hata kama tusipokubali ndugu zangu ni ukweli kuwa waliotoka ccm kipindi hiki wana lao moyoni japo wote wanajitetea kuwa hawakubaliani na maamuzi ya kamati kuu ya ccm kukata jina la lowassa dodoma. ukifuatilia kwa undani kihistoria utagundua kuwa waliohama baada ya lowassa kuhama ccm walikuwa ni wale wanaomuunga mkono na alishawaaahidi vyeo katika serikali kama angepata urais, na walikuwa kwenye mtandao wake kwa zaidi ya miaka mitano nyuma, lakini njia pekee ya kuufanya umma wa watanzania waamini ni kurudia kauli ileile kuwa hawakubaliani na kukatwa jina la mzee huyo, ukiangalia vizuri utaelewa maana yake ni nini.
ahueni imeanza kurejea ccm baada ya mtandao wa mzee lowasa ambao ungeendeleza madudu ndani ya ccm na serikali kuvunjika na wengi wao kumfuata mzee huyo. kwa msimamo wa magufuli masihara yatakoma ndani ya ccm . na ni wazi sasa kuwa ukawa wamepokea watu ambao waliharibu ccm na waliandaliwa kudumisha mtandao huo mbovu ndani ya ccm na wajiandae kuishi na watu hao, hongera zao ccm , pole kwa ukawa kwa kukumbatia bomu la mkono huku kiringi kikiwa kilishakatwa na mda wowote litawalipukia.