Magufuli: Subirini ushindi wa Tsunami

Magufuli: Subirini ushindi wa Tsunami

haki ya nani vile , nlianza kuheshimu ccm baada ya kutokumpitisha lowassa, alitumia zaidi ya bil 57 kupita kuwa mgombea akiwa ndani ya ccm, do we need such kinda leader?
 
HapakaziTu, wasiofanye kazi na wasile

Bila kufanya kazi nchi haiwez endelea, wanaotaka maendeleo ya nchi kura zoote kwa magufuli
 
CHADEMA hawana jipya, ulishawahi kusikia wakisema watawashughulikia mafisadi mara baada ya kupokea wageni?Jibu ni hapana.Wao wamekalia msemo MABADILIKO, ndicho walichong'ang'ania hawamwagi sera.Swali kwa wabishi wa JF kama lowasa angepitishwa na CCM leo mngemuona Chadema?Kama Sumaye angepitishwa na CCM kuwania Uraisi leo mngemuona Chasdema?Walichokifanya chadema ni sawa na mtu anasafiri kwenda sehemu fulani kwa miguu halafu likatokea gari la taka akaamua kudandia bila kujali atapata madhara gani ili mradi afike, uchu wa madaraka ndio tatizo.Mtu akiwa na njaa basi hutamani chakula cha aina yoyote hata najisi na majuto huja baadae, Watanzania twapaswa kuamka hawa jamaa walituaminisha jamaa ni fisadi leo wanageuka na kusema jamaa ni msafi kisa tuna njaa ya mabadiliko basi na wao wanakuja na gia ya mabadiliko!Ukweli hawatufai.Na ndio maana siku zote nasema mwaka huu ushindani mkubwai ni baina ya Original CCM (CCM A - DR MAGUFULI) na CCM B (CHADEMA- LOWASA).Tuchague kiongozi muadilifu na mchapakazi.
 
Kura Yangu Haiibiki Atakayeiba Afe Atakapotoka Kuhesabu Kura Tu Pia Tsunami Asihesabie Na Kura Yangu Kura Yangu Kwa Lowasa.
 
CHADEMA hawana jipya, ulishawahi kusikia wakisema watawashughulikia mafisadi mara baada ya kupokea wageni?Jibu ni hapana.Wao wamekalia msemo MABADILIKO, ndicho walichong'ang'ania hawamwagi sera.Swali kwa wabishi wa JF kama lowasa angepitishwa na CCM leo mngemuona Chadema?Kama Sumaye angepitishwa na CCM kuwania Uraisi leo mngemuona Chasdema?Walichokifanya chadema ni sawa na mtu anasafiri kwenda sehemu fulani kwa miguu halafu likatokea gari la taka akaamua kudandia bila kujali atapata madhara gani ili mradi afike, uchu wa madaraka ndio tatizo.Mtu akiwa na njaa basi hutamani chakula cha aina yoyote hata najisi na majuto huja baadae, Watanzania twapaswa kuamka hawa jamaa walituaminisha jamaa ni fisadi leo wanageuka na kusema jamaa ni msafi kisa tuna njaa ya mabadiliko basi na wao wanakuja na gia ya mabadiliko!Ukweli hawatufai.Na ndio maana siku zote nasema mwaka huu ushindani mkubwai ni baina ya Original CCM (CCM A - DR MAGUFULI) na CCM B (CHADEMA- LOWASA).Tuchague kiongozi muadilifu na mchapakazi.

Sera yao ni mabadiliko, hawana sera wala ilani. Na hata hayo wanaita mabadiliko yasiyo na kichwa wala miguu ni sisi wananchi wenye mamlaka hayo na si eti Fulani anatamani iwe hivyo, usitake mabadiliko ya lazima kwasababu wananchi kama wamekunyima wewe kubali hawakukupa, usilazimishe mawazo yako make badala yake sasa utaonekana wewe ni mshari na unalenga mapinduzi kwa mgongo wa uchaguzi, sisi wapiga kura mawazo yetu yaheshimiwe, hatutaki mihemko isiyo na maana, itabidi upigwe tu make umelikiroga mwenyewe
 
MGOMBEA urais kwa tiketi ya CCM, Dk John Magufuli, amewahakikishia wana-CCM na Watanzaia kwa ujumla kuwa mwaka huu, chama kitapata ushindi wa Tsunami na si wa kishindo wala kimbunga.

Dk Magufuli alisema hayo nje ya ofisi ya chama hicho mkoani Mtwara juzi alipokuwa akizungumza na wanachama wa chama hicho ambapo alisisitiza kuwa wapinzani watapiga kelele sana, wataongea sana lakini ushindi kwa CCM ni lazima na upo pale pale.

Alisema ushindi huo unatokana na matawi yaliyoanguka ndani ya chama na kuhama na kwamba watu hao wameiacha CCM ikiwa safi na salama zaidi. Alisema watu hao walikuwa wakitumia fedha nyingi kurubuni watu wakati wa mchakato wa kumpata mgombea urais wa CCM ambapo chama kiliwakata na kukimbilia vyama vingine vya upinzani.

Aliwataka wana-CCM wasikatishwe tamaa na watu wa aina hiyo na badala yake washikamane, wawe kitu kimoja na kwamba mwaka huu, chama kitafanya kampeni za kisayansi. Aidha, Mbunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba alisema ni kazi rahisi kumnadi Dk Magufuli kutokana na vigezo na sifa alizonazo.

Mwigulu, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha, alisema walioshindwa kwenye mchakato wa kura za maoni na kuhama ndani ya chama, hivi sasa wanahaha kutafuta urais wenyewe ambapo wanatoa mpaka hela ili kutafuta uongozi, lakini wataumbuka mapema.

Akizungumza na mamia ya wana-CCM waliojitokeza kumpokea katika hiyo ofisi ya chama ambapo alifika kwa ajili ya kuwasalimia na kuwashukuru kwa kumchagua kuwa mgombea na kumdhamini, Dk Magufuli aliwataka makada hao na Wtanzania kwa ujumla kutoyumba kwa kuwa Watanzania walio wengi bado wanakipenda Chama.

“Ushindi wa mwaka huu wala si wa kimbunga ni wa Tsunami, watapiga kelele sana, watakuja na propaganda nyingi sana, lakini ushindi wa CCM ni lazima. Ni lazima tupate ushindi wa rais, wabunge, wawakilishi na madiwani,” alisema. Alisema walikuwa watu 42, wakati wakiomba kuteuliwa na chama hivi sasa, CCM ina kundi moja tu la ushindi.

“Hako ka tawi kamoja ndio kakameguka kwenda uko mbali, mti ambao unataka upate mbao zake nzuri matawi kudondoka chini ni vizuri ili upate mbao safi. “Lakini baada ya kudondoka hilo ni jambo la kawaida kwa chama kikubwa kama CCM.

Hata ukiangalia tangu enzi za Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere wapo waliotoka wako akina Kambona walitoka na wengine walifukuzwa na wengine walijua watafukuzwa wakakimbia wenyewe kabla ya kufukuzwa kama hao,” alisema.

Alisema iwapo atachaguliwa kuongoza dola atapenda awe mtumishi wa watu, asiyekuwa na majivuno ili aweze kuwatumikia wananchi na atomize matarajio yao. Dk Magufuli alisema wakati wa kampeni ukifika zitafanyika za kistaarabu na kisayansi na kwamba zitakuwa za shina kwa shina, tawi kwa tawi, kata kwa kata, jimbo kwa jimbo, wilaya, mkoa na taifa.

Aliwataka wana-CCM wasimame imara kwani wananchi wengi wanakipenda Chama. Dk Magufuli akizungumzia uzoefu wake ndani ya CCM, alisema alikuwa mbunge katika kipindi chake cha miaka 20, ambapo vipindi viwli alipita bila kupingwa na alikuwa waziri kwa miaka 20 katika wizara mbalimbali.

Alisema anaifahamu vizuri Mtwara, Tanzania, CCM na kero za Watanzania anazifahamu vya kutosha hivyo akipewa nafasi watashudia wenyewe kasi ya utendaji kwa maendeleo ya taifa. “Nilichaguliwa na mkutano mkuu kutoka kila kona ya nchi kwa asilimia 87, wale walionichagua waliwakishia Watanzania wote.

Niwahakikishie kuwa mwaka huu, tutashinda zaidi,” alisema. Aliwataka wana-CCM katika umoja wao kutulia na kutoyumbishwa na maneno ya porojo kwa kuwa chama kinajiuliza kwa kile walichofanya kwa wananchi na si maneno matamu bila vitendo.

“Chama nakifahamu, shida za wana-CCM nazifahamu, matarajio yao nayafahamu, shida za wananchi nazifahamu hivyo kama nitachaguliwa nitawatumikia kwa uadilifu mkubwa ili kuwaletea maendeleo,” alisema.

Chanzo: Habari Leo

Mwambie aendele kuota ndoto za mchana. Hapati urais aende tuu akalime.
 
Kura zipigwe au Zisipigwe it does make a difference kwa serikali iliojaa Mafisadi km hio.

USA wameshasema ashinde Magufuli Pombe bin Gongo.

Hapa naskia harufu ya Damu kwa wingi sana.
Mungu ailinde Nchi yangu Tz.

Ccm wako Tayari kwa Lolote kubakia Ikulu

Hivi wewe akili zako za udini na kumwaga damu ndio dini yako au?....Kenge sana wewe .
 
HapakaziTu, wasiofanye kazi na wasile

Bila kufanya kazi nchi haiwez endelea, wanaotaka maendeleo ya nchi kura zoote kwa magufuli

Tunatambua kuwa ccm imekata pumzi!
Mambo yakawaida kabisa,yatakayoiangusha ccm ni haya:

* Hospitali za binafsi kuna dawa,ila za serikali hakuna,

* serikali ya ccm iliwaahidi watanzania kuwa watoto wadpgo ,wazee na akina mama wajawazito watatibiwa bure,lakini hilo limekuwa kiini macho!

* ccm iliahidi kuweka vitanda vya mama na mtoto kwa mgonjwa mmoja kitanda kimoja lakini hadi jana wanalala kitanda kimoja watu wawili

* ccm iliahidi Elimu bure s/ m,leo hii wanafunzi wanachangia maji,umeme,mlinzi,madawati,mitihani ya mock na dawa?

* ccm iliahidi wanafunzi wa sekondari kusoma bure kwa kulipa Ada tsh 20,000 tu,leo hii wanalipa tsh 250,000 !

Ukiondoa kutotimizwa kwa Ahadi lukuki
Nani atachagua ccm?
 
Point, nilikuwa sijalifikiria hilo mkuu, Tena baada ya Lowassa kuhamia Ukawa speed ya kujiandikisha iliongezeka

Yaani wewe una akili nyingi sana,speed ya kujiandikisha iliongezeka mara 10 zaidi baada ya Lowassa kuhamia Ukawa tena muda ukaongezwa.
Hapo ndio penye siri ya ushindi wa Ukawa.
 
Kwakifupi tu, hatuna ubaya na "Mgombea wenu" hata kidogo. Adui yetu mkubwa na lichama lenu la mafisadi, mtambo wa kuzalisha mafisadi wapya kila kukicha na kila sehemu. Mafisadi wa raslimali zetu wapo kila kona Halmashauri, Manispaa, Tamisemi, Wizarani na hadi IKULU (akina NGURUMO et al).Kama unaipenda TANZANIA MPYA, ikifika tarehe 25/10/2015 TOKOMEZA HUYU NDULI CCM.
 
Tunatambua kuwa ccm imekata pumzi!
Mambo yakawaida kabisa,yatakayoiangusha ccm ni haya:

* Hospitali za binafsi kuna dawa,ila za serikali hakuna,

* serikali ya ccm iliwaahidi watanzania kuwa watoto wadpgo ,wazee na akina mama wajawazito watatibiwa bure,lakini hilo limekuwa kiini macho!

* ccm iliahidi kuweka vitanda vya mama na mtoto kwa mgonjwa mmoja kitanda kimoja lakini hadi jana wanalala kitanda kimoja watu wawili

* ccm iliahidi Elimu bure s/ m,leo hii wanafunzi wanachangia maji,umeme,mlinzi,madawati,mitihani ya mock na dawa?

* ccm iliahidi wanafunzi wa sekondari kusoma bure kwa kulipa Ada tsh 20,000 tu,leo hii wanalipa tsh 250,000 !

Ukiondoa kutotimizwa kwa Ahadi lukuki
Nani atachagua ccm?

Acha kuzikiliza siasa kama mtoto mdogo, angalia uhalisia!
Kwa suala la hospitali nampa heko kubwa sana JK, kuna watu nawafaham wamefanyiwa opreshen pale muhimbili na wako vzr, watu wamefanyiwa opreshen hadi ya ubongo, ni kweli hajafikia tunapotaka ila kusema hospitali hazijaboreshwa nuongo, akisema mwanasiasa namuelewa manake wanasiasa wote n waongo tu! muhim n kutafuta mwenye nafuu katika uongo wake, na kwa ss Magufuli anasiza hizo,
Ndo maana nasema Magufuli atashinda na asiyemkubali magufuli anachuki binafsi hana jingine
 
Back
Top Bottom