Mahakama ya Kadhi ni nini?

Mahakama ya Kadhi ni nini?

TAMKO

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2011
Posts
1,090
Reaction score
763
Ndugu watanzania, Tanzania sio nchi wa wanyama wa mikumi au wa ngorongoro, si nchi ya samaki wa nyanza wala mwanza, si nchi ya ndege wala mijusi ya selui. Hii ni nchi yetu sote. Sio uungwana wala ubinaadamu kwa mtanzania yeyote kuonyesha dhamira ya makusudi kutaka kulipasua katikati taifa letu hili kwa mlengo wa kikundi au kitaasisi ama kisiasa au kidini. Kuikataa mahakama ya kadhi kwa nguvu na povu kubwa ukiwa hujui maana yake ni kulipasua taifa.

Kushinikiza mahakama ya kadhi kuingizwa kwenye katiba ya nchi mchanganyiko wa dini wakati wananchi hatujui maana yake nako tena ni kukipasua taifa. Naamini tukielimishana kwa lugha tutayoielewa sote tutapinga au kukubali tunachokielewa barabara.

Hii kitu mahakama ya kadhi sijaanza kuisikia jana, muda sasa, waislam wanasema chao wakristu wanasema chao tusio na upande wowote tunasema chetu na serikali inatengeneza kwa taabu piko la pande zote. Hatari kubwa serikali yenyewe inatokana na watu wa dini hizi hizi, hilo piko lazima liwe na kila dalili za hatari, sana!

Nimepitia michango mingi sana na post humu jf , vitabu na magazeti kutafuta hasa mahakama ya kadhi ni kitu gani lakini sijapata, zaidi sana ni malumbano ya watu kushinikiza ianzishwe na itambuliwe kisheria na kufadhiliwa na nchi na upande mwingine wanapinga. Watu wote makini huwa hatupingi wala kukataa tusicho na ufahamu nacho.

Niseme wazi mahakama ya kadhi sijui ni nini na inahusika na nini na umuhimu wake kwenye jamii mchanganyiko hii, napoona watu wa dini flani wanalazimisha mambo ya dini yao yaingizwe kwenye katiba ya watu wote kwa upande wangu naona kama watu wabaya wenye agenda mbaya ya udini na hatari. Naona kama ni uchochezi wa hatari sana. Kwa kizazi hiki na kijacho. Lakini maskini naweza kuwa kumbe sijui maana ya kitu hii.

Niombe akiwepo mtu au kikundi wanielimishe waziwazi juu ya mahakama ya kadhi, yakiwepo maswali niulize au niulizwe kwa lengo la kuelimishana sio ubishi au kusutana wala dhamira ya udini kutuongoza. Na nikijua mahakama ya kadhi ni nini na nikaelewa umuhimu wake kuhudumiwa na jamhuri niunge mkono harakati kwa nguvu zote. Lakini nikishindwa kuielewa basi nitawapinga wanaovuruga taifa langu kwa nguvu zangu zote.

Tuelewe hapana aliyekuja na ukristu wake hapa wala uislam wake hapa. Dini hizi zilikuja tu kutokea mbali wala sio asili zetu hivyo mtu asivimbe shavu sana kupambana kwa ajili ya dini yoyote. Taifa kwanza.

Tafadhali wenye matusi na kebehi za udini mkitupisha tutafurahi sio lazima uchangie au utukane. Hatuongelei udini, tunaelimishana hapa. Nina imani watu wengi wakielewa watakuwa na uamuzi unaotokana na uelewa wa kitu.

Jibu
Kubwa linalo kera ni Talaka kutolewa hovyo hovyo Mke na mtoto wanapata shida.
Kadhi hawezi kuruhusu unyanyapaa ndani ya ndoa kati yao wote WAWILI hishima na uvumilivu lazima uwepo.
Leo watu tunataka kubadilisha wake waume kama cm!!!""
Maudhi makubwa ni kesi za Miradhi. Wengi wamedhulumia Mahakamani. Nina hakika kuna miradhi leo zaidi ya miaka 17 mridhi hajapewa. Khaki yake eti kuna chombo nacho kinaitwa RITA kina kalia miradhi ya watu bila huruma.

Tazama Tanesco inavyo angaliwa ktk Utendaji na RITA wala uafikiri haipo wakati INA kazi kubwa kweli kweli ikianza na kusajili Vizazi Ndoa na Vifoo.
Huko ni sehemu nyingine inayo dhdlilisha Umma
Kadhi anao utaratibu kamili wa kugawa miradhi bila ya kuwepo malalamiko wala dhuluma.

Asante Kwa mchango wako..

1.0 NDOA:- tujuaVYO ndoa hufungwa Na kamishna wa ndoa aliye sahiriwa Na Serikali. Awe sheick, padili, au ofisi ya mkuu wa Wilaya. Na kamishna huyu ana mamlaka ya kutoa idhinisho la kutengua ndoa. Sheria Za Nchi zinafafanua Kwa Kina andiko la Talaka Na dhamana ya wanandoa Na watoto kutokana Na Mali iliyopatikana wakati wa uhai wa ndoa husika. Na Sheria ya ndoa ya mwaka 1971 Na emendment ya 2002 zinafafanua Kwa Kina Haki Na stahiki Za wanandoa Kama kipeperushi http://www.kwieco.org/Pdf/SHERIA YA NDOA.pdf
kinavyoonyesha. Embu tuzichambue Sheria hizi tuangalie mapungufu yake Na kisha tuje Na Hoja mbili mosi Kwamba Je Inawezekana mapungufu haya yakaingizwa Kwenye Sheria Hii au pili kutafuta Njia mbadala ya kusolve matatizo hayo Kwa Kufanya mahakama Za kidini zenye mamlaka kamili Kama mahakama ya kadhi, Ardinin, Na nyinginezo.

2.0:- Mirathi. Sheria ya mirathi ya TOKA 1985 ambayo imetokana Na maboresho ya Sheria ya Urithi ya India inafafanua mambo ya mirathi. Kunaweza Kuwa Na kasoro embu tuzichambue kwanza Na kuziweka wazi ndipo tujenge Hoja mpya.

Embu Jenga Hoja, eleza usilalamike, eleza ubaya wa A Na unadhani B watafanya hivi au vile kuboresha. Sio tu kusema Sheria Za Rita Za uthibitisho wa Kifo au kuzaliwa Kwa Mtu zinatubana, no Mtu ukitaka kurithi Mali ya Mtu lazima utambulike Kwamba Kweli ni Mtoto au ndugu wa marehem Na Serikali inaangalia document.

Watanzania hatuna utamaduni wa Kuwa Na vitambulisho. Cheti Cha Kuzaliwa ni moja ya kitambulisho ambacho Ni Haki yako kumpatia mwanao anapozaliwa. Na Cheti hiki humsaidia Kwenye mambo mengi ya kimaisha. Badala ya Mtu kulalamika Kwamba Mahakama wanataka kunitambua Kwamba Mimi Ni Mtoto wa flan kupitia Cheti Ni Vema kujenga utamaduni wa Kuwa na document hizi muhimu.

Lakini pia utaratibu wa kupata document Za Rita si mrefu kiviile, Ni utaratibu wa Uwazi wa kisheria
 
Yaani bora umesema ukweli. Maana watu tumeshajengewa kama kauadui kwa jambo ambalo hatuuelewi kiufasaa. Naungana nawe WALE WENYE UJUZI TU NDO WACHANGIE kuhusu hili.

Naomba tuilinde TANZANIA yenye watz wenye dini. Tusirumbane!
 
Tafsiri nzuri ya KADHI itafute vizuri ktk bibilia ipo .
Kadhi ni Mwamuzi au Mshauri ktk MASHAURI yenu iwe kufungisha Ndoa ama Talaka kwa kosa linalopasa na sio kuonja Bint wa mtu kisha utowe Talaka utakavyo.
Miradhi kwa waridhi bila kudhulumiana.
Kutoa Haki kwa anayedhulumia nk.
 
Huyu anahitaji kuelimishwa tu, baada ya kupewa Elimu akataye.
Tatizo ni kubebe Bibilia pasipo kuisoma, Mchungaji asome wewe uridhiye tu basi.
Atenge muda wa kusoma aya kwa aya na ukurasa kwa ukurasa utajua ila iatabakia shida moja tu kuelewa yakini.
 
Tafsiri nzuri ya KADHI itafute vizuri ktk bibilia ipo .
Kadhi ni Mwamuzi au Mshauri ktk MASHAURI yenu iwe kufungisha Ndoa ama Talaka kwa kosa linalopasa na sio kuonja Bint wa mtu kisha utowe Talaka utakavyo.
Miradhi kwa waridhi bila kudhulumiana.
Kutoa Haki kwa anayedhulumia nk.

Je unadhani Hii Ndiyo Sababu inayojaza kiu ya takwa hili? Na labda ungefafanua kinachomiss Kwenye Sheria Za Nchi Kwa sasa. Labda kuna Mtu hapewi Haki Yake?
 
Tafsiri nzuri ya KADHI itafute vizuri ktk bibilia ipo .
Kadhi ni Mwamuzi au Mshauri ktk MASHAURI yenu iwe kufungisha Ndoa ama Talaka kwa kosa linalopasa na sio kuonja Bint wa mtu kisha utowe Talaka utakavyo.
Miradhi kwa waridhi bila kudhulumiana.
Kutoa Haki kwa anayedhulumia nk.

Je wanawake wanaitaka?
 
Kwani kuna ulazima gani wanawake waitake, uislam hauendeshwi kwa matakwa ya wanawake kama ilivyo dini yako.
 
Kubwa linalo kera ni Talaka kutolewa hovyo hovyo Mke na mtoto wanapata shida.
Kadhi hawezi kuruhusu unyanyapaa ndani ya ndoa kati yao wote WAWILI hishima na uvumilivu lazima uwepo.
Leo watu tunataka kubadilisha wake waume kama cm!!!""
Maudhi makubwa ni kesi za Miradhi. Wengi wamedhulumia Mahakamani. Nina hakika kuna miradhi leo zaidi ya miaka 17 mridhi hajapewa. Khaki yake eti kuna chombo nacho kinaitwa RITA kina kalia miradhi ya watu bila huruma.

Tazama Tanesco inavyo angaliwa ktk Utendaji na RITA wala uafikiri haipo wakati INA kazi kubwa kweli kweli ikianza na kusajili Vizazi Ndoa na Vifoo.
Huko ni sehemu nyingine inayo dhdlilisha Umma
Kadhi anao utaratibu kamili wa kugawa miradhi bila ya kuwepo malalamiko wala dhuluma.
 
Waislamu wanadai Kadhi ni sehemu yao ya Ibada. Ila Jk ashawajibu ndugu zake wa kiislamu pale Dodoma kwenye msikiti wa Gadafi. Alisema hivi,'sio kazi ya serikali kuendesha ibada za dini'. Wakaanzishe wao na kuhukumiana hukohuko na serikali haitowaingilia.
 
TAMKO

Aisee wewe jamaa ni noma sana..!!! Kitu hukijui na hujui kinahusika na nini halafu unaeleza namna hii...!!!?? Kama huijui mahakama ya kadhi na hujui inahusika na nini sasa wewe ya nini kujua..!!!?? Unatugilibu hujui kumbe unajua. Unapima akili zetu eenhee...!!! Mkuu usilete mada usiyoijua bana...!!! Lete unayoijua tukusaidie uijue zaidi...!!!!
 
Last edited by a moderator:
Kinacho takiwa ni kutambuliwa kisharia.
Kadhi akiwa maamuzi Serikali iyatambue
Usilolijua Usiku wa Kiza
 
Mtu ukiulizwa Swali elezea ujuavyo mambo ya Nani anajua au hajui sio Hoja hapa. Mambo ya kuulizwa maswali kisha majibu hayapatikani Ndiyo yazuayo kizungumkuti Na kuonyesha jamii Kwamba something fishy-is on process. Please tuwe open. Ongea Hii kitu na nini Na Ina manufaa gani Na kwanini unadhani ni lazima iwepo Kwenye KATIBA ya Jamhuri.
 
Last edited by a moderator:
Kinacho takiwa ni kutambuliwa kisharia.
Kadhi akiwa maamuzi Serikali iyatambue
Usilolijua Usiku wa Kiza

Kama nisilolijua Ni Usiku wa kiza sasa kwanini uwepo ulazima wa nisilolijua liingizwe Kwenye KATIBA nayoijua!?!??.. Natafuta kulijua Kwa Sababu linawindwa kuingizwa Kwenye KATIBA nayoijua. Ni Haki ya kila Mtanzania kuijua Na kuielewa KATIBA ya Nchi Yake. Si busara kusema baadhi ya Vifungu VYA KATIBA uvielewe vingine hupaswi kuvielewa ..!!
 
Jambo zuri soma kwa main I Torati Zaburi Injli na Furqan.
Utaona hii katiba inatakiwa iweje! Naamini utashangaa sana sana na hizi tafauti zetu za kijinga tanazo taka kuzijenga sasa
 
Mahakama ya kadhi ni mahakama inayoshughulikia masuala ya wale wenye imani ya Kiislamu. Tanzania haijawanyima Waislamu kuwa na hiyo mahakama ila waiendeshe wenyewe.pasipo kuishusisha serikali. Waisalmu wanataka kadhi atambuliwe na kulipwa Serikali huku wakijua dini ni hiari ya mtu. Itakuwaje na imani nyingine zikadai nazo viongozi wa sheria kwenye imani zao nao watambiliwe na Serikali? Hili ni jambo lisolowezekana ingawa Mrema ndo mchochezi wa jambo hili akitafuta kura za Waslamu. Kwa kuwa Mungu hadhihakiwi angalia Mrema alikofikia kisiasa. Yote haya ni kutokana na ulaghai wake. Shame on him.
 
Kubwa linalo kera ni Talaka kutolewa hovyo hovyo Mke na mtoto wanapata shida.
Kadhi hawezi kuruhusu unyanyapaa ndani ya ndoa kati yao wote WAWILI hishima na uvumilivu lazima uwepo.
Leo watu tunataka kubadilisha wake waume kama cm!!!""
Maudhi makubwa ni kesi za Miradhi. Wengi wamedhulumia Mahakamani. Nina hakika kuna miradhi leo zaidi ya miaka 17 mridhi hajapewa. Khaki yake eti kuna chombo nacho kinaitwa RITA kina kalia miradhi ya watu bila huruma.

Tazama Tanesco inavyo angaliwa ktk Utendaji na RITA wala uafikiri haipo wakati INA kazi kubwa kweli kweli ikianza na kusajili Vizazi Ndoa na Vifoo.
Huko ni sehemu nyingine inayo dhdlilisha Umma
Kadhi anao utaratibu kamili wa kugawa miradhi bila ya kuwepo malalamiko wala dhuluma.

Asante Kwa mchango wako..

1.0 NDOA:- tujuaVYO ndoa hufungwa Na kamishna wa ndoa aliye sahiriwa Na Serikali. Awe sheick, padili, au ofisi ya mkuu wa Wilaya. Na kamishna huyu ana mamlaka ya kutoa idhinisho la kutengua ndoa. Sheria Za Nchi zinafafanua Kwa Kina andiko la Talaka Na dhamana ya wanandoa Na watoto kutokana Na Mali iliyopatikana wakati wa uhai wa ndoa husika. Na Sheria ya ndoa ya mwaka 1971 Na emendment ya 2002 zinafafanua Kwa Kina Haki Na stahiki Za wanandoa Kama kipeperushi http://www.kwieco.org/Pdf/SHERIA%20YA%20NDOA.pdf
kinavyoonyesha. Embu tuzichambue Sheria hizi tuangalie mapungufu yake Na kisha tuje Na Hoja mbili mosi Kwamba Je Inawezekana mapungufu haya yakaingizwa Kwenye Sheria Hii au pili kutafuta Njia mbadala ya kusolve matatizo hayo Kwa Kufanya mahakama Za kidini zenye mamlaka kamili Kama mahakama ya kadhi, Ardinin, Na nyinginezo.

2.0:- Mirathi. Sheria ya mirathi ya TOKA 1985 ambayo imetokana Na maboresho ya Sheria ya Urithi ya India inafafanua mambo ya mirathi. Kunaweza Kuwa Na kasoro embu tuzichambue kwanza Na kuziweka wazi ndipo tujenge Hoja mpya.

Embu Jenga Hoja, eleza usilalamike, eleza ubaya wa A Na unadhani B watafanya hivi au vile kuboresha. Sio tu kusema Sheria Za Rita Za uthibitisho wa Kifo au kuzaliwa Kwa Mtu zinatubana, no Mtu ukitaka kurithi Mali ya Mtu lazima utambulike Kwamba Kweli ni Mtoto au ndugu wa marehem Na Serikali inaangalia document.

Watanzania hatuna utamaduni wa Kuwa Na vitambulisho. Cheti Cha Kuzaliwa ni moja ya kitambulisho ambacho Ni Haki yako kumpatia mwanao anapozaliwa. Na Cheti hiki humsaidia Kwenye mambo mengi ya kimaisha. Badala ya Mtu kulalamika Kwamba Mahakama wanataka kunitambua Kwamba Mimi Ni Mtoto wa flan kupitia Cheti Ni Vema kujenga utamaduni wa Kuwa na document hizi muhimu.

Lakini pia utaratibu wa kupata document Za Rita si mrefu kiviile, Ni utaratibu wa Uwazi wa kisheria
 
Jambo zuri soma kwa main I Torati Zaburi Injli na Furqan.
Utaona hii katiba inatakiwa iweje! Naamini utashangaa sana sana na hizi tafauti zetu za kijinga tanazo taka kuzijenga sasa
Tatizo my friend hujui kujielezea.. Ukiulizwa A ujajibu Q Na G . Tulia jikite Kwenye Hoja, jenga fikra zako kutuelewesha tusiojua, lakini Kama uko kiimani zaidi Basi bakia kiimani usiingie mipaka ya watu wengine wenye Imani nyingine
 
Back
Top Bottom