Mahakama Kuu: Sheria inayozuia watuhumiwa kupewa dhamana ni kinyume cha Katiba. Serikali yaazimia kukata rufaa

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
8,258
2,000
Hii sheria ya kuwazuia watu kupata dhamana ni ya kijinga, ya kihuni, ya uonevu na ambayo haistahili kuwepo katika jamii yoyote ya watu waliostaarabika. Ubaya wa sheria hii umeonekana zaidi awamu hii ambapo serikali na vyombo vya dola vimeitumia sheria hiyo kuwakomoa na kuwatesa wananchi wasio na makosa.

Na huyo aliyesema atakata rufaa sijui anafanya hivyo kwa faida ya nani. Siamini mtu mwenye hekima, busara na aliye na roho ya Mungu anaweza kuchukua uamuzi huo ili tu serikali na Polisi waendelee kuwatesa watu wasio na hatia kwa kupitia sheria hii, labda kama yeye ni miongoni mwa mawakala wa shetani waishio ndani ya utawala.

Tunamwomba Mungu atembee na wenye haki, na huyo shetani asifanikiwe na badala yake mateso ya wasio na hatia ikawe laana juu yake na kizazi chake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

KOMBESANA

JF-Expert Member
Jun 18, 2009
914
225
LAWS and consequently courts of law are like cobwebs.TOO STRONG if you are WEAK and too WEAK FOR THE STRONG!
 

Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
46,565
2,000
kwenye mahakama ya rufaa watakuja marafiki wa mahakama kina kabudi na kubetua haya mamuzi kama alvyotufanyia kwenye kesi ya mgombea binafsi
 

ostrichegg

JF-Expert Member
Jun 30, 2013
8,186
2,000
Mkuu kwa jinsi kulivyo na ukiukwaji mkubwa wa sheria awamu hii, hata kama kukifanyika mabadiliko ya hiyo sheria, bado wanaotakiwa kukomolewa watakomolewa bila kujali hiyo sheria.
Halafu ndugu zetu waliofilisika kule mtaa wa Lumumba bila chembe ya aibu, wanasifia ETI huo ni uthubutu.
 

Vyamavingi

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
4,976
2,000
Kinachosababisha watu walalamikie sheria ya dhamana ni vyombo vya dola na DPP kuitumia sheria hiyo vibaya. Hii ni pale kosa linalostahili dhamana linabadilishwa kwenda kwenye shitaka lisilo na dhamana.

Vv

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Top Bottom