Mabibi na mabwana ni wazi kuwa awamu ya sita imepokelewa vyema na wapenda haki wote.
Hata hivyo ni wazi kuwa kwa waliokuwa na maslahi yao binafsi katika awamu ya tano, awamu ya sita imekuwa ni mwiba mchungu kweri kweri. Walipo wanatweta hawaamini kuwa hii ni awamu ya sita na bendera ziko milingoti mizima tena.
Miito inapoendelea kusikika kuhamasisha kuungwa mkono kwa awamu ya sita, uwepo kwa watendaji wakereketwa wa awamu ya tano kwenye awamu hii kutaendelea kuwa ni kikwazo kwa mama kwa muda mrefu.
Vipi aliyeshadadia Corona kuwa si ugonjwa bali vita vya kiuchumi tu dhidi ya Tanzania atabadilika ghafla leo na kuiacha busara na sayansi kushika hatamu zake?
Vipi ambaye hakuiona dhuluma ikiwamo ya TRA kwa wananchi atakuwa na msimamo sawa na serikali ya sasa?
Vipi ambaye hakuziona rushwa, urasimu, manyanyaso nk katika awamu ya tano atakuwa na msimamo sawa na serikali ya sasa?
Vipi aliyeshadadia maendeleo fyongo ya kule kwetu atatambua umuhimu wa haki sawa leo?
Vipi walioasisi na kushadadia sheria kandamizi kwenye awamu ile wakawepo kwenye awamu hii?
Vipi hawa akina Kabudi, Majaliwa, Jaffo, Gwajima, Mollel, Mwigulu, Chalamila, nk kwenye waliyokuwa wakiyasimamia yaliyotufikisha huku tunakohitaji kutoka leo?
Vipi watakuwa wa kubatizwa upya? Watakuwa na yapi mapya ya kutwambia leo tofauti na waliyokuwa wanatwambia kule?
Mama safari yake inafanyika kuwa ngumu zaidi kwa kuwapo watendaji wakereketwa 'ma "zealot"' hawa wa awamu ya tano kwenye awamu ya sita.
Tunapolazimika hata kuwataja kwa majina ni katika kuwahimiza kustaarabu tu kuyaweka maslahi ya taifa mbere! Ikiwezekana hata wakapisha kistaarabu tu.
Yaani ni katika kuhimiza kuwepo kwa uzalendo kweri kweri tu.
Au nasema uongo ndugu?
Mungu mbariki mama yetu.
Mungu ibariki Tanzania.