masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 18,173
- 13,776
Enter Magufuli, na sasa uozo wa mikataba iliyoingiwa na viongozi waliomtangulia inaanza kuonekana wazi jinsi watu walivyoridhia nchi kuibiwa mchana kweupe.
Uzuri wa Magufuli anayafanya yote mchana kweupe, tena mbele ya umma ili kila mmoja ajionee uozo aliourithi.
Mimi siwalaumu moja kwa moja marais waliopita lakini najiuliza swali sipati jibu, Ni kwa nini walibariki usiri wa mikataba kwa nchi kuibiwa kiwazi wazi ?
Wananchi tuliowengi tulikuwa tunajiuliza, wakati mwingine hata kupitia wawakilishi wetu bungeni, usiri huu wa mikataba ni kwa faida ya nchi au watu fulani tu?
Tutashitakiwa kwa kuvunja mikataba hii ya wizi, lakini hata Mwalimu alisema , heri madini yetu yabaki ardhini hadi tutakapojua namna ya kufaidika nayo kama nchi.
Naona Magufuli analitekeleza hilo kwa umakini mkubwa.
Tumeibiwa vya kutosha, sasa tuseme basi.
Wananchi tulio wengi twasema Magufuli asikate tamaa, wizi huu ukomeshwe.