Peter Madukwa
JF-Expert Member
- Sep 20, 2012
- 3,135
- 2,471
Habari zenu wana Jf,
Sote tu mashahidi kuwa miaka ya nyuma kabla ya awamu ya 5 ya Mh. Rais John Pombe Joseph Magufuli kulikuwa na matukio ya kila mara ya ujambazi ikiwemo uporaji ktk mabenki na kuleta hofu na taharuki kwa wananchi.
Benki ilikuwa siyo sehemu salama kwa sababu ya matukio ya ujambazi ya kila mara.
Hujuma za hapa na pale za uporaji wa fedha na mali zilikuwa zinaleta hofu kubwa sana.
Ilikuwa ni kawaida ndani ya mwezi kusikia uvamizi ktk benki tena mchana kweupe na kuleta athari kubwa ya kiuchumi na hofu katika jamii. Lakini tangu aingie Mh Magufuli, amejitahidi kiasi kikubwa kudhibiti matukio ya uhalifu na kuimarisha usalama wa wananchi na mali zao.
Majambazi na vibaka kwa kiasi kikubwa wamedhibitiwa na wengi wao wameacha na kuamua kufanya shughuli zingine halali za kujipatia kipato.
Wale ambao walikuwa wabishi wameishia kukaa kolokoroni na wengine hata kufa katika matukio.
Rejea tukio la majambazi waliojaribu kuvamia benki ya crdb usiku huko Igoma Mwanza, hawakufanikiwa badala yake wameambulia kifo na kuuawa.
Pia kwa kiasi kikubwa Serikali ya awamu ya 5 imefanikiwa kudhibiti uingizaji, uuzaji na utumiaji wa madawa ya kulevya ambayo kwa kiasi kikubwa ilikithiri na kuharibu vijana wetu wengi ambao ni nguvu kazi ya Taifa.
Wengi ambao walikuwa wanajishughulisha na uuzaji wa madawa ya kulevya wameacha biashara hiyo na kuamua kufanya ishu zingine katika hili tunampongeza Mh Rais.
Hii ndiyo Tanzania tunayoitaka. Tanzania yenye uhakika wa usalama wa wananchi na Tanzania watu wanaofanya kazi kwa bidii ktk shughuli halali.
Kama kila mwananchi ataamua kupambana ktk shughuli halali za kiuchumi nchi yetu itapanda kutoka daraja la kati na kuwa ktk daraja la juu zaidi na pia itaendelea kusaidia kupunguza matukio ya uhalifu ambayo hufanywa na watu wenye tamaa ya kupata mafanikio ktk njia rahisi na haramu.
Hongera mh Rais kwa kudhibiti matukio ya Ujambazi na uhalifu.