonazo kwa sasa. Leo tunaambiwa mahakama hii itaanza kufanya kazi. Mimi kwa upande wangu sijui mahakama hii imeanza kujengwa na kumalizika lini, na ni wapi mahakama hii imejengwa? isijekuwa kesi za mafisadi tunaenda kuzisikilizia palepale kisutu kwenye mahakama tulizozoea kuona wanapelekwa akina Lissu
Upeo wako sijui unashida gani?Kama umeshindwa at a kunyumbua hili...ulitaka uone wakichukua matofari wanajenga...what's matter was establishment and its division of high court...go beyond your passion na ukeleketwa
 
R Mbuna

R Mbuna

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2015
Messages
1,715
Likes
3,040
Points
280
R Mbuna

R Mbuna

JF-Expert Member
Joined Dec 30, 2015
1,715 3,040 280
Hii mahakama ipo katika nchi ya kusadikika kusini inapakana na aridhi magharibi inapakana na mbingu.
 
G

Godfrey-K

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2016
Messages
1,454
Likes
1,927
Points
280
Age
48
G

Godfrey-K

JF-Expert Member
Joined Jan 5, 2016
1,454 1,927 280
Hicho ni kitengo kama kilivyo mahakama ya ardhi,biashara nk.
Wewe kaa tayari kusikia mafisadi papa wakianza kupelekwa kwenye mahakama ya mafisadi na wahujumu uchumi akiwemo baba wa ufisadi Tanzania mh.mgombea urais wa kudumu wa Chadema.
Hakitakua na majengo? Au kitaendeshwa chini ya mti kama ile shule ya sekondari kisaba
 
mrangi

mrangi

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2014
Messages
30,845
Likes
17,687
Points
280
mrangi

mrangi

JF-Expert Member
Joined Feb 19, 2014
30,845 17,687 280
Hicho ni kitengo kama kilivyo mahakama ya ardhi,biashara nk.
Wewe kaa tayari kusikia mafisadi papa wakianza kupelekwa kwenye mahakama ya mafisadi na wahujumu uchumi akiwemo baba wa ufisadi Tanzania mh.mgombea urais wa kudumu wa Chadema.
Bila kuwasahau wale wa kwa msoga na Yule aliyetuita malofa
 
mpiga domo

mpiga domo

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2013
Messages
826
Likes
1,164
Points
180
mpiga domo

mpiga domo

JF-Expert Member
Joined Apr 30, 2013
826 1,164 180
Hahahaha nchi ya kusadikika hii.

"Fairy Tale country"

Kituko zaidi subiri hao watuhumiwa watakaopelekwa, miniscule charges za kuiba vimilioni lakini watavyokuwa paraded kwenye magazeti na tv for publicity stunt.

Cha kushangaza waliotufikisha hapa kwa kuiba matrillioni hutakaa uwaone zaidi watazidi kuvyikwa vyeo.
 
myoyambendi

myoyambendi

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2013
Messages
65,183
Likes
317,033
Points
280
myoyambendi

myoyambendi

JF-Expert Member
Joined Sep 13, 2013
65,183 317,033 280
wakati wa kampeni za uchaguzi tulisikia habari za wakulima,wafugaji,wavuvi kuboreshewa mazingira yao. baada ya uchaguzi je ni kiasi gani wameboreshewa au angalau wanatajwa?
 
C

chabusalu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Messages
6,592
Likes
3,897
Points
280
C

chabusalu

JF-Expert Member
Joined Apr 29, 2016
6,592 3,897 280
Hicho ni kitengo kama kilivyo mahakama ya ardhi,biashara nk.
Wewe kaa tayari kusikia mafisadi papa wakianza kupelekwa kwenye mahakama ya mafisadi na wahujumu uchumi akiwemo baba wa ufisadi Tanzania mh.mgombea urais wa kudumu wa Chadema.
Hivi hii mahakama itafanya kazi chini ya utawala wa CCM tu? I mean CCM ikitoka mahakamani inaondoka na mahakama hiyo?
 
Utamaduni

Utamaduni

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2007
Messages
1,215
Likes
220
Points
160
Utamaduni

Utamaduni

JF-Expert Member
Joined Oct 23, 2007
1,215 220 160
Mamvi naomba awe mshitakiwa wa kwanza kwenye hiyo mahakama, maana yeye ndiyo chanzo cha ufisadi wote.
 
Usher-smith

Usher-smith

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2015
Messages
6,742
Likes
5,733
Points
280
Usher-smith

Usher-smith

JF-Expert Member
Joined Jul 7, 2015
6,742 5,733 280
Bila shaka dhana ya "kujenga" inafahamika kwa kila mtu. Kipindi cha kampeni tuliaminishwa kuwa tukiwachagua watajenga mahakama ya mafisadi na kwa kila aliyesikia hili alijenga taswira mahususi kabisa kuwa mahakama hiyo itajengwa kweli na itakuwa tofauti na hizi mahakama tulizonazo kwa sasa.

Leo tunaambiwa mahakama hii itaanza kufanya kazi. Mimi kwa upande wangu sijui mahakama hii imeanza kujengwa na kumalizika lini, na ni wapi mahakama hii imejengwa?

Isijekuwa kesi za mafisadi tunaenda kuzisikilizia palepale kisutu kwenye mahakama tulizozoea kuona wanapelekwa akina Lissu
Mahakama sio lazima jengo lijengwe
Wanaweza hata kupanga
 
M

magafumukama

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2016
Messages
742
Likes
196
Points
60
Age
68
M

magafumukama

JF-Expert Member
Joined May 31, 2016
742 196 60
Mimi jesho siyo issue. My main concern ni kwa watendaji; watakuwa imported K utoka nchi gani? Au ni walewale waliofaidika na escrow ?
 
K

kalulukalunde

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2016
Messages
1,056
Likes
1,064
Points
280
K

kalulukalunde

JF-Expert Member
Joined May 27, 2016
1,056 1,064 280
MAHAKAMA Maalumu ya kushughulikia Makosa ya Rushwa na Ufisadi, inaanza rasmi leo Julai mosi.

Pamoja na kuanza kwa mahakama hiyo, serikali imeanza mchakato kuifanyia marekebisho Sheria Namba 11 ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini ya Mwaka 2007 ili kuongeza ukubwa wa adhabu zinazotolewa sasa.

Mahakama hiyo iliyoahidiwa na Rais John Magufuli wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 na imo katika Ilani ya Uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi, itaimarisha zaidi taasisi za uwajibikaji zinazohusika na mapambano dhidi ya rushwa.

Ahadi hiyo ambayo inatimizwa ndani ya kipindi cha miezi isiyozidi saba tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani ni sehemu ya mapambano ya kujenga misingi ya uchumi kwa kudhibiti rushwa na mianya yake na kuleta uwajibikaji.

Akiahirisha Bunge jana mjini hapa, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alisema utekelezaji wa ahadi hiyo unakwenda sambamba na kuonesha dhamira ya serikali ya kushughulikia makosa ya rushwa na kuweka misingi imara ya uwajibikaji katika sekta zote.

“Mahakama itawafanya watu waliozoea rushwa na ufisadi kujiuliza mara mbili kabla ya kufanya uhalifu huo yaani kuwa deterrent,” alisema Waziri Mkuu na kuongeza kuwa kuwapo kwake kutahamasisha wafanyabiashara kufanya shughuli zao bila shaka huku umuhimu kwao, ikiwa ni kulipa kodi.

Akielezea umuhimu wa mahakama hiyo, alisema kwamba itasaidia kuendeleza nia ya serikali ya watu kulipa kodi kwa maendeleo ya taifa.

Akielezea umuhimu wa kodi, alisema kuna mahitaji makubwa ya fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo na uendeshaji wa shughuli za serikali na hivyo serikali itaendelea ukusanyaji wa mapato ya ndani na kudhibiti mianya ya ukwepaji kodi.

Aidha, alisema serikali itaanzisha Kikosi Maalumu cha kufuatilia kwa karibu matumizi ya mashine za kielektroniki (EFDs) za kutoa risiti kila mfanyabiashara anapouza bidhaa au huduma na kuhakikisha kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) wanashirikiana na Wakala wa Serikali wa Serikali Mtandao kutekeleza mfumo wa kuwa na dirisha moja na pia kudhibiti kikamilifu mizigo inayoingia na kutoka bandari kavu.

Udhibiti wa matumizi

Akizungumzia matumizi, Waziri Mkuu alisema serikali itaendelea na kudhibiti matumizi yasiyokuwa ya lazima na kufuatilia bajeti na matumizi ya fedha za umma.

Na ili kufanikisha hilo, itafanya mapitio ya majukumu ya wizara na taasisi za umma ili kuwianisha majukumu ya vyombo vya serikali na hivyo kupunguza gharama za uendeshaji.

Aidha, uhakiki wa wafanyakazi utaendelea na watendaji wakitakiwa wanadhibiti matumizi ya fedha za umma kwa kuzingatia ukomo wa bajeti ya fungu husika lililoidhinishwa na Bunge.

Aidha, Waziri Mkuu aliagiza halmashauri zote nchini kuanzia leo kuhakikisha kwamba zinatumia mifumo ya kielektroniki katika kukusanya mapato, kulipa, kuweka na kutekeleza kikamilifu mikakati madhubuti ya kuboresha makusanyo iwe yanafanywa na halmashauri au kupitia wakala wake.

Waziri Mkuu alisema wabunge wamepitisha Bajeti ya Serikali inayotegemea sana ukusanyaji wa mapato ya ndani ili kupunguza utegemezi kutoka nje na kuhimiza uwajibikaji katika kuongeza juhudi za kukusanya na kupanua wigo wa kutoza kodi ili mapato yaongezeke.

Aidha, alisema ipo haja ya wananchi kudai risiti kwa huduma mbalimbali wanazonunua na kushirikiana na serikali kubaini wakwepa kodi na kuziba mianya ya upotevu wa mapato ya serikali.

Aliwataka watumishi wa umma kuendelea kufanya kazi kwa maadili katika maeneo yao wakijenga utamaduni wa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu katika utumishi wa umma ili kuongeza ufanisi na tija.

Mpango wa Maendeleo

Akizungumzia maeneo manne ya Mpango wa Maendeleo, Waziri Mkuu alisema kwa sasa Serikali ya Awamu ya Tano imeweka msingi kupitia Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Taifa wa kukuza na kujenga uchumi wa viwanda kwa kuweka mazingira yatakayochochea maendeleo ya viwanda.

Aidha, imejiweka katika hali ya kufungamanisha maendeleo ya uchumi na maendeleo ya watu kwa kuhakikisha kwamba elimu inayotolewa ni bora na inayojenga msingi wa rasilimali watu wanaohitajika kuipeleka nchi katika uchumi wa kati.

Alisema ili kufanikisha hayo serikali itaimarisha mifumo ya kisheria kuwa rafiki na kuvutia wawekezaji wa ndani na nje huku ikiimarisha miundombinu ili iweze kutumika kirahisi na kupunguza gharama zake.

Ili kufanikisha ufanisi na tija, Waziri Mkuu alisema serikali itaimarisha usimamizi, ufuatiliaji na tathmini ya mpango wenyewe wa maendeleo mara kwa mara.

Ili kufanikiwa ametaka tabia ya vijana kushinda katika pombe na kucheza pool table kuachwa na kuwataka viongozi waliochaguliwa sasa wilayani na mikoani kuhakikisha kwamba maeneo ya starehe hayafunguliwi wakati wa muda wa kazi ili vijana washiriki katika uzalishaji mali.

Akizungumzia mkakati wa ujenzi wa uchumi wa viwanda, Waziri Mkuu alisema serikali itategemea zaidi sekta binafsi kama injini ya ukuzaji uchumi na maendeleo na kwamba serikali haitajiingiza moja kwa moja katika kujenga viwanda na kufanya biashara.

Miradi ya umeme

Akizungumzia uimarishaji wa uchumi kwa kuwa na uhakika wa nichati hadi vijijini, alisema serikali imetenga fedha kwa ajili ya kuyapatia maeneo yaliyo nje ya gridi ya taifa nishati bora ikiwa ni pamoja na maeneo ya visiwani.

Alisema Serikali ya Uingereza na Sweden zinachangia katika kuhakikisha kwamba mifumo hiyo ya kupeleka umeme maeneo yaliyo nje ya gridi inafanikiwa. Alisema serikali imetenga zaidi ya Sh trilioni moja kutoka ndani na benki ya dunia kwa ajili ya kuendeleza nishati vijijini.

Habari Leo
 
M

Mtarban

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2015
Messages
3,219
Likes
3,588
Points
280
M

Mtarban

JF-Expert Member
Joined Jan 14, 2015
3,219 3,588 280
Upeo wako sijui unashida gani?Kama umeshindwa at a kunyumbua hili...ulitaka uone wakichukua matofari wanajenga...what's matter was establishment and its division of high court...go beyond your passion na ukeleketwa
"Tutajenga mahakama ya mafisadi" lands haujui maana ya kujenga ndio maana unalopoka tu
 
M

Mtarban

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2015
Messages
3,219
Likes
3,588
Points
280
M

Mtarban

JF-Expert Member
Joined Jan 14, 2015
3,219 3,588 280
Mamvi naomba awe mshitakiwa wa kwanza kwenye hiyo mahakama, maana yeye ndiyo chanzo cha ufisadi wote.
mahakama yenyewe ya kusadikika, au unajua ilipo?
 
M

Mozambiki

Member
Joined
Dec 25, 2015
Messages
16
Likes
4
Points
5
Age
53
M

Mozambiki

Member
Joined Dec 25, 2015
16 4 5
Mahakama si jengo, Mahakama ni "Jurisdiction", hakuna uhusiano wowote kati ya jengo na Mahakama, inawezekana kabisa kesi ikasikilizwa chini ya mti na uamuzi ukafikiwa.
 
Forum statistics

Threads 1,237,525
Members 475,533
Posts 29,291,933