Magufuli amesema Serikali katika kupambana na foleni Jijini dar es Salaam wameamua Kujenga flyover maeneo ya daraja la salenda. Kasema daraja lililopo halitabomolewa bali daraja jipya litajengwa upande wa baharini.
Kasema mkataba wa awali umeshasainiwa kati ya Serikali ya Tanzania na Korea tayari kwa maandalizi ya Kujenga.
Daraja litakua na urefu wa zaidi ya km7.
Magufuli akiongea na TBC1 alisema;
Mia
HAPA ANAONGEZEA shiidda tu sidhani kama ndio ametatua tatizo. iangalie hiyo picha yake vizuri tu afu piga picha tu hiyo daraja linapoanzia na linapoishia na pia piga picha msururu kutoka ALIHASAN MWINYI RD changanya na msururu unaotokea OCEAN ROAD yote hii ije ikutane ni hilo daraja jipya inamaana ameongezea kipande kingine cha msururu wa foleni ambazo ndio ziatkuja kukutana hapo kwenye makutano na njia ya zamani karibia kwenye mataa ya kuelekea kinondoni. je huoni kuwa hapa kaongeza msongamano mkubwa zaidi??
TUNAPATA HAYA KWA HISANI YA WAHISANI. maumivu yakizidi tutoroke hospitalini
kuna lingine wanataka kujenga dar hadi zenjiyaani tangu ameanza kuzitaja hizo flyover sijaona hata moja ambayo imeshaanza kujengwa walau kuchimba msingi tu. au jamani mtuambie, ile ya ubungo aliyosema je, ile ya TAZARA je, ile ya fire je?, ya magomeni je? sasa anasema ya salanda....wanatudanganya au nini, tell us mr magufuli why should we believe what you are telling us?....
Nimeshangaa sana.Siamini kama Magufuli amefanya tathmini ya kutosha kujua kama hili daraja litakuwa na tija.kutoka Aghakan hadi Cockcock beach maana yake ni kwa wale wanaoelekea Masaki,Osterbay kidogo na Msasani kidogo. Sasa kwa kiasi cha mabilioni zaidi ya 100 sioni tija yake.
Lakini kwa kutengenezeka wakorea hilo daraja la km 7 kwao ni kazi ndogo mno.Korea kuna hadi daraja la km 20 na hili daraja limeshikiliwa na nguzo ndefu za kimo cha mita 70.hayo ya km 7,2,4,6 ni kitu cha kawaida sana kwa kuwa kule ni nchi ya vimilima.
Nasikia utaanza june 2017Mradi umeshaanza?
Una vinasaba vya unabiiHongera rais mtarajiwa!
Barabara ya morocco - mwenge imeshapanuliwa. Ujenzi fly-over ya Tazara umepamba moto, wa-Japan wako kazini pale. Ujenzi fly-over ya ubungo design zimeshakamilika, Mwenge fly over itafuata inshallah..Ni sawa, ila naona hata barabara juanzia moroko waongeze upana hadi hapo salenda, ila la muhimu ni fly over ya tazara na ubungo, wajenge hizo kwanza, sio salenda, mbona tunaishia kuonyeshwa mapicha tu, tuone na kazi.
Tuvute subira mpaka June 2017Hizi ni porojo tu! CCM hawana jipya.
Utafikiri wanakaribia kwenda mwezini. Is that the only problem that cause traffic in this area?