Nakubaliana nawewe kwa asilimia 100%. Vilevile tusiwasahau ndugu zetu wahindu. maana na wao pia ni raia wa tanzania, wana haki ya kuheshimiwa na kutambuliwa utu, imani na itikadi yao. Na hata waislamu tutenganishe sherehe za shia, sun, ahmadiya, kadiria, kadian, sufian. Wote hawa sherehe zao na siku zao za kupumzika tuzitambue. Na ndugu zetu wasabato wanasherehe zao za makambi ama sikukuu ya vibanda. Ni vyema tuwatambue hawa na kupumzika kwa wiki mbili. Siku hizi wachina wameanza kuomba uraia wa tanzania. Chinese new year ni tofauti ya hii tunayoifuata. Inabidi tuwatambue vilevile. Yangu ni hayo tu.