Magufuli sio kiongozi, ni mwanaharakati tu kama wengine

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,229
116,840
Ukimsikia anavyo lalamika na kuongea kwa uchungu unaweza fikiri ndie Rais aliepewa mzigo mkubwa kuliko wote katika historia ya Tanzania kumbe sivyo kabisa

Kama Rais Ally Hassan Mwinyi angekuwa na 'kipaji cha kulia na kulalamika' kwa uchungu basi sijui ingekuaje.

Mwinyi aliikuta...
Nchi imefilisika kabisa.
Chakula hakuna mvua hazinyeshi.
wananchi wanapanga foleni kupata unga wa njano wa msaada kutoka USA..
maarufu ugali wa Yanga.
sigara na bia zinaweza kukupeleka polisi.

Nchi ilikuwa hali mbaya mno kutoka Dar hadi Mbeya siku tatu jinsi barabara ilivyo mbovu.

Ruvuma kuja Dar njiani siku tano, huko Lindi na Mtwara ni meli tu hata mabasi hayafiki mishahara ndo kabisa hakuna.Watu kukaa miezi mitatu bila mishahara ni kawaida.

Sabuni hakuna watu hadi wakawa wagunduzi wa majani ya mipapai kufulia
viatu ndo usiseme tunavaa katambuga vipande vya matari ya magari.

Hali ilikuwa mbaya kupita maelezo lakini Rais Mwinyi hakuwahi hata mara moja.

Kulia kuwa 'kapewa mzigo mzito' wala kumlaumu mtangulizi wake Mwinyi alikuwa 'anatabasam' tu huku anatatua tatizo moja hadi lingine.

Wananchi walikuwa wala hawahamasishwi kumsiikiliza Rais akihutubia, alionyesha 'uongozi' kimya kimya tu hadii mambo yakabadilika.

Sifa ya kiongozi sio kulialia na kulalamika kila mara.Hizo ni sifa za wanaharakati ambao hupenda kuwachota wananchi kwa kuwatia uchungu na kuwaonesha adui wao ambae pengine wala sio adui wao kweli mradi tu 'mhusika ajitoe lawama' ya kushindwa kuja na solution ya matatizo yaliyopo.

Ndo maana wanaharakati wengi hushindwa kabisa kuongoza wakipewa nafasi imetokea mara nyingi wala sio kitu kipya.
 
upload_2017-6-13_14-5-10.jpeg
 
Ukimsikia anavyo lalamika na kuongea kwa uchungu unaweza fikiri ndie Rais aliepewa
mzigo mkubwa kuliko wote katika historia ya Tanzania...kumbe sivyo kabisa

Kama Rais Ally Hassan Mwinyi angekuwa na 'kipaji cha kulia na kulalamika' kwa uchungu
basi sijui ingekuaje...

Mwinyi aliikuta nchi imefilisika kabisa...
chakula hakuna..mvua hazinyeshi
wananchi wanapanga foleni kupata unga wa njano wa msaada kutoka USA..
maarufu ugali wa Yanga
sigara na bia zinaweza kukupeleka polisi

nchi iikuwa hali mbaya mno....kutoka Dar hadi mbeya siku tatu jinsi barabara ilivyo mbovu
Ruvuma kuja Dar njiani siku tano...huko Lindi na Mtwara ni meli tu
hata mabasi hayafiki....mishahara ndo kabisa hakuna...
watu kukaa miezi mitatu bila mishahara ni kawaida...

Sabuni hakuna..watu hadi wakawa wagunduzi wa majani ya mipapai kufulia
viatu ndo usiseme..tunavaa katambuga ...vipande vya matari ya magari...

Hali ilikuwa mbaya kupita maelezo....lakini Rais Mwingi hakuwahi hata mara moja
kulia kuwa 'kapewa mzigo mzito'...wala kumlaumu mtangulizi wake
Mwinyi alikuwa 'anatabasam' tu huku anatatua tatizo moja hadi lingine...

Wananchi walikuwa wala hawahamasishwi kumsiikiliza Rai akihutubia...
alionyesha 'uongozi' kimya kimya tu hadii mambo yakabadilika....

Sifa ya kiongozi sio kulialia na kulalamika kila mara..
hizo ni sifa za wanaharakati ambao hupenda kuwachota wananchi
kwa kuwatia uchungu na kuwaonesha adui wao ambae pengine wala sio
adui wao kweli...mradi tu 'mhusika ajitoe lawama'....ya kushindwa
kuja na solution ya matatizo yaliyopo......

Ndo maana wanaharakati wengi hushindwa kabisa kuongoza wakipewa nafasi..
imetokea mara nyingi...wala sio kitu kipyaa

Hataki kushauriwa na hataki kukosolewa,halafu anataka tumuombe!Sijui kama anajua yeye ni RAIS wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
 
The Boss,

Hayo mambo acha tu!!!

Mimi mama yangu ni mtu wa Lindi! Enzi hizo tupo wadogo ikabidi twende likizo kule! HUwezi amini nini kilitukuta!!!

Tulitoka Lindi kurudi Dar es salaam wiki moja kabla ya mashule kufunguliwa!!!

Hadi tunafika Dar sister angu ambae alikuwa mmwanafunzi; alikuwa tayari amechelewa wiki mbili... which means, Lindi - Dar ambayo ni safari ya saa 5-6 ilituchukua wiki 3!!!!!

"Better" option ilikuwa ni kupitia Songea! Sasa hebu fikiria... mtu unaenda Lindi au unatoka Lindi kwenda Dar lakini unalazimika kupita Songea... wapi na wapi!!!!

Mbaya zaidi, Lindi to Songea ni mbali zaidi kuliko Lindi to Dar es salaam!!! Lakini unalazimika kusafiri umbali mrefu zaidi kuliko kule unakoenda ili tu ukakutane na barabara ambayo nayo itakuongezea umbali mara 2 zaidi na kufanya safari mzima kuwa zaidi ya 1300 km badala ya 450 km!!!

Lakini hata ukisema upite barabara ya Songea; ilikuwa kutoka Masasi hadi kuipata Songea mnaweza kutumia siku 2 hadi 3!!!

Ulichosema ni ukweli mtupu!!! Bwana Mkubwa huyu ndo angeikuta Tanzania ile sijui angefanyaje!!

Na anavyoboa utadhani kuna mtu alimlazimisha!! Always trying act cry innocent aliyebebeshwa zigo as if kuna mtu alimlazimisha!!!

Kapewa nchi almost mahitaji yote muhimu bado analilia wakati akina Mwinyi wameingia madarakani wakikuta mkoa mzima una shule chini ya 5 za sekondari!!!!

Li-Dar es salaam lote hili nalo shule zilikuwa zinahesabika!!!

Enzi hizo tunatoka Kurasini, shule St. Anthony's... basi mvua zikichanganya mnalazimika kuteremkia Mtongani manake unakuta kuanzia pale relini hadi Mission hapapitiki!!
 
Sasa kama hajui solution na hataki kushauriwa
tushauri nini?
sisi tuna observe na kutoa maoni tu
Uliwahi kumshauri Rais Magufuli kwa kutumia proper channel za kiutawala na akakataa ushauri wako au na wewe unalalamikana na kulalama tu wakati hujui hata proper channels za kutolea ushauri wako.

Nani alikudanganya kama Rais Mwinyi hakulalamika wakati wa utawala wake

Ninakumbuka baada ya kuanza kazi alianza kulalamika akitoa mfano wa mtu ambaye wenziwe wamemsadia kupanda juu ya mti na kisha kumtelekeza ilihali chini kuna machupa.
 
Back
Top Bottom