Mahakama ya Kadhi: Wabunge wafanya vurugu wakati wa Semina

Makosa 2 aliyoyafanya baba wa Taifa Mwl Nyerere kwa waislam wakati anashika usukani wa kuiongoza nchi ndio sasa unaleta tabu.1.Kuifuta mahakama ya KADHI.2.Kuwanyima waislam elimu ya juu kwa makusudi!!!
Hebu toa ufafanuzi aliwanyimaje hiyo elimu ya juu? Taasisi nyingi za kikristu ndiyo zilizikuwa zinamiliki mashule na vyuo,yeye kwa msaada akazitaifisha ili ziweze kuwanufaisha hata wa si kuwa waislamu.Hebu nionyeshe shule ngapi za msingi na sekondari zilizokuwa zinamilikiwa na waislamu Kabla ya Uhuru,mapungufu yenu ya kuona elimu ya sioni n muhimu kuliko ya darasani,badilikeni
 
Mimi nimezisoma hoja za wabunge na hakika imenishangaza sana kuona ELIMU yao milivyokuwa finyu katika mambo ya wananchi wanaowawakilisha, elimu ya dunia na hata Kiimani. Na wapo baadhi yao ni Waislaam walokataa kwamba mahakama ya kadhi haipo ktk nguzo wala imani za kiislaam wakasahau kwamba Uislaam haisimamishwi na nguzo na imani pekee bali matendo yaloamrishwa na kuongozwa na Quran. sasa kama Muislaam mwenyewe haijui dini yake ataweza vipi kuwakilisha hoja Bungeni?

Wapo wabunge walosema kwamba Ujio wa mahakama ya kadhi utaleta kadhia, dini nyingine zitataka kuwa na mahakama zao. Sidhani kama inakatazwa ikiwa mahakama ya kadhi ni ibada kwao ktk kutoa suluhu za mirathi, Ndoa na madai mengineyo ya kifamilia na wakataka yatambuliwe kisheria na serikali. Swala hapa ni kutambulika kwa madai, na hukumu za kesi za madai baina ya waumini kulingana na sheria za kiimani ktk ndoa zao, ama sivyo basi serikali isikubali hata vyeti vya ndoa vinavyotokana na imani za dini. Kwa nini serikali inatambua vyeti vya ndoa za dini ikiwa hawataki kuhusika na dini za watu. Ikumbukwe tu kwamba serikali haina dini isipokuwa inatambua kwamba raia wake wana dini zao na muhimu kwa serikali kuheshimu kwa kuwapa fursa wananchi ktk kutimiza ibada zao.

Hakuna mahala waislaam wanapinga kuwepo kwa mahakama za dini nyinginezo kuhusiana na mirathi au ndoa ikiwa sheria zilizopo zinapingana na imani zao. Kikatiba hizi zipo katika sheria ya Common law na zimetambulika toka Uhuru. Hivyo sherria za mahakama ya kadhi zipo na zinatumika katika mahakama zetu isipokuwa hutolewa maamuzi na watu wasiokuwa na elimu ya dini. Hili ndilo tatizo na mwanzo wa kuitaka mahakama ya kadhi. Hoja hii kuwa hapa ni kutokana na hakimu wa kesi za madai ya kiislaam awe Muislaam mwenye elimu ya kesi za madai ya kiislaam.

Na ifahamike tu kwamba kinachozungumziwa hapa ni kesi za madai na sio kesi za Jinai japo wapo waislaam wanaopingana na ujio wa mahakama ya kadhi pia. Sheria hazipo kuridhisha matakwa ya watu isipokuwa kuwaongoza katika imani waloichagua. Hutaki mahakama ya kadhi ondoka ktk Uislaam, ama acha kufunga ndoa katika misingi ya Kiislaam kuna option ya hamashauri ya miji au kimila ukawa na uhuru wa kuoa mke mmoja au wake 10 na ukawafukuza unapotaka.

Mwisho, Kuhusu Bakwata mimi napingana nao lakini sioni tatizo lolote kuhusu Kadhi kuchaguliwa na Mufti mkuu maana sii kosa la Mufti isipokuwa Bakwata kuchukuliwa kama ndio chombo cha waislaam. Kinachotakiwa kufanyika ni serikali kuto itambua Bakwata kama chombo cha Waislaam. Kikaundwa chombo na Waislaam wenyewe na kwa ridhaa yao ambacho kitamchagua Mufti pasipo kuingiliwa na serikali kulingana na sifa zao kisha huyo Mufti ndiye akatambuliwa kama Askofu Pengo wa Wakristu. Na uongozi wake watamchagua kadhi. Swala la kugharamia sii hoja kabisa wala sipendi serikali ihusishwe maana kama waislaam wanaweza kuwalipa Masheikh wake, walimu wake watashindwa vipi kulipia gharama za kesi zao za Madai? hakuna mahala popote ndani ya Quran imesemwa Kadhi ni mwajiliwa wa serikali bali ni mtumishi wa Mungu ktk kutoa haki za waislaam...
 
Ninaposema wote simaanishi asilimia 100 ni wahuni, hapana, ninakuambia tabia za wabunge wetu, na ninadhani unadhani ninapokuambia wahuni namaanisha kama wale wahuni wa kwenye vituo vya mabasi. Inaonekana wewe muhuni kwako ni mtu asiyevaa suti na anaishi kwenye vijiwe tu. Hapana, unaweza kukuta mtu anavaa suti na ni mtanashati lakini ni muhuni kwa vitendo. Kama waziri anakuja anatoa takwimu za uongo huyo kwetu ni muhuni regardless ni msomi na ana handhi. Kama mtu anasimamia wizi wa kura kama alivyo fanya Samuel 6 wakati wa bunge la katiba, huyo ni muhuni tena kuliko muhuni wa kariakoo.

Ni kweli unachosema hata tukibadilisha hizo kasoro bado tutapata viongozi wa aina hii, sina ubishi na hili, je nini kinatufanya tusibadili hizo kasoro ili huo ushuhuda wako wa kupata viongozi wa aina hii hii kimaadili na kiutendaji utimie? Nyinyi ndio wale mnaoishi kwa mazoea kwahiyo mnaridhika na ukiritimba unaofanywa na serekali na hamko tayari ubadilishwe kisa mmezoea mambo madogo. Ila kama ni mtu unayewaza mambo makubwa hakuna sababu ya kubaki na sheria zenye mapungufu ambazo zinaacha mifumo inayopelekea kupata viongozi wabovu. Unakuta mtu anataka uongozi wa eneo fulani ama hata nchi kabisa lakini hayuko tayari kukutana na mijadala huru, bali anakuja kuhutubia na kumwaga porojo kibao bila kutoa ufafanuzi wa utekelezaji wake, dakika ya mwisho anaingia madarakani tena kwa hila na kuishia kufanya apendavyo.
Unaweza kujenga hoja yako bila kumshambulia wala ku-generalize kuhusu mtazamo wa mtu binafsi. Sidhani kama unanifahamu kiasi cha ku-conclude kama hivyo nilivyobold kwenye mada yako. Tukirudi kwenye hoja ninasema kuwa wabunge ni wawakilishi wetu namaanisha kuwa unaweza kupata sample ya tabia za wananchi kwa kuangalia tabia za wabunge. Kama kuna wahuni bungeni hata huku kwa wananchi wapo tena wengine ni watanashati kuliko wabunge. Kuhusu kuwabadili naamini kuwa tunatakiwa kubadilika kama jamii kwanza wa kuchukia uhuni kwa aina zake zote na kuwakataa wahuni wanapokuja kuomba kura kwetu kwa njia za udanganyifu. Lakini kama wananchi wataendelea kutoa kura kwa watoa rushwa mbalimbali hata ungefanyaje wataendelea kuwepo bungeni tena kwa wingi.
 
Hebu tueleze alifanyaje katika kurudisha hiyo elimu?aliwaambia mpeleke watotonwenu should siyo madrasa kwanza?
Daaaah nini wewe? Aliyerudisha hadhi ya elimu kwa waislamu ni Profesa Kighoma ali malima kwa Bara na Seif Sharif Hamad kwa upande wa Zanzibar. Mbona iko simple tu. Mnajifanya mazuzu?
 
Ni akheri ya kasa kuliko kobe. Kumbe hadi wabunge nao wanaudini sijaona dhambi ya kurudishwa mahakama ya kadhi nchi. Sijajua kenya waliwezaje au zanzibar ikoje na hapa tz itakuwaje mpk TEC kufanya waumin wao kuonyesha misimamo yao ktk kujadili maswala ya taifa.
Pole sana Tanzania kwa 2015.
 
Kwani waislamu walipoanzisha shule za seminary, vyuo vikuu, hospital na taasisi zao mbalimbali walileta hoja bungeni? Iweje hili walilete bungeni kama ni kwa ajili yao wenyewe?

Kwanini washinikize kadhi iingizwe kwenye katiba wakati nchi hii haina dini?
 
"Kabla ya kuanza majadiliano, Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia, alitoa hoja kwa Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge, Katiba, Sheria na Utawala, William Ngeleja, kwamba wakati wa majadiliano waandishi wa habari wasiwepo ukumbini kwa kile alichoeleza ni unyeti wa jambo hilo."

Kama kuna kitu kinanishangaza ni hii hali ya wabunge (ambao wanapenda kuitwa waheshimiwa) eti kujiona wao wana haki kuliko watanzania wengine. Hii ilijitokeza wakati wa Bunge la Katiba na sasa naona Mbatia naye anataka kurudia yale yale!

"Eti waandishi wa habari wasiingie kwenye kikao wakati wabunge wanajadili suala la Mahakama ya Kadhi"!!!!

Swali hapa; Ni Kwanini wasiingie lakini kwenye vikao vingine ni rukhusa????

Au ndiyo yale aliyoyasema waziri mmoja katika bunge la Katiba "Eti wahandishi wa habari watawachanganya wananchi"!!! Mawazo haya yanaonyesha wabunge wanatuona wananchi tuna uelewa mdogo wa kung'amua mambo na wao ndiyo think tanks za taifa ambavyo si kweli hata kidogo. Wabunge nyie ni wawakilishi wetu na mnapolisahau hilo jua hamtedi haki.
 
Ni akheri ya kasa kuliko kobe. Kumbe hadi wabunge nao wanaudini sijaona dhambi ya kurudishwa mahakama ya kadhi nchi. Sijajua kenya waliwezaje au zanzibar ikoje na hapa tz itakuwaje mpk TEC kufanya waumin wao kuonyesha misimamo yao ktk kujadili maswala ya taifa.
Pole sana Tanzania kwa 2015.

Sio TEC pekee wanaopinga MAHAKAMA YA KADHI bali ni Wakristo wote chini ya JUKWAA LA WAKRISTO wakiwepo CCT na Wapentekoste.waliobaki ni Wapagani ambao wakiona huduma za Kijamii zinazotolewa na Makanisa wakilinganisha na Hekaheka za MAGAIDI lazima wawaunge Mkono WAKRISTO.
 
Kwani waislamu walipoanzisha shule za seminary, vyuo vikuu, hospital na taasisi zao mbalimbali walileta hoja bungeni? Iweje hili walilete bungeni kama ni kwa ajili yao wenyewe?

Kwanini washinikize kadhi iingizwe kwenye katiba wakati nchi hii haina dini?

Uendeshaji wa Dini yao unategemea Fadhila ya Serikali.
 
Suala si waislam, suala ni watendaji wa serikali na mamlaka zake kutotambua mashauri hayo. mathalani nimekwenda kukata hukumu ya ndoa mahakama ya kadhi Bakwata, na mpaka tunaenda bakwata/kadhi maana yake wote tuna Imani thabiti ya Uislamu na tumeridhia, Bakwata huwa inatoa certificate ya talaka na ndoa unapoipeeka serikalini hawaitambui unaelezwa uende ukasajili mahakama za serikali ukifika huko nao hawatambui wanakuabi ilipaswa iskilizwe kwa mujibu wa taratiu za serikali sasa utaona jinsi tunavyohangaika. nikweli katiba inatambua uhuru wa kuabudu lakini serikali haitambui ni namna gani waislamu wanaabudu ili uhuru huo wajue unaishia wapi. kwa kuzingatia hilo ndio maana tunaomba uhuru huu wa kuabudu ufahamike kuwa hata kukata mashauri mbalimali yanayohusu waislamu ni ibada na hata kama katiba itatamka bayana uhuru wa kuabudu mipaka yake nadhani isingeleta utata huu ambao tunataka kuachana nao baada ya miaka mingi kuwa nao. Hata mkiukataa leo itakuja kuwa wazi tu is just the matter of time

Hii sababu yako mkuu ndiyo inanipa shida huko tuendako manake hata hawa wakristo makanisa yao hayataki kabisa mambo ya talaka. Yanadai eti ndoa ni mpaka kifo tu kitawatenganisha, lakini serikali inavunja ndoa hizo, je wao nao siwatataka kuwa na mahakama zao ili kuaddress hili tatizo la ndoa na talaka? Ukichukulia hizi dini za siku hizi ambazo viongozi wanajipa majina makubwa "Mara nabii, mara Mtume n.k"

Dini ni mambo ya hiari ni vyema ikaachwa hivyo, sheria za nchi hazina hiari. Kuanzisha mahakama alafu ukasema ni hiari kwenda mahakamani nafikiri hapa matokeo yake tunayajua.
 
Nikuulize wewe ndugu yangu juu ya hii Mahakama ya kadhi unaafiki? Je, kiimani unaweza kunambia haswa misingi ya madai ya Mahakama hii imetokana na nini na shauri kubwa ni lipi...

Ni mahakama inayo tatua migogoro/madai/malalamiko ya kijamii ya Waislaam katika sheria na kanuni za misingi ya Kiislaam. Mambo hayo ya kijamiu ni ndoa, mirathi na talaka.
 
Sio TEC pekee wanaopinga MAHAKAMA YA KADHI bali ni Wakristo wote chini ya JUKWAA LA WAKRISTO wakiwepo CCT na Wapentekoste.waliobaki ni Wapagani ambao wakiona huduma za Kijamii zinazotolewa na Makanisa wakilinganisha na Hekaheka za MAGAIDI lazima wawaunge Mkono WAKRISTO.

Sasa unapingaje jambo lisilo kuhusu! ? Kwani Mahakama ya Kadhi itahukumu Wagalatia na Wapagani.
Nyie hamkuwahi kuwa na akili ndio maana mkamuwamba.msalabani mungu wenu!
 
Back
Top Bottom