mahakama ya kadhi yaiweka Tume ya katiba njia panda, watuhumiana kuchakachua maon ya wananchi?

MORIAH

Senior Member
Aug 13, 2012
103
51
Nimepata habari kwamba Wajumbe wa Tume ya katiba wako ktk mvutano wa chini kwa chini kuhusu hoja ya mahakama ya kadhi. Kuna wajumbe wanataka Mahakama ya kadhi iwepo, wakati wajumbe wengine wanapinga. Nini chanzo cha Manug'uniko? Baadhi ya wajumbe wanadhani kwamba makatibu wa Tume ambao wote ni waislamu wamechakachua ripoti ya maoni kwa kuonesha kwamba maoni ya wengi yalipendekeza uwepo wa kadhi. Tatizo ni nini hapa? Ili Kurekebisha jambo hilo ni lazima wajumbe warudie kusikiliza maoni yote upya ili kujua wangapi waliunga mkono na wangapi walipinga. Kumbuka wajumbe walikuwa ktk makundi tofauti. Kwa kuzingatia idadi ya maoni, That is next to impossible. Hakuna muda.

2 kuna utata wa kwamba si kila ambaye hakupinga uwepo wa mahakama ya kadhi anaunga mkono. Kwa hiyo, kama kila mtu angeulizwa kutoa maoni yake kuhusu jambo hilo idadi ya waliounga au kupinga hoja hiyo ingekuwa na maana.

3, kuna ushahidi wa wazi wa baadhi ya vyama vya siana na dini kuwalisha watu maoni ili wayatoe kwenye tume ya katiba.

4, Sheria yenyewe ya mabadiliko ya katiba inazuia masuala ya dini kuingizwa ktk katiba. Mimi si mjumbe wa Tume ila ni mwanafamilia wa mmoja wa wajumbe wa Tume ya katiba ambaye anadhani kwamba suala la kadhi litaivuruga nchi yetu.

Hata hivyo, jambo jema ni kwamba wako wajumbe wa dini zote mbili kubwa za waislamu na wakristo ktk Tume hiyo wanaotaka suala kadhi lisiwekwe. Tatizo wajumbe wote kutoka z'bar ambao ni 50% wanataka kulazimisha jambo hilo kuwekwa ktk katiba. Kwa upande wa Bara wanaounga mkono hoja hiyo ni wachache sana bila kujali dini zao. Nawasilisha.
 
Hii kitu mbona iko very simple...Kama wanataka mahakama ya kadhi iwekwe kwenye katiba(Maana yake nchi yetu ina dini), basi katiba hiyohiyo iruhusu sheria za madhehebu yote ziwekekwe kwenye katiba na zisimamiwe na serikali na watumishi/wataalamu wao wa sheria walipwe na serikali...! Tupate wote/tukose wote...hakuna dini iliyo juu ya nyingine...!
 
Kuna kitu mimi sielewi hapa, hii tume inasikiliza maoni na kuwasilisha kama yalivyo kwa baraza la katiba au inachagua maoni inayoona yanafaa kupelekwa kwenye baraza??

Isijekuwa wabongo tunapigwa changa la macho. Na vipi kuhusu TUME YA UCHAGUZI, fununu ulizosikia itakuwa huru au we ulitega sikio kwenye Mahakama ya kadhi pekee?
 
Jamani nchi hii haina dini. Mambo hayo yaende zanzibar maana wao ndo wanayajua sisi huku hatuna dini vinginevyo tume mtasababisha vurugu.
 
Nyie mnahangaika na dini.mimi mshahara wangu haukidhi zaidi kunitesa naóekana nafanya kazi hata shati ya shule ya mwangu inanipa wakati mgumu kununu.lipi lianze?
 
Hiki kitu ni SIMPLE lakini waislamu wanataka ku-complicate. Moja ya madai makubwa ya Waislamu ni kwamba hawaitambui BAKWATA kwasababu iliundwa na serikali na SIO Waislamu wenyewe.

Pili katika UISLAMU POMBE na NGURUWE ni HARAMU. Sasa hapa ndiyo inakuja HYPOCRISY ya Waislamu, kama hawaitambui BAKWATA kwasababu iliundwa na serikali kwanini leo basi wanataka MAHAKAMA YA KADHI iundwe na SERIKALI?

Kama pombe na nguruwe ni haramu, kwanini basi WAISLAMU wanataka mahakama ya kadhi pamoja na kodi nyingine iendeshwe na kodi za pombe na nguruwe?!. Kumbuka mlipa kodi mkubwa wa kwanza hapa Tanzania ni Tanzania Breweries Limited.

Suala hili lingekuwa rahisi kama waislamu wangekubali kufuata USHAURI wa Rais, kwamba mahakama ya Kadhi RUKHUSA lakini ianzishwe nje ya mfumo wa serikali. Yaani waislamu waanzishe na kuendesha wenyewe kama ilivyo UK. Kitu kicho wazi ni kwamba inaoneakana waislamu hawana RESOURCES za kuendesha mahakama ya kadhi, hivyo wanataka MBELEKO ya serikali.

Lakini tukiingiza mambo ya dini katika katiba, yatatuvuruga sana, nchi hii ni SECULAR. Pia mnajua mahakama zetu zilivyo hoi bin taabani, majengo ni yale yaliyojengwa na Mjerumani. Serikali miaka 51 ya uhuru imeshindwa kujenga majengo ya mahakama zetu. Wazee wa baraza wanaidai serikali mabilioni ya posho zao. Serikali imeshindwa kuwalipa. Sasa najiuliza serikali ijitwishe tena mzigo wa kugharamikia na kuendesha mahakama ya kadhi kweli itaweza? Make no mistake, yatazuka tena malalamiko mengine, kuwa serikali haijali mahakama ya kadhi ndiyo maana imeshindwa kujenga mahakama hizo na kuboresha posho za makadhi.
 
maneno ya mtu mwenye hekima ni dawa
 
Jamani mwenzenu huu uzi nimeingia kwenye jukwaa la siasa lakini sijui uko jukwaa gani? HUKU UMEFUTWA.
 
Back
Top Bottom