Mahabusu wagoma kupelekwa mahakamani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mahabusu wagoma kupelekwa mahakamani

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Rutashubanyuma, Jan 7, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,988
  Likes Received: 420,627
  Trophy Points: 280
  Mahabusu wagoma kupelekwa mahakamani


  na Ambrose Wantaigwa, Tarime


  [​IMG] BAADHI ya mahabusu waliokuwa wakitolewa katika gereza kuu wilayani hapa kupelekwa mahakamani jana waligoma na kulala chini nje ya gereza hilo wakipinga kucheleweshwa kusikilizwa kesi zao. Mahabusu hao zaidi ya wanne wanakabiliwa na kesi za mauaji ambapo walikuwa wakipinga muda ambao unachukuliwa na waendesha mashitaka kuwasilisha ushahidi mahakamani, hali inayowanyima haki zao.
  Hata hivyo, mahabusu hao walirejeshwa katika gereza hilo chini ya ulinzi mkali wa polisi huku wenzao wakifikishwa mahakamani.
  Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Tarime/Rorya, Sebastian Zacharia, alisema jana kuwa mahabusu hao walirudishwa na wanatarajia kufunguliwa shitaka la kukaidi amri halali ya serikali.
  Alisema ingawa kila mtuhumiwa katika kesi hana hatia hadi itakavyodhibitiswa na mahakama, sheria haizuii mtuhumiwa kufunguliwa mashitaka iwapo ataonekana kutenda kosa jingine kabla ya kutolewa uamuzi wa shitaka la awali.
  “Wengi wa mahabusu hao waliogoma wanakabiliwa na tuhuma za mauaji ambapo kisheria ni Mahakama Kuu pekee ndiyo yenye uwezo wa kusikiliza kesi kama hizo sasa upande wetu tumeshawakilisha mashitaka na vielelezo vyote muhimu tunasubiri uamuzi wa mwanasheria wa serikali kuamua vinginevyo,” alisema Zacharia.
  Gereza la Tarime linakabiliwa na msongamano wa mahabusu hususan wa kesi za mauaji ambapo katika siku za hivi karibuni mashirika ya kutetea haki za binadamu wilayani hapa yameitaka serikali kupitia Jeshi la Polisi kuharakisha kesi hasa za mauaji, ili kupunguza msongamano huo.  [​IMG]

   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 7, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,988
  Likes Received: 420,627
  Trophy Points: 280
  Ni lini kero za mahubusu zitapatiwa ufumbuzi?
   
Loading...