Magufuli siyo shujaa wa Afrika, Kikwete ni shujaa wa Afrika

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,502
51,098
Nilipokuwa nafuatilia msiba wa Magufuli, kwenye Television ya Taifa TBC, walikuwa wameweka maneno kumhusu Magufuli kuwa ni Shujaa wa Afrika lakini nikawa navuta fikra. Je, ushujaa wa Magufuli kwa Afrika ni upi?, Nikasema pengine ni kwa "Rhetoric" zake za kutukana Wazungu na kuwaita Mabeberu, lakini Mabeberu hao walipokuwa wakikohoa tu, mzee mzima anagwaya na anatii.

Kiufupi Magufuli alikuwa akiogopa sana Kibinyo cha Wazungu kuliko kelele za raia wake wenyewe. Tuliona kwa mfano “Mabeberu" wakimwambia abadilishe sheria za takwimu na akatii, Walimwambia aruhusu watoto wajawazito waendelee na masomo akabadili mwelekeo. "Mabeberu" ndiyo walioingilia kati Lissu apewe safe passage kurudi Ulaya na serikali ya Magufuli ikampa na passport kabisa, la sivyo habari leo hii ingeukwa nyingine!.

Mfano mwingine ni kwenye Makubaliano na Barick kuhusu mustakbali wa kampuni hiyo juu ya uchimbaji madini nchini, Kabla ya makubaliano hayo Serikali ya Magufuli ilipeleka muswada chapuchapu bungeni juu ya rasilamli zetu, na mle ndani sheria iliyotengenezwa ikasema Makinikia yatakuwa yanachenjuliwa hapahapa Tanzania, Lakini cha ajabu kwenye makubaliano na Barick mwaka mmoja au miwili baadae akavunja sheria yake mwenyewe, kwa kuruhusu makinikia yawe yanasafirishwa nje!. Sasa hiyo hype ya kuwa alipambana na Mabeberu inatoka wapi?

Najiuliza ushujaa wa Magufuli kwa Afrika ni upi wakati dalili zote za aina ya uongozi wake ilikuwa ni kutaka kuturudisha kwenye Afrika ya kale ambapo mtawala akiongea hakuna wa kuquestion la sivyo utakiona cha mtema kuni. Kiufupi Magufuli aliparalyse mifumo ambayo ingeijenga nchi kusimama kitaasisi na badala yake akaanza kutunga sheria na kufanya matendo ambayo yanazidi kumlibikizia yeye madaraka, chukulia mfano sheria ya rasilimali za Taifa, Hiyo sheria ilienda kuweka madini yote chini ya ofisi ya rais

Kwa kweli nikiangalia kitu chochote exclusive ambacho Magufuli amefanya kwa ajili ya Afrika nzima ni kama hakuna!

Lakini hii ni tofauti na Mstaafu Kikwete, Kikwete kuna mambo aliyafanya naweza kusema bila wasiwasi na kwa rekodi kuwa huyu mwana wa Afrika anastahili kupewa heshima yake na Afrika nzima

1. Kikwete alishiriki katika Usuluhishi wa Kenya
Baada ya uchaguzi mkuu wa Kenya mwaka 2007,wakati Wakenya wakichinjana na kuhasimiana kitu kilichohatarisha kuzuka kwa vita ya wenyewe kwa Wenyewe, Rais Kikwete aliingilia kati kusuluhisha kambi hasimu za Raila Odinga na Mwai Kibaki, Pamoja na Juhudi za Kikwete pia walikuwepo marais wastaafu wa Afrika akiwemo hayati Mkapa. Ni kutokana na kazi hii Nchi ya Kenya ilimpa heshima ndugu Kikwete kuhutubia mabunge mawili ya Kenya, heshima ambayo ilikuwa hajawahi kupewa rais yeyote wa Tanzania kabla yake. Pia kwa kutambua kazi ya kikwete kwenye kuleta amani Kenya, barabara moja nchini Kenya , jijini nairobi ilibadilishwa na kupewa jina lake

2. Kikwete ainusuru Comoro dhidi ya kikosi cha Wahuni cha kanali Bacar
Wakati Comoro ikiwa inaelekea katika mtanzuko wa machafuko baada ya kikosi cha Muasi Kanali Bacar kuasi, Ni dhahiri visiwa hivi vya Comoro vingekuwa katika machafuko makubwa ikiwemo umwagaji damu, Ilikuwa ni Intervention ya Rais Kikwete kupeleka jeshi letu la JWTZ kwenda kuweka mambo sawa. JWTZ walipiga kazi nzuri na ndani ya wiki moja nchi ile ikawa imeshakuwa stabilized. Je ni watu wangap wangeuawa kama si kwa intervention ya Tanznaia, Ni wanawake wangapi wangebakwa?.Ikumbukwe siyo JK wa kwanza kuisapoti Comoro kijeshi, Hata mwalimu Nyerere amewahi kuisaidia Comoro ili kupambana na wakoloni wa ufaransa.

3. Kikwete ainusuru Congo dhidi ya Wahuni wa M23
Hawa wanayarwanda walikuwa wakiiba mali, kuua watu congo, Ni mpaka Viongozi wenye maono kama Kikwete waliojitolea kuendesha mission ya UN ya kuwadhibiti hao waasi. JWTZ kwa kushirikiana na majeshi ya Afrika ya kusini na Malawi walifanya kazi nzuri sana ya kuwadhibiti hao akina Jenerali Nkunda. Bila shaka ukiwauliza watu wa mashariki ya Congo kuhusu Intervention hiyo ya Kikwete, watakwambia huyu mtu ni shujaa wao

4. Usuluhishi wa Mgogoro Madagascar
Hali ya Madagascar ilikuwa imeshakuwa tete, magonvi na kupinduana kukiwa kumeiweka ile nchi katika hali ya sintofahamu, hali ya hofu mitaani. Ilikuwa ni kazi nzuri ya Kikwete kutafuta usuluhishi wa kisiasa huko

Maandiko yanasema heri wapatanishi!

Nikimpima Kikwete na Magufuli katika kutafuta ustawi wa bara la afrika, ikiwemo usuluhishi na upatanaishi, kutafuta amani ya watu wake, Kwa kweli Kikwete aliifanyia makubwa Afrika. Huyu anafaa kuitwa shujaa wa Afrika katika viongozi wa rika la hivi karibuni.

Magufuli yeye ni shujaa wa Afrika katika lipi?
 
Kikwete pia si shujaa wa Africa kwa lipi hasa? Shujaa wa Africa ni Baba wa Taifa pekee yake.
Nilipokuwa nafuatilia msiba wa Magufuli, kwenye Television ya Taifa TBC, walikuwa wameweka maneno kumhusu Magufuli kuwa ni Shujaa wa Afrika
Lakini nikawa navuta fikra, Je ushujaa wa Magufuli kwa Afrika ni upi?, Nikasema pengine ni kwa "Rhetoric" zake za kutukana Wazungu na kuwaita Mabeberu, lakini Mabeberu hao walipokuwa wakikohoa tu, mzee mzima anagwaya na anatii...
 
Back
Top Bottom