Mkatavimeo
JF-Expert Member
- Jan 3, 2011
- 2,150
- 868
Mmeongea mengi sana, tena yenye busara, lakini mwisho wa mchezo ni 90 mins, kipenga cha mwisho. Hapo ndo tutajua kuwa nani kaliwa, wananchi kama kawaida au wenye nchi.
Pamoja na kwenda ICC, The Arbitration Act inasema kuwa Mahakama ya Tanzania ndiyo yenye uamuzi wa mwisho iwapo maamuzi ya ICC yatekelezwe au la. Hivyo mwenye final say kwenye hili jambo ni the High Court of Tanzania na si ICC kwani ruling ya ICC lazima iwe registered kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania na mahakama iseme kama malipo haya ni halali au siyo halali na kuyakataa. Kama ilivyokuwa quoted kwenye hii habari ya THISDAY, sheria ya Tanzania inasema:
"Where an arbitrator or umpire has misconducted himself or an arbitration or award has been improperly procured, the court may set aside the award."
Ni sahihi kabisa, arbitration contract na ICC ruling vyenyewe vinatambua kuwa ili hukumu ya ICC iweze kuwa enforced, ni lazima isimamiwe na itafsiriwe kwa mujibu wa sheria za Tanzania. Hii ina maana kuwa Mahakama Kuu ya Tanzania kwa kutumia The Arbitration Act inaweza kabisa bila wasiwasi wowote kuitupilia mbali hukumu ya ICC kwa hoja mbalimbali ikiwemo kuwa hukumu ya ICC inapingana moja kwa moja na sheria ya Tanzania ya PPA ya 2004 au hata on moral grounds kama ulivyosema.
Tatizo ni kuwa kuna nguvu kubwa sana za kifisadi ndani ya serikali, miongoni mwa wanasiasa (wakiwemo hata wa upinzani) na humu JF kutaka kulazimisha malipo kwa Dowans kwa hoja potofu kuwa maamuzi ya ICC ni final, mali za Tanzania nje zinaweza kupigwa mnada, we messed up we must pay up, etc.
Ukweli ni kuwa Mahakama Kuu ya Tanzania ina uwezo, mamlaka na kila sababu ya kutupilia mbali hukumu ya ICC kwani ICC judges erred in their interpretation of Tanzania's PPA Act of 2004. No one is better placed to declare the correct interpretation ya sheria hii kuliko Mahakama Kuu ya Tanzania.
Hapa ndipo unapochanganya vitu tena. Mahakama Kuu ya Tanzania haina mamlaka ya ku-set aside award ya ICC. Unachotaka kushinikiza wafanye ndicho kinachotoa credence kwa mashirika/makampuni ya nje kukataa dispute resolution kuwa governed na sheria za Tanzania. Mahakama Kuu mamlaka yake yanaishia kwenye mipaka ya Tanzania wakati mamlaka ya ICC yameenea kwenye nchi zote ambazo ni signatories wa New York Convention ya 1958. Mahakama yetu ikiingilia uamuzi huo, Dowans watakuwa bado wana uwezo wa kwenda kwenye nchi nyingine ambako Tanzania ina assets na kudai ziwe seized ili kutimiza award. Tusidhanie kuwa the only recourse ya ku-enforce award hii ni judicial system ya Tanzania. Tutakuwa tunajidanganya na mwisho wa siku tutalipa kuliko hiki tunachotaka kukataa.
Amandla.......
You said it ALL!Iyo ela itasaidia CCM kurecover from the billions of money spent kwa election
Ulazima wa kutaka ruling ya ICC ipate blessing ya Mahakama Kuu ya Tanzania maana yake ni kuwa hukumu hii haina meno na haiwezi kuwa enforced mpaka Mahakama Kuu ya Tanzania ikubali. Vinginevyo wangeenda kuikazia hii hukumu Costa Rica, New York, Paris au Iran.
Endeleeni kujaribu kupotosha mambo, lakini ukweli unabaki pale pale. Mwenye final say kuhusu kutekelezwa kwa hukumu ya ICC ni Mahakama Kuu ya Tanzania na ina mamlaka ya kuitupilia mbali hukumu hii.
Ni uzushi na fear mongering kusema mali za Tanzania nje zinaweza kukamatwa. SI KWELI. Tanesco inajitegemea kama shirika linaloweza kushitaki na kushitakiwa, huwezi kukamata mali za serikali.
Kukamata assets za serikali nje itakuwa ni kama wewe Fundi Mchundo uishitaki Tanzania Ports Authority (TPA) kwa kuwa kontena lako limepotea bandarini halafu mahakama itoe hukumu kuwa TPA ikulipe sh milioni 200 kwa mfano. TPA ikikaidi kukulipa au ikasema haina pesa, je unaweza kwenda kuikamata shangingi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar kwa vile ni mali ya serikali na kusema unaipiga mnada ili kufidia deni lako na TPA?
Tusitake kudanganyana bure hapa.
refer to post niliyo weka juu au ukitaka kitu yote fuata hiyo link, uone maelezo umuhimu au ulazima ya hii kitu kuwa registered katika mahakama husika ili iwe enforceable case ya dowans sa costa rica vs tanesco itkuwa maakama ya tanzania au huko costa rica kwa sababu interested parties ndiko makazi yao.Uongo tena. Ingekuwa award haiwi enforced mpaka Mahakama ya nchi husika ikubali basi hakuna ambaye angekubali kupoteza muda kwenda Paris wakati mwisho wa siku maamuzi yote yatafanyika Kivukoni. Hii imeletwa Tanzania kwa registration na primary enforcement kwa sababu ni hapa ndipo mkataba uliingiwa na mdaiwa ana makao makuu yake. Recourse ya kwenda Costa Rica, New York, Paris au Iran ipo kama Mahakama Kuu itaonekana inataka upindisha maamuzi ya ICC. Ni uzushi kudai kuwa Mahakama Kuu ya Tanzania ina uwezo wa ku-set aside award ya ICC. Ni kama vile kusema kuwa Mahakama Kuu yetu inaweza ku-set aside hukumu iliyotelewa na International Criminal Court. Tutaweza kujibalaghua humu mwetu lakini vyombo hivi ni pan-territorial, watatubana kwengine. Dowans ana haki ya ku-submit maombi ya enforcement kokote ambako nchi zake ni signatories wa New York convention.
Unazidi kupotosha. Hapo hatuzungumzii jurisdiction. TPA hawataomba Mahakama i-set aside hukumu kwa vile hawana uwezo wa kunilipa. Pamoja na wao kusema hivyo, nitakuwa na uwezo wa kwenda mahakamani na kuonyesha kuwa TPA wana assets ambazo zinashikika tofauti na wanavyosema. Mahakama itanipa mamlaka ya kuzishika sasa kwa nini nikamtafute Mkuu wa Mkoa?
Ni wewe unayetaka kutudanganya kwa kulazimisha hoja isio na mantik.
Amandla.......
refer to post niliyo weka juu au ukitaka kitu yote fuata hiyo link, uone maelezo umuhimu au ulazima ya hii kitu kuwa registered katika mahakama husika ili iwe enforceable case ya dowans sa costa rica vs tanesco itkuwa maakama ya tanzania au huko costa rica kwa sababu interested parties ndiko makazi yao.
An award is treated as being made at the seat of the arbitration in spite of where it was signed, sent from or delivered to. For example, if an award is made in Paris, the seat of the award is France. France is a party to the New York Convention and the award can therefore be enforced internationally as a New York Convention award.
Ndugu yangu wanasheria waliokuwa na patriotism ni wakina marehemu Ndyanabo na hawapo tena. Leo tumezalisha wanasheria wengi sana lakini?! Mmmhhh ni kama ni mafisadi tu pia. Wanatuingiza mikenge makusudi kwenye mikataba mibovu na wanashindwa kututetea kwenye shida kama hizi.TUMEKWISHA.Hivi hawa wanasheria wa-Tanzania wanafanya nini???, hii sio issue ya mtu mmoja inabidi wote kuumiza vichwa ili tuweze kupata loopholes, am sure there is nothing like open and close case..... if you look hard enough lazima kuna kipengele kitapatikana cha kuweza kujinasua kwenye hii issue, au hawa jamaa hawawezi ku-work for free... mpaka wapelekewe kesi na mshiko??? Jamani hivi hakuna any patriotism??
Kushauri kuwa tuvimbishe misuli ni kuwa myopic.
Amandla.....
kwahiyo in not so many words ni kwamba "we are done for", tumekwisha......, "no way out".....
Mi naona sasa tungeconcentrate kuwatafuta hao wahusika waliotufikisha hapa ili tutaifishe mali zao ziweze kulipia huu uozo. I am sure you cant tell me kwamba hata hao wahusika hatuwezi kuwapata au kuna kipengele kinachowalinda kwa kufanya huu uozo, and I mean kuwafunga jela haitoshi, hata wasipofungwa ila mali zao zipigwe mnada....
pamoja na sarakasi nyingi za kisheria kuonyesha nani yuko right in legal terms...............the reality ni kuwa kama Taifa TUNAIBIWA.............na hiyo ndio recourse yetu
ICC inaangalia mkataba ( Contract ) baina Ya Tanzania & Dowans na inaamua kufuatana na huo mkataba vipi unasema na haingalii kuwa kuna kipengele fulani ndani ya mkataba hakikubaliani na sheria za Tanzania sababu mkataba ume sainiwa na Tanzania au muakilishi was serikali ya Tanzania. Bora kulipa au tuombe mfadhili atulipie la sivyo tuta wakimbiza wawekezaji na labda hatutapata mikopo na misaada. Tunaweza kushi bila wafadhali wetu au wawekezaji ?