Mwizukulu wa Buganda
JF-Expert Member
- Nov 19, 2024
- 810
- 2,039
Waziri wa fedha, Balozi Khamis Mussa Omar akiwasilisha hotuba ya bajeti kuu ya serikali kwa mwaka wa fedha 2026/2027 amesema .....
"...mkakati wa kuongeza mapato.
Mheshimiwa Spika, takwimu za miaka ya karibuni zinaonesha kuwa misaada kutoka nje imeendelea kupungua mwaka hadi mwaka na hivyo haiwezi kuwa chanzo cha kuaminika cha mapato katika utekelezaji wa bajeti yetu. Aidha, utekelezaji wa miradi kwa fedha za mikopo nao umeendelea kuleta changamoto kwa kuzingatia uhimilivu wa deni, gharama za mikopo, na athari yake kwa uhuru wa taifa letu. Hali hii inasababisha uhitaji wa kuongeza kasi yetu kwenye kujitegemea kiuchumi na mapato. Serikali itachukua hatua zaidi za kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa kuziba mianya ya upotevu na kuimarisha taasisi za ukusanyaji.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2026/2027, serikali kupitia utekelezaji wa Mkakati wa Ukusanyaji wa Mapato wa Muda wa Kati (2025/2026 hadi 2027/2028), itaendelea kuchukua hatua mbalimbali za kuimarisha ukusanyaji wa mapato, na miongoni mwake zikiwemo hizi zifuatazo:
Moja, kuvutia uwekezaji zaidi wa ndani na nje kwa azma ya kutanua wigo wa kodi na kuongeza fursa za ajira.
Pili, kuhamasisha ulipaji kodi kwa hiari kwa kuimarisha mahusiano baina ya sekta ya baina ya serikali na walipakodi kupitia majadiliano kwenye majukwaa mbalimbali ikiwemo Baraza la Taifa la Biashara na CEOs Round Table.
Tatu, kuendelea kusimamia na kuhimiza matumizi ya sifa hii ya mashine za kutolea risiti za kielektroniki kupitia utoaji wa elimu na uendeshaji wa programu mbalimbali za hamasa.
Nne, kuendelea kujenga na kuboresha mifumo ya tehama ya usimamizi na ukusanyaji wa mapato ya ndani kutumia teknolojia ya kisasa ya akili mnemba na matumizi ya taarifa ya big data na kuhakikisha mifumo yote inabadilishana taarifa.
Tano, kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji wa taasisi za umma ili kuhakikisha zinaongeza tija katika ukusanyaji wa mrahaba pamoja na kuhakikisha zinawasilisha gawio na michango stahiki na kwa wakati katika mfuko mkuu wa serikali.
Sita, kuhakikisha bidhaa zote zinazozalishwa nchini, zinazoagizwa na kuuzwa ndani na nje ya nchi zinakuwa na msimbopau, yaani bar code.
Na saba, kuendelea kufanya uchambuzi wa kina na kuanza utekelezaji wa baadhi ya mapendekezo 284 yaliyotolewa na tume ya rais ya maboresho ya mfumo wa kodi.