Mahakama Kuu ya Tanzania kuzuia malipo kwa DOWANS?

Hivi hilo deni liko freezed au Interests ndio zinazidi kuongezeka?, when is the deadline ya kulipa?
 
Pamoja na kwenda ICC, The Arbitration Act inasema kuwa Mahakama ya Tanzania ndiyo yenye uamuzi wa mwisho iwapo maamuzi ya ICC yatekelezwe au la. Hivyo mwenye final say kwenye hili jambo ni the High Court of Tanzania na si ICC kwani ruling ya ICC lazima iwe registered kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania na mahakama iseme kama malipo haya ni halali au siyo halali na kuyakataa. Kama ilivyokuwa quoted kwenye hii habari ya THISDAY, sheria ya Tanzania inasema:

"Where an arbitrator or umpire has misconducted himself or an arbitration or award has been improperly procured, the court may set aside the award."
Kumbe kuna vipengele kibao vya kuwabana ma "Mafia" hawa? Kumbe Werema au ana maslahi na hii Dowans au ni kilaza wa sheria. Mimi si mwanasheria, lakini kwa kusoma maoni ya wana Great Thinkers nimeona kuna jambo nyuma ya pazia katika wateule wa serikali ya Kikwete kushabikia malipo yafanywe "Haraka". Ilishakuwa prooved beyond reasonaable doubt kwamba Richmond ilikuwa genge la ma "Mafia" lililokuwa na malengo ya kuifilisi nchi hii, sasa iliwezaje kuurithisha mkataba wa kitapeli kwa Kampuni nyingine ya kitapeli yaani Dowans? Na Serikali "makini" ya Kikwete ilikubali vipi mkataba wa kampuni iliyothibitishwa tapeli kurithishwa kwa nyingine kama hiyo? CCM itafute namna nyingine ya kuchakachua fedha lakini si kwa hili. Tumewashtukia na wakilipa watauona uchungu wetu kwa kuandamana hadi ikulu hata kama nusu yetu tutauwawa na majeshi yao, tutakuwa tumeasisi vita ya ukombozi dhidiya ugandamizaji wa CCM.
Mwitikio wa kesi hii unadokeza msisitizo wakumnyima Rais madaraka makubwa ya kuteuwa watendaji ambao baada ya uteuzi wanakuwa watiifu kwake (Vibaraka) si nchi. Laiti watendaji wa asasi hizo wangekuwa "independent" kama kwa wenzetu, TISS, TAKUKURU na hata Polisi wangekuwa kazini kuwaandama wahalifu hawa ikiwa pamoja na Rais.
 
Bandugu mimi naomba tu nieleweshwe hili hapa kwenye "ICC Rules"
The arbitration agreement contained in this Section shall be governed by and construed in accordance with the Laws of Tanzania.
Hii maana yake ni nini na je, kama Mahakama yetu itatofautiana na tafsiri kama ilivyotolewa na ICC kuhusu sheria yetu ya manunuzi, then what ? Is somebody suggesting that we should just swallow it and like it !

Tunajua vizuri kabisa kuwa hiyo arbitration ilitakiwa ifanyike nchini (Dar es Salaam, Tanzania), je kikao cha ICC kilifanyika hapa ?"
 
Tanesco has every reasons not to pay,
1. Contract was between Tanesco & Richmond, ( kampuni hewa) wakavunja contract, period, Dowans hawamjui, hawajasign nae biashara,
simple as that.
2. Richmond hawakufuata/ kupewa tender kihalali na Tanesco as PPA 2004 directed
3. kama Katiba inaruhusu High Court to rule out wasilipwe then watabase hapo namba 1 & 2 above, Ila tatizo si sheria Rais ndio tatizo, kila
mmoja anajua, spinning na usanii full time, eg, kaahidi 1130 MW kwa miaka 3 during campaigns OCt 2010. while for 5 yrs kaigiza 145 MW tu.
 
Powered by Google Docs

hii link ina issue ya registration na enforcement ya hukuma za icc england and wales naomba mpitie au kila moja wenu a google kwa kuandika registration of arbitration judgement pinset mason
 
viewer
 
hizo hapo juu za uingereza lakini tukijua sheria nyingi zipo sawa na wakati mwingine zetu ni kali zaidi ukitilia maanani nyingi zilitungwa wakati wa mwalimu, na zili lenga kulinda maslahi ya taifa, labda kama hawa wachakachuaji wetu wame chakaco sheria, na hivi mshauri wa raisi kuhusu sheria ni nani? zaidi ya ag?
 
...................This is the argument -- TANESCO ambayo ni legal entity ndani ya Tanzania iliitumia sheria ya PPA na kuamua kuwa mkataba wa Richmond/Dowans ni illegal na ikauvunja. ICC judges ambao ni foreigners walifanya tafsiri yao ya sheria hiyo ya Tanzania ya PPA na kudai kuwa mkataba ulikuwa legal................

Nakumbuka kwenye zile "dozi" alizotuwekea Mkuu Invisible......................kuna sehemu walielezea kuhusu authority ya Accounting Officer na uhalali wa procurement procedures..........na kwamba hiyo ipo kwenye PPA...............je hapo unasemaje..........yule Mwakapugi na mabosi wake walituingiza Mkenge aisee..............
 
Wana JF wenzangu awali ya yote nawatakieni nyote Heri ya mwaka mupya wa 2011.
Nilikuwa nimepotea kwenye mtandao kwa muda baada ya kuwa banned kwasababu za kuwakashfu CCM kwa kuwaita mashoga kutokana na upuuzi walioufanya kwa Mhe.Godblace Lema(MB)wa jimbo la Arusha mjini wakti wa mchakato wa uchaguzi wa Meya wa Jiji la Arusha.

Ifuatayo ni sehemu ya ripoti ya Tume ya Bunge iliyoongozwa na Dk. Harrison Mwakyembe kuhusu Richmond na baadaye Dowans iliyopelekea hatima ya PM Lowassa kumwaga manyanga. Ukisoma between the lines unaweza kubaini kabisa hii pesa 185 Billion Tshs atalipwa nani na kwasababu gani! Kamati teule ya Bunge iliyoongozwa na Dk. Mwakyembe imeweka bayana kabisa Ricmond au Dowans ni kina nani na wako wapi! Kuna sababu gani ya Serikali ya Tanzania kuwalipa MATAPELI WA KIMATAIFA wakishirikaina na Wabongo wenzetu kina RA,EL na AC????????? Kwa kweli hii haikubaliki kama Malaria.


6.0 RICHMOND DEVELOPMENT COMPANY LLC NI KINA NANI?

6.1 Utambulisho wake Kisheria
Mheshimiwa Spika, Mkataba wa uzalishaji umeme wa dharura unaielezea kwenye utangulizi Richmond Development Company LLC kuwa ni kampuni iliyosajiliwa chini ya sheria za Jimbo la Texas, Marekani na yenye anuani ifuatayo: 5825 Schumacher, Houston Texas 77057, Marekani. Aidha, kifungu cha 5.1 (a) cha Mkataba huo kinatoa maelezo ya ziada kuhusu Richmond Development Company LLC kuwa ni kampuni yenye ukomo wa hisa (limited by shares) ambayo uwepo wake Tanzania haukinzani na sheria za nchi. Kifungu hicho kidogo kinamalizia kwa kutamka bayana kuwa kampuni hiyo ina nguvu na mamlaka yote stahili ya kikampuni (all requisite corporate power and authority) ya kumiliki au kukodisha na kutumia mali zake na kuendesha biashara zake kama ilivyokusudiwa nchini Tanzania.

Mheshimiwa Spika, hiyo ndiyo sura ya Richmond Development Company LLC kama ilivyoainishwa katika Mkataba huo wa kisheria uliotiwa saini kwa upande wa TANESCO na aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji wa TANESCO, Johannes G. Lottering na kushuhudiwa na aliyekuwa Kaimu Katibu (Ag. Company Secretary) wa TANESCO, Godson Makia na kwa upande wa Richmond na Meneja wake, Mohamed Gire na kushuhudiwa na wakili maarufu nchini, Dr. Ringo Tenga ambaye alijitambulisha katika mkataba huo kama Katibu wa Richmond Development Company LLC.

6.2 Hadhi ya Richmond kisheria/kikampuni Marekani
Mheshimiwa Spika, uchunguzi wa kina uliofanywa na Kamati Teule ndani na nje ya nchi na kwa msaada mkubwa wa Ubalozi wa Tanzania Washington D.C na Wizara yetu ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, umetoa picha tofauti kabisa na ile iliyomo kwenye mkataba huo. Kamati Teule imejiridhisha kuwa hakuna kampuni yenye jina la Richmond Development Company LLC iliyokuwa imesajiliwa Jimbo la Texas wakati wa kusaini mkataba huo au iliyosajiliwa baada ya mkataba huo hadi tunapowasilisha ripoti hii kwa Mhe. Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 31 Disemba, 2007.
Hitimisho tulilofikia linashabihiana kwa vigezo vyote na ushauri wa kitaalamu uliotolewa na kampuni mashuhuri ya mawakili ya Virginia, Marekani inayoitwa Hunton & Williams LLP kwa Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO mwezi Oktoba 2006. Katika ripoti yake yenye jumla ya kurasa 19, kampuni hiyo ya mawakili imetamka bayana kuwa hakuna kampuni yenye jina la Richmond Development Company LLC kwenye masijala ya Katibu wa Jimbo la Texas ambaye moja ya majukumu yake ni sawa na ya Msajili wa Makampuni wa Tanzania.
Hunton & Williams LLP wameituhumu Richmond Development Company LLC kwa upotoshaji wa hadhi yake kikampuni (misrepresentation of its corporate status) na kutoa tamko lisilo sahihi (incorrect statement) kuhusu hadhi yake chini ya sheria za Texas. Ukaguzi wa kumbukumbu za Katibu wa Jimbo la Texas uliofanywa na kampuni hiyo ya mawakili Oktoba 2006, ulionesha kuwa hakuna kampuni yenye jina la “Richmond Development Company LLC” iliyokuwa imeanzishwa na kuendesha shughuli zake jimboni Texas wakati huo.
Mheshimiwa Spika, aidha, tarehe 10 Oktoba, 2006 gazeti la kila siku la Kiingereza linalochapishwa hapa nchini, The Citizen, lilimkariri afisa mmoja katika Jimbo la Texas, Bw. William Pate, akisema makampuni yote yanayofanya biashara halali jimboni humo yana kumbukumbu zake katika ofisi ya Katibu wa Jimbo la Texas. Alisema ofisi hiyo haina taarifa au kumbukumbu zozote kuhusu kampuni hiyo inayojiita Richmond Development Company LLC.
Wajumbe wa Kamati Teule waliotembelea Marekani kati ya tarehe 10 na 16 Disemba, 2007 waliambiwa na Bwana Mohamed Gire, kuwa Richmond Development Company LLC ni jina mbadala la biashara la kampuni yake iitwayo RDEVCO LLC. Bwana Gire ambaye aliamua mkutano wake na Wajumbe wa Kamati Teule ufanyike ofisini kwa wanasheria wake, Duane Morris LLP waliopo 3200 Southwest Freeway, suite 3150, jijini Houston, alisisitiza kuwa sheria za Texas zinawaruhusu wafanyabiashara na makampuni kutumia majina mbadala au tofauti na yale yaliyopo kisheria kwa sababu za kibiashara. Kamati Teule iliyazingatia maelezo ya Bwana Gire kwa lengo la kuyafanyia kazi.

Ni kweli kabisa kuwa majimbo mengi Marekani, likiwemo la Texas, yanaruhusu matumizi ya majina mbadala katika biashara au huduma. Kwa Kiingereza majina hayo yanaitwa “assumed names” au “dba”, kwa kirefu: “doing business as”. Katika nchi nyingine nyingi kama vile Tanzania, Uingereza, Ireland, Australia na baadhi ya majimbo ya Marekani na sehemu za Kanada, neno linalotumika zaidi ni “t/a”, yaani “trading as”.

Mheshimiwa Spika, katika nchi zote hizo, sheria zinaweka taratibu za kuzingatia ili kuepusha vitendo vya kitapeli katika matumizi ya majina mbadala ya kibiashara. Nchini Tanzania na nchi zingine za Jumuiya ya Madola, zipo sheria maalum za usajili wa majina ya biashara tu ambapo kampuni au mfanyabiashara au mtu yeyote yule ambaye kwa sababu za kibiashara au vinginevyo, asingependa kutumia jina lake halali katika biashara fulani, anaweza kusajili jina mbadala kwa biashara hiyo bila kulazimika kuunda kampuni tofauti. Majina mbadala ya kibiashara hapa kwetu Tanzania yanasajiliwa chini ya Sheria ya Usajili wa Majina ya Biashara (Business Names (Registration) Ordinance) Sura ya 213.

Nchini Marekani vilevile, huwezi ukakurupuka tu na kuanza kutumia jina mbadala la biashara bila kupitia usajili maalum ambao unawawezesha watu wengine kukagua jalada la majina hayo mbadala kwa lengo la kupata utambulisho kamili wa wanayoyatumia. Vilevile, sheria zinalazimu majina hayo kuchapishwa magazetini kwa lengo la kuutaarifu umma. Lengo, kama tulivyodokeza awali, ni kulinda raia wema dhidi ya vitendo vya udanganyifu.
Katika Jimbo la Texas ambako Bwana Gire anaishi, ni kosa la jinai kutumia jina mbadala bila kulisajili. Usajili wa jina mbadala unadumu kwa miaka mitano ambapo mtumiaji lazima asajili jina hilo upya kati ya tarehe 1 Januari na 31 Disemba ya mwaka wa tano.
Sasa je, ni kweli kwamba jina la Richmond Development Company LLC ni jina mbadala la kampuni ya Bwana Gire iitwayo RDEVCO LLC? Je, jina hilo lilisajiliwa ipasavyo? Katika kujibu maswali hayo mbele ya mawakili wake wawili, Bwana Gire aliwakabidhi Wajumbe wa Kamati Teule hati ya uthibitisho ya Harris County, Texas ambayo kwa maoni yake, ilikuwa inathibitisha kuwa Richmond Development Company LLC ni jina mbadala la biashara!

Kamati Teule imeikagua hati hiyo kwa kina na kuona kuwa badala ya kumsaidia Bwana Gire, inazidi kuthibitisha kuwa si mfanyabiashara mwadilifu ila tapeli kwa sababu kuu mbili:
(a) Mbali na kwamba hati hiyo ya Bwana Gire ni kivuli tu au nakala ya “hati” halisi (kama ipo), nakala ambayo haina uthibitisho wowote wa uhalali na uhalisia wake, ilikuwa ina saini ya afisa mmoja tu badala ya wawili walioainishwa katika hati hiyo;
(b) Badala ya hati hiyo kutamka kuwa RDEVCO LLC imesajili jina la Richmond Development Company LLC kama Bwana Gire alivyotaka Kamati Teule ielewe, hadithi mpya kabisa inaanzishwa kuwa Richmond Development Company ni jina mbadala lililosajiliwa na Richmond Development Company LLC! La kushangaza ni kuwa katika baadhi ya barua zake alizoiandikia TANESCO na Wizara ya Nishati na Madini, Bw. Gire anatamka kuwa Richmond Development Company ni jina mbadala la biashara la RDEVCO LLC,

Mheshimiwa Spika, mtu anaweza akadanganyika akafikiri kuwa kiwango hiki cha ubabaishaji hakithibitishi utapeli pekee, bali vilevile elimu duni ya mmiliki wa kampuni hizo, Bwana Gire, inayomfanya asione hatari kubwa anayojitwalia ya hata kumfikisha jela kwa udanganyifu. Lakini kwa mfanyabiashara mzoefu aliyejizungushia mawakili wa kumtetea mambo yakimwendea mrama, anajua analolifanya. Hivyo basi, Richmond Development Company LLC ni kampuni ya kimakusudi, ya kimkakati ambayo haikamatiki, haishitakiki, haipigiki faini na haiadhibiki kwa lolote lile itakalolifanya kwani haina uhai wa kikampuni (corporate personality).

Mheshimiwa Spika, pamoja na Bwana Gire kuamua kufanyia mkutano wake na Wajumbe wa Kamati Teule ofisini kwa wanasheria wake na si kazini kwake mwenyewe, Wajumbe walihakikisha kuwa wanatembelea mtaa unaotajwa kwenye mkataba kuwa ofisi za Richmond Development Company LLC, yaani 5825 Schumacher, Houston Texas, 77057, USA. Anuani hiyo ikawafikisha kwenye jengo lenye jina la Richmond Printing LLC, jina walilothibitisha kuwa la kampuni iliyosajiliwa chini ya Sheria ya Kampuni yenye Ukomo wa Hisa ya Texas (Texas Limited Liability Company Act) tarehe 1 Agosti, 1994 kwa madhumuni ya kuendesha biashara ya uchapishaji na biashara zingine zinazoruhusiwa na sheria kwa kampuni ya aina hiyo. Kampuni hiyo ilianzishwa ikiwa na mwanahisa na meneja mmoja tu kwa jina Mohamed Gire.

Aidha, Wajumbe wa Kamati Teule wakatambua kuwa jengo hilo la Richmond Printing LLC linatumiwa vilevile kama ofisi za RDEVCO LLC, kampuni ambayo ilisajiliwa chini ya sheria hiyo hiyo ya Texas tarehe 11 Septemba, 2003 ikiwa na madhumuni mapana ya kujishughulisha na “biashara yoyote halali”. Kampuni hiyo vilevile ilianzishwa ikiwa na mwanahisa na meneja mmoja tu kwa jina Mohamed Gire. Tunalazimika kusema kuwa jengo hilo vilevile ni “makao makuu” ya kampuni hewa ya Richmond Development Company LLC.
Licha ya kutumia jengo moja, kampuni zote hizo zinamhusu mtu mmoja, Mohamed Gire, na zinatumia anuani moja. Kutokana na uchambuzi huu, ni wazi kuwa maelezo yaliyomo kwenye utangulizi wa Mkataba kati ya Richmond Development Company LLC na TANESCO kuwa chombo hicho cha biashara cha Bw. Gire ni “kampuni iliyosajiliwa chini ya sheria za Jimbo la Texas”, si sahihi hata kidogo.
6.3 Hadhi ya Richmond kisheria/ kikampuni Tanzania
Mheshimiwa Spika, Richmond Development Company LLC si jina geni Tanzania. Jina hilo lilianza kusikika nchini kwa mara ya kwanza mwaka 2003 na kwa kishindo likihusishwa na mradi mkubwa wa takriban shilingi bilioni 400 wa ujenzi wa bomba la mafuta la urefu wa kilometa 1,150 kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza.
Mheshimiwa Spika, katika barua yake ya kujitambulisha iliyotumwa kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) tarehe 28 Mei, 2003, Richmond Development Company wakati huo ikijiita kwa kifupi RDC, ikajitambulisha kuwa kampuni yenye uzoefu wa zaidi ya miaka 25 katika miradi ya nishati na kwamba imekamilisha miradi mbalimbali ya aina hiyo kwa zaidi ya Dola za Kimarekani milioni 500 katika nchi zinazoendelea. Kutokana na wasifu huo, TPDC ikawapa RDC nakala ya ripoti ya upembuzi yakinifu iliyofanywa na kampuni ya COWIconsult (Tanzania) Consulting Engineers and Planners Ltd mwaka 1997 ili kupata taarifa za awali kuhusu mradi huo. Aidha Wizara ya Nishati na Madini ikairuhusu RDC kuleta mapendekezo ya awali kuhusu mradi huo.
Mapema mwezi Oktoba, 2003 Wizara ikapokea mapendekezo ya awali ya mradi kutoka RDC ambayo yalipitiwa na wataalamu wa Wizara na TPDC na kukutwa na mapungufu mengi yakiwemo: kukosekana kwa tathmini za kifedha na za kiuchumi za mradi, kukosekana kwa tathmini za mazingira, na kukosekana kwa mpango wa kuwapa makazi waathirika katika njia ya bomba. Kutokana na mapungufu hayo, Wizara ikasita kuipa RDC mradi huo muhimu na kuitaka kampuni hiyo kwanza irekebishe mapungufu yote yaliyojitokeza. RDC nayo ikaweka sharti la kupewa upendeleo wa kutoruhusu kampuni nyingine kwenye mradi huo kwa kipindi maalum (exclusivity period) ili kukamilisha kazi hiyo bila wasiwasi wa kunyang’anywa mradi.

Mheshimiwa Spika, tarehe 30 Juni, 2004 Mhe. Daniel Yona, wakati huo Waziri wa Nishati na Madini na Bwana Mohamed Gire, wakati huo akijiita Mwenyekiti wa RDC, wakasaini mkataba wa awali (Memorandum of Understanding) ulioipa RDC exclusivity period ya miezi 18 kufanya upembuzi yakinifu wa kina. Mkataba huo, pamoja na mambo mengine, uliitaka RDC kuipa Wizara ripoti za maendeleo ya utekelezaji wa mradi kila baada ya miezi sita na uliipa Wizara jukumu la kuhakikisha kuwa mradi huo unatekelezwa na RDC mara baada ya zoezi la upembuzi yakinifu wa kina kufanikishwa.
Mheshimiwa Spika, tangu mkataba huo usainiwe, RDC haikuonekana tena ikijishughulisha na utekelezaji wa sehemu yake ya mkataba. Kumbukumbu za mawasiliano kati ya Wizara na kampuni hiyo, zimetawaliwa na malalamiko ya watendaji wa Wizara kuhusu ubabaishaji wa RDC. Hatimaye tarehe 9 Januari, 2006, Ndugu. Bashir J. Mrindoko, kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, akaiandikia barua RDC kuitaarifu kuwa mkataba kati yake na Wizara kuhusu bomba la mafuta ulikoma tarehe 30 Disemba, 2005 na wawekezaji wengine sasa wanapewa fursa kuendelea na mradi huo.
Sehemu ya barua ya Katibu Mkuu inasomeka hivi: “The Ministry of Energy and Minineral (sic) notes with regret that throughout the 18 month exclusivity period, in spite of several reminders, the Richmond Development Company failed to honor its obligations as provided for in Art.2.1 and 2.2 of the Memorandum”. (Wizara inasikitika kuwa kwa kipindi chote cha miezi 18 ya upendeleo, Richmond Development Company, pamoja na kukumbushwa mara kwa mara, ilishindwa kuheshimu wajibu wake kama ulivyoainishwa katika Ibara ya 2.1 na 2.2 ya Mkataba).
Mheshimiwa Spika, naomba turejee kwenye hoja ya awali ya kupima ukweli uliomo kwenye kifungu cha 5.1 (a) cha Mkataba kati ya TANESCO na kampuni hiyo ya Richmond tulichokinukuu awali kinachosema Richmond Development Company LLC ni kampuni yenye ukomo wa hisa ambayo uwepo wake Tanzania haukinzani na sheria za nchi na kwamba kampuni hiyo ina nguvu na mamlaka yote stahili ya kikampuni ya kumiliki au kukodisha na kutumia mali zake na kuendesha biashara zake nchini.
Katika kupima ukweli wa kauli hizo ndani ya mkataba, kikwazo kikubwa cha mwanzo ambacho Kamati Teule ilikipata kilikuwa ni msingi wa kuichunguza Richmond Development Company LLC kama kampuni wakati uhalali wake kama kampuni huko ilikotoka unabishaniwa au kwa lugha iliyonyooka, haupo. Richmond Development Company LLC, kwa maneno mengine, si kampuni ya mchana bali ya usiku, kampuni ya mfukoni au ya sanduku la barua (mail box company)! Hiyo ndiyo kampuni ambayo shirika la umma, TANESCO, iliingia nayo mkataba wa mabilioni ya fedha za walipa kodi wa Tanzania.
Mheshimiwa Spika, kampuni ya wanasheria ya Kimarekani ya Hunton & Wiliams LLP iliyopewa kazi na Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO kuichunguza Richmond Development Company LLC, kama tulivyoeleza hapo awali, inathibitisha kuwa tarehe 23 Juni, 2006 siku ambayo mkataba huo ulisainiwa, Richmond Development Company LLC haikuwa na nguvu za kisheria wala mamlaka yoyote ya kikampuni kuiwezesha kuendesha shughuli zake Tanzania.
Kamati inaamini kuwa wamiliki au waendeshaji wa kampuni hiyo wanaotambulishwa kwenye tovuti ya kampuni hiyo (www.rdevco.com), Bwana Mohamed A. Gire na Dk. Mohammed S. Huque, waliliona tatizo hilo na kuamua siku 19 tu baada ya kusainiwa kwa Mkataba huo kusajili kampuni mpya kwa jina la Richmond Development Company (T) Limited yenye makao yake makuu jijini Dar es Salaam. Kampuni hiyo mpya ilisajiliwa tarehe 12 Julai, 2006 na kupewa Hati ya Usajili nambari 57014 ikiwa na wanahisa wawili, kwa majina:
1. Richmond Development Company LLC yenye anuani ya 5825 Schumecher (tunadhani ni Schumacher), Houston – Texas 778057, USA (hisa 750,000) na
2. Naeem Gire wa S.L.P. 1998, Dar es Salaam (hisa 250,000).
Mheshimiwa Spika, kwa kusajili kampuni hiyo mpya, ni dhahiri kuwa wamiliki wa kampuni hiyo walitaka wasibanwe na Kifungu cha 434 cha Sheria ya Makampuni ya Tanzania (Na. 12 ya 2002) kinachotamka wazi kuwa kampuni zote za nje ambazo zinaanzisha ndani ya nchi mahali pa biashara (a place of business), zinawajibika kuwasilisha kwa Msajili wa Makampuni taarifa mbalimbali za kampuni ndani ya siku 30 toka zianzishe mahali pa biashara, kama vile: sheria au mkataba unaoelezea muundo wa kampuni (charter, statutes or memorandum and articles of association); orodha ya wakurugenzi na katibu wa kampuni; anuani kamili ya ofisi kuu ya kampuni; na nakala ya taarifa ya mahesabu ya kampuni na shughuli za kampuni.
Mheshimiwa Spika, kwa kutekeleza masharti yote chini ya kifungu cha 434 cha Sheria ya Makampuni ya 2002, kampuni ya nje itathibitishwa na Msajili wa Makampuni kuwa imetimiza masharti. Uthibitisho huo utakuwa ushahidi kamili wa usajili wa kampuni hiyo ya kigeni nchini ambao utaipa kampuni hiyo haki sawa na kampuni iliyosajiliwa Tanzania katika kumiliki ardhi. Ni dhahiri kuwa taarifa zinazodaiwa chini ya kifungu hicho cha sheria zisingeweza kutolewa na Richmond Development Company LLC, kwa sababu kampuni hiyo isiyo na usajili stahili Marekani haiwezi kuwa nazo.
Pamoja na juhudi hizo za wamiliki wa kampuni ya Richmond, Kamati Teule ilibaini kutokana na ushauri mbalimbali iliopata wa kisheria, kuwa tatizo la uhalali wa Richmond ya Tanzania lilikuwa palepale kwani kifungu cha 3(1) cha Sheria ya Makampuni kinataka watu wawili au zaidi kuwa na uwezo wa kufungua kampuni. Kwa kuwa mmoja wa wanahisa waliofungua kampuni hiyo ya Richmond ya Tanzania ni Richmond Development Company LLC ya Marekani (yenye asilimia 75 ya hisa zote za kampuni hiyo iliyosajiliwa Tanzania) na kwa kuwa kampuni hiyo ya kimarekani haijasajiliwa Marekani wala hapa Tanzania kwa mujibu wa kifungu cha 434 cha Sheria ya Makampuni na kwa kuwa, kutokana na hiyo sababu, kampuni hiyo ya kimarekani haina nguvu wala mamlaka stahili ya kikampuni, Richmond Development Company (T) Limited ina mwanahisa mmoja tu kwa jina Naeem Gire, hali ambayo haikubaliki kisheria.

Mheshimiwa Spika, ni wazi kuwa picha iliyojengwa kwenye mkataba tunaouongelea hapa kuhusu hadhi na uhalali wa Richmond Development Company LLC nchini Tanzania ilikuwa ya kisanii, ya uongo na isiyo na msingi wowote kisheria. Kinachosikitisha hapa ni kuwa mwezi Februari, 2006, yaani mwezi moja tu baada ya Wizara ya Nishati na Madini kuiandikia barua Richmond Development Company LLC kuwa haina imani nayo, “kampuni” hiyo ya Bwana Gire, ikajitosa kwenye zabuni nyingine ya Wizara hiyohiyo ya Nishati na Madini, zabuni ya kuingiza nchini jenereta za kuzalishia umeme wa dharura wa Megawati 100.
6.4 Uwezo wa Richmond Kifedha, Kitaalamu, Kiutendaji
Mheshimiwa Spika, tumeeleza kuwa Richmond Development Company LLC iliweza kuaminiwa na Serikali kufanya upembuzi yakinifu wa kina wa mradi wa bomba la mafuta la Dar es Salaam hadi Mwanza kwa kujitambulisha kuwa:
(a) Kampuni hiyo ina uzoefu mkubwa wa zaidi ya miaka 25 katika kuendeleza miradi ya nishati;
(b) Kampuni hiyo inaaminiwa na taasisi mbalimbali za biashara na fedha za Marekani na ina mahusiano ya karibu na Serikali ya Marekani;
(c) Kampuni hiyo imekamilisha miradi mikubwa ifuatayo duniani: kituo cha umeme cha MW 130 cha Gaziantep, Uturuki (gharama za mradi $117 milioni) na utafutaji wa mafuta na gesi kusini mashariki mwa Ulaya ($150 million).
Mheshimiwa Spika, Serikali ingejaribu kuzichunguza sifa hizo za rejareja za Richmond Development Company LLC hata kwa kuuandikia Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam au kukagua tovuti yake (www.rdevco.com), ukweli ungelidhihirika kuwa “kampuni” hiyo si chochote wala lolote. Tovuti yake yenyewe imesheheni makosa madogo madogo ya Kiingereza na kupambwa na taarifa za juu juu za miradi ambayo “kampuni” hiyo inadai kuitekeleza, hivyo kuzua maswali mengi na hali inayoashiria upeo mdogo kielimu wa wamiliki wa kampuni hiyo.
Kwa mfano ukurasa wa kwanza wa tovuti hiyo iliyoandaliwa mwaka 2004 unabeba dhamira mbili za “kampuni”, lakini dhamira ya kwanza haieleweki, inahitaji mpangilio mpya wa sentensi kwa Kiingereza sanifu. Mbali na makosa madogo madogo ya kisarufi na mpangilio, ambayo yamepamba kurasa zote 11 za tovuti hiyo, ukurasa wa 7 unaorodhesha miradi mbalimbali ambayo “kampuni” hiyo ilikuwa inatekeleza: ujenzi wa uwanja wa kisasa wa michezo unaoweza kuchukua watazamani 65,000; ujenzi wa bomba la mafuta la kilometa 1,150 na ukarabati wa viwanja mbalimbali vya ndege nchini Tanzania. Miradi yote hiyo ilikuwa porojo tupu ambazo watendaji wetu Serikalini hawakustahili kuzifumbia macho.
Mheshimiwa Spika, kama ilivyotarajiwa, “kampuni” hiyo ikashindwa kutekeleza sehemu yake ya mkataba. Mashahidi kadhaa walioongea na Kamati Teule wakati wa uchunguzi, walisema ingelikuwa maajabu kwa “kampuni” ya aina hiyo iliyokuwa haina uwezo kifedha hata wa kuwasafirisha wawakilishi wao kwenda Afrika ya Kusini kwa mazungumzo ya kutafuta fedha za mradi, kampuni iliyokuwa haina uelewa stahili wa masuala ya nishati na iliyokosa rekodi nzuri ya utendaji, kufanikisha mradi huo.

Kwa hali ya kawaida, kampuni yoyote inayoshindwa kutekeleza masharti ya mkataba na Serikali, inalazimika kukaa pembeni kwa muda kusubiri angalau mapungufu yake yasahaulike kidogo. Aidha muda ambao kampuni hiyo itakuwa imekaa pembeni utachukuliwa na waungwana kuwa wa kujisahihisha, wa kurekebisha mapungufu na kuweza kuaminiwa tena. Lakini si kawaida kwa kampuni iliyoshindwa kutekeleza kazi moja ya mteja kurejea muda mfupi baadaye kutafuta kazi nyingine tena yenye unyeti mkubwa kwa mteja huyohuyo bila kigugumizi wala soni.
Hivyo basi, Mheshimiwa Spika, kwa Richmond Development Company LLC kuingia kwenye mchakato wa zabuni nyingine ya Wizara ya Nishati na Madini hata kabla wino kwenye barua iliyoandikiwa na Wizara ikilalamikia utendaji kazi wake haujakauka sawasawa, na kwa Wizara kufumbia macho ubabaishaji bayana wa “kampuni” hiyo na kuiruhusu kushiriki kwenye zabuni ya umeme wa dharura inayohitaji uzoefu maalum bila wasiwasi wa madhara ambayo yangeweza kutokea kwa Taifa, hisia za maslahi binafsi ya baadhi ya viongozi wa Serikali hazikwepeki
 
Bandugu mimi naomba tu nieleweshwe hili hapa kwenye "ICC Rules"
Hii maana yake ni nini na je, kama Mahakama yetu itatofautiana na tafsiri kama ilivyotolewa na ICC kuhusu sheria yetu ya manunuzi, then what ? Is somebody suggesting that we should just swallow it and like it !

Tunajua vizuri kabisa kuwa hiyo arbitration ilitakiwa ifanyike nchini (Dar es Salaam, Tanzania), je kikao cha ICC kilifanyika hapa ?"

In my understanding, wanaposema: "The arbitration agreement contained in this Section shall be governed by and construed in accordance with the Laws of Tanzania", ina maana kuwa mkataba huo utasimamiwa na kutafsiriwa kwa kutumia sheria za Tanzania, in this case The Arbitration Act.
 
Hili la Serikali yetu kupinga haya malipo ya kitapeli ya 185b/-Tshs kwa Dowans linawezekana kabisa kama Wanasheria wetu wataamua kuweka uzalendo mbele. Lakini kwa vile Tanzania inaoongozwa na mafisadi wa CCM ambao tayari wameaanza kutafuta pesa za Uchaguzi mkuu wa 2015 hii pesa italipwa kwa hali yoyote ile.

Haiingii akilini kuwa Serikali hii hii iliyovunja mkataba kwasababu Richmond/Dowans walishindwa kutimiza masharti ya mkataba leo tena ikubali kulipa mabilioni ati kwamba ilifanya makosa kuvunja mkataba. Hii Watanzania lazima tukomae na tukatae upuuzi huu wa kubebeshwa mizigo na mafisadi. Hakuna anayebisha kuwa gharama za umeme zimepanda kutokana na upuuzi huu wa kina Ricmond/Dowans,IPTL,Songas n.k.

Kama serikali itang'ang'ania kulipa hizi Bilioni 185/= na Wanasheria wetu waendelee kunyamaza tu bila kuchukua hatua za kisheria, basi WATANZANIA WOTE NCHI NZIMA TUFANYE MAANDAMANO YA AMANI KUPINGA MALIPO HAYO BANDIA SAMBAMBA NA ONGEZEKO LA NISHATI YA UMEME! Naamini vyama vya siasa makini kama CHADEMA they can organize peaceful demonstration all over the country to send a shockingwave message to Kikwete and his government!
 
ICC inaangalia mkataba ( Contract ) baina Ya Tanzania & Dowans na inaamua kufuatana na huo mkataba vipi unasema na haingalii kuwa kuna kipengele fulani ndani ya mkataba hakikubaliani na sheria za Tanzania sababu mkataba ume sainiwa na Tanzania au muakilishi was serikali ya Tanzania. Bora kulipa au tuombe mfadhili atulipie la sivyo tuta wakimbiza wawekezaji na labda hatutapata mikopo na misaada. Tunaweza kushi bila wafadhali wetu au wawekezaji ?
 
ukifuatilia hiyo report ya harrison hawa wote gire na haque wanatakiwa wafungwe kwa fraud, na Yona nae anatakiwa ashugulikiwe, na mkataba huu hauwezi kuwa transfered toka kwa taperi moja kwenda kwa mwingine. hiyo hukumu ya icc ni mpango wa serikali ya tanzania kutafuta njia za kulipa mkataba haramu au kujilipa kama mdau moja alivyoweka kwenye thread yake.
 
ICC inaangalia mkataba ( Contract ) baina Ya Tanzania & Dowans na inaamua kufuatana na huo mkataba vipi unasema na haingalii kuwa kuna kipengele fulani ndani ya mkataba hakikubaliani na sheria za Tanzania sababu mkataba ume sainiwa na Tanzania au muakilishi was serikali ya Tanzania. Bora kulipa au tuombe mfadhili atulipie la sivyo tuta wakimbiza wawekezaji na labda hatutapata mikopo na misaada. Tunaweza kushi bila wafadhali wetu au wawekezaji ?

kwenye kesi za mkataba kitu cha kwanza kinacho angaliwa ni legal capacity ya wahusika, then legality of the contract itself the mengineyo.
sasa wewe unazungumzia contract uliofanya na minor/mwizi/kichaa kuna kuwa hakuna contract.
exemption kwa minor ni vitu hivyo vikiwa necessesity yake, kichaa ikiwa wakatati ana funga mkataba akili yake ilikuwa sawa, kwa frauderstar hakuna exemption.
na zaidi ya hapo kukiwepo mis -representation, then mkataba unakuwa batili
 
ICC inaangalia mkataba ( Contract ) baina Ya Tanzania & Dowans na inaamua kufuatana na huo mkataba vipi unasema na haingalii kuwa kuna kipengele fulani ndani ya mkataba hakikubaliani na sheria za Tanzania sababu mkataba ume sainiwa na Tanzania au muakilishi was serikali ya Tanzania. Bora kulipa au tuombe mfadhili atulipie la sivyo tuta wakimbiza wawekezaji na labda hatutapata mikopo na misaada. Tunaweza kushi bila wafadhali wetu au wawekezaji ?

akili zako hazina akili, kwani lazima uchangie kama huna points za kuchangia? seem unauelewa mdogo sana wa sheria, ndo nyie ambao tunawasema kila siku.
 
Bandugu mimi naomba tu nieleweshwe hili hapa kwenye "ICC Rules"
Hii maana yake ni nini na je, kama Mahakama yetu itatofautiana na tafsiri kama ilivyotolewa na ICC kuhusu sheria yetu ya manunuzi, then what ? Is somebody suggesting that we should just swallow it and like it !

Tunajua vizuri kabisa kuwa hiyo arbitration ilitakiwa ifanyike nchini (Dar es Salaam, Tanzania), je kikao cha ICC kilifanyika hapa ?"

Mkuu, kifungu hicho hakiwezi kuwepo kwenye ICC rules maana zenyewe ni general na si particular kwa hiyo haziwezi kuzungumzia sheria za nchi yeyote. Naomba utueleze ni kifungu gani kifungu hicho kinapatikana?

Amandla.....
 
Mkuu, ni sahihi kuwa regulations za ICC zinasema kuwa ruling ya ICC ni final and an aggrieved party cannot appeal to ICC or any other legal body. Lakini si kweli kuwa hukumu za nje hazihusiki na The Arbitration Act. Sheria hii inahusu arbitration za ndani na za nje ya nchi. Ndio maana hukumu ya ICC lazima isajiliwe High Court kupitia sheria hii.

At the same time, ili ruling ya ICC iwe enforceable hapa Tanzania, regulations za ICC yenyewe na sheria ya Arbitration ya Tanzania inatamka kuwa lazima hiyo ruling ya ICC iwe submitted High Court of Tanzania na mahakama hiyo ya Tanzania ndiyo inayotoa maamuzi ya mwisho.

Section 17 (1) of The Arbitration Act states:

"An award on a submission on being filed in the court in accordance with this Act shall, unless the court remits it to the reconsideration of the arbitrators or umpire or sets is aside, be enforceable as if it were a decree of the court."

Kwa maana nyingine, ingawa TANESCO imefungwa kwenye mkataba kuwa it can't appeal, High Court inaweza kuirudisha ruling back to ICC for reconsideration na kuwaambia you erred in law in your ruling, kindly review the proceedings of the case. Au High Court of Tanzania pia inaweza kuamua to set aside (kuutupilia mbali) uamuzi wa ICC.

Lazima tutenganishe vitu viwili, ni kweli kuwa TANESCO haiwezi kukata rufani dhidi ya maamuzi ya ICC, lakini Mahakama Kuu ya Tanzania kwa kutumia busara yake ina uwezo wa kukataa kusajili hukumu ya ICC na badala yake kuirudisha hukumu hii ICC ipitiwe upya au kuitupilia mbali kabisa hukumu hii.

The law is on our side, tusibabaike!

Fareed kama uliiona thread ya Invisible mimi nimekuwa na opinion ya kutolipa Dowans based on moral grounds kwamba pamoja na ruling ya ICC kuwafavor Dowans sote tunajua tunaibiwa.
After reading your comments napata matumaini kidogo tena kwamba we still have some room.
Docet II ya Invisible ina mahala 14.2 Choice of Law:This Agreement and All rights under this Agreement and the Annexes shall be governed by, construed and enforced in accordance with the Laws of Tanzania.

Can this clause support your argument kwamba all is not lost yet??
 
Fareed kama uliiona thread ya Invisible mimi nimekuwa na opinion ya kutolipa Dowans based on moral grounds kwamba pamoja na ruling ya ICC kuwafavor Dowans sote tunajua tunaibiwa.
After reading your comments napata matumaini kidogo tena kwamba we still have some room.
Docet II ya Invisible ina mahala 14.2 Choice of Law:This Agreement and All rights under this Agreement and the Annexes shall be governed by, construed and enforced in accordance with the Laws of Tanzania.

Can this clause support your argument kwamba all is not lost yet??

Ni sahihi kabisa, arbitration contract na ICC ruling vyenyewe vinatambua kuwa ili hukumu ya ICC iweze kuwa enforced, ni lazima isimamiwe na itafsiriwe kwa mujibu wa sheria za Tanzania. Hii ina maana kuwa Mahakama Kuu ya Tanzania kwa kutumia The Arbitration Act inaweza kabisa bila wasiwasi wowote kuitupilia mbali hukumu ya ICC kwa hoja mbalimbali ikiwemo kuwa hukumu ya ICC inapingana moja kwa moja na sheria ya Tanzania ya PPA ya 2004 au hata on moral grounds kama ulivyosema.

Tatizo ni kuwa kuna nguvu kubwa sana za kifisadi ndani ya serikali, miongoni mwa wanasiasa (wakiwemo hata wa upinzani) na humu JF kutaka kulazimisha malipo kwa Dowans kwa hoja potofu kuwa maamuzi ya ICC ni final, mali za Tanzania nje zinaweza kupigwa mnada, we messed up we must pay up, etc.

Ukweli ni kuwa Mahakama Kuu ya Tanzania ina uwezo, mamlaka na kila sababu ya kutupilia mbali hukumu ya ICC kwani ICC judges erred in their interpretation of Tanzania's PPA Act of 2004. No one is better placed to declare the correct interpretation ya sheria hii kuliko Mahakama Kuu ya Tanzania.
 
Back
Top Bottom