Mahakama ya kodi ilisema ACACIA imesajiliwa BRELA

Mahakama ya kodi ilisema ACACIA imesajiliwa BRELA

Iyo karatasi iliyoandikwa kizungu inasemaje?me sielewi au kunawazungu tupu humu
 
Wadau jadilini kwa hoja kwa hoja bila jazba wala matusi...ukweli utajulikana tu siku moja
 
African Barrick ndio Acacia?
Mkuu kama wana affidavit ya "change of name from barrick to acacia hiyo ni legal". isitoshe waliotoa hiyo hukumu ni wanasheria waliobobea. Let us wait and see. Mfano mzuri ni daudi bashite tunaambiwa ana affidavit ya change of name. Hivyo jina analotumia sasa hivi ni legal kwa ile affidavit labda iwe proven aliidanganya mahakama. Hilo litakuwa jambo lingine.
 
Wewe ni kilaza kweli aliyesajiliwa na brela hapo ni barrick acacia kaibuka kuanzia 2014.....Kwa nini utafute data mahakamani badala ya brela??

Msaliti mkubwa we...
Mbona una paniki jibu hoja matusi ya nini hatuwezi wote kuwa kama kasuku.
 
Mkuu kama wana affidavit ya "change of name from barrick to acacia hiyo ni legal". isitoshe waliotoa hiyo hukumu ni wanasheria waliobobea. Let us wait and see. Mfano mzuri ni daudi bashite tunaambiwa ana affidavit ya change of name. Hivyo jina analotumia sasa hivi ni legal kwa ile affidavit labda iwe proven aliidanganya mahakama. Hilo litakuwa jambo lingine.
Mbona Barrick ipo Na acacia ipo
 
Ivi jina la kampuni linasajiliwa kama? Sasa huo si ndiyo wizi number one kama ule wimbo. Acheni zenu hata huyu aliye draft hii barau uwezo wake ni mdogo na yeye apelekwe mahakamani. Ana siri kubwa..??
 
Na majuzi Acacia alitaka kuiuza hii kampuni kwa wachina na wakimbie na kodi zetu. Rais akashutuka. Zitto alilaumu sana serikali kwa kusema tumepoteza bilioni 800. Sasa tuna mwizi wetu mkononi tutapata matrilioni
 
kumbukumbu za Brela hazionyeshi acacia kusajiliwa.

inaonekana hawa acacia wameichezea nchi yetu kila kona wakisaidiwa na wazawa ambao si wazalendo!!
hili ni 'dude" !!!!

walewote walio shirikiana kufanikisha " dude" hili likaendelea kupora rasilimali zetu wachukuliwe hatua za kisheria kwani hii itakuwa fundisho kwa viongozi wengine.
 
Makampuni ya kigeni mengi yanatumia mwanya huu wa tax holidays kutokulipa kodi sio kwa madini tu hata mahoteli mengi ya kitalii. Unaweza ukapita pale ngorongoro ukakuta hoteli inaitwa kwa jina fulani afu baada miaka chache hiyo jina imebadilishwa ili tax holidays ziendelee. Sera zetu za uwekezaji ni za unyonyaji 100%
 
“Utakuta mtu anajidai anajua, mimi namwangalia tu kwa sababu wakati mwingine hajai kwenye kiganja changu.” — Andrew Chenge, mnyamaa [emoji23][emoji23][emoji23]
[emoji2] [emoji2] [emoji2]
 
Si umesikia pendekezo kuwa Mtendaji wa TRA LTP department chunguzwe na vyombo vya usalama?
 
Hawa inawezekana waliingizwa kwenye 18 na inavyo onekana apo brela ndio mkia ulioshikiliwa na mangu kwingine kupo kwene maji akiachia huo mkia huyu samaki acacia atakimbia speed kama samaki papa!!! Brela ndipo penye mtego tegemewa!!
 
African Barrick ndio Acacia?
Huna uelewa wowote kuhusu sheria inazosimamia makampuni.

Kuna tofauti kati ya kampuni mpya na kampuni kubadili jina. Barrick African Gold ilisajiliwa BRELA, baadaye ilibadilisha jina. Kubadili jina kunahitaji notification tu kwa mamlaka husika na siyo kujisajili upya.

Mimi ninafanya kazi kwenye kampuni iliyobadili jina, baada ya kubadili jina, hatukusajiliwa upya BRELA. Mkanganyiko wa ACACIA huko BREKA huenda unatokana na ugeni wa maafisa wake.

Tusiwe wepesi wa kuamini kuwa maadfisa wote wa BRELA, TRA, DSE, mabenki, Wizara ya Madini, n.k. wote hao wawe wajinga wa kutojua umuhimu wa kampuni kusajiliwa nchini. Hivi kweli wote walikuwa wajinga kiasi hicho ila hawa wajumbe wa kamati walioteuliwa mwezi uliopita ndiyo wawe wajuzi wa kila jambo?

Kwa sasa kila anayehoji anaonekana mjinga, siyo mzalendo, msaliti, na aliyehongwa. Kwa hiyo twende vitani tukiwa vipofu na bubu?

Jambo la muhimu pekee kubwa alilolisema Rais leo ni kutaka kuongea na Acacia ili kuona kama kuna maeneo yanaweza kufanyiwa marekebisho kwa njia ya maelewano.
 
Makampuni ya kigeni mengi yanatumia mwanya huu wa tax holidays kutokulipa kodi sio kwa madini tu hata mahoteli mengi ya kitalii. Unaweza ukapita pale ngorongoro ukakuta hoteli inaitwa kwa jina fulani afu baada miaka chache hiyo jina imebadilishwa ili tax holidays ziendelee. Sera zetu za uwekezaji ni za unyonyaji 100%
Unachoki3leza siyo kweli. Msamaha hutolewa kwa mradi siyo kwa kampuni. Msiwadanganye watu.
 
Back
Top Bottom