Magufuli Pumzika, yatosha sasa!

Naomba uagize supu ya mamba nakuja kulipa au njoo mji wa Canberra uje ule vitu maana duuuh, Lisu karibu home watanzania tunakuita
 
Eti maisha magumu kuliko awamu zote!
Ungepiga ugali wa Yanga kutoka kwenye duka la kaya usingeongea hayo.
Kizazi cha maziwa ya nido bana.
 
Ni ajabu unalinganisha Tanzania na nchi zilizoendelea hapo hapo unasema Serikali haijaajiri, ni Serikali gani Dunia hii hutoa ajira kwa Wananchi? Tangia lini Serikali ikawa mwajiri mkuu? Isitoshe unaelewa kwa nini huitwa Shirika la ndege huitwa ,,national airline“ ?

unataka utuambie nchi kama rwanda au somalia kuna economic opportunities nyingi kiasi kwamba watu wengi wameajiliwa kwenye private sector ? usiwe unakuja jf kudanganya watu
zaire ajira nyingi zilitoka serikalini miaka ya 80 watu wengi waliajiliwa katika shirika la taifa la kilimo


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwisha habari yako...kama mawazo yako ndiyo haya!!! Mtu aliyediriki kuutangazia ulimwengu wamama na watoto wa kitanzania wakose fedha za kujikimu kwa kuwashawishi washirika wetu wa maendeleo watususie kiuchumi...ndiye karata yako ya turufu!!! Hamna kitu wewe...kwisha habari yako.
Hivi unafahamu kwamba mpaka sasa mmeishasuswa kiuchumi ?
 
Kusema anaamini si sawa na kuamini.

Ingekuwa hivyo, uhalifu 7ngekuwa mdogo sana duniani.

Wahalifu wakubwa wengi ni hao hao wanaosema wanaamini Mungu, lakini matendo yao yanaonesha wanasema kwa geresha tu.



Sent using Jamii Forums mobile app
Kiongozi hujajibu swali langu. Kuna sehemu au wakati wowote Pope alishakiri "MUNGU YUPO"?

Zingatio hilo liwepo kwenye kukiri Mungu yupo au Kuamini uwepo wa Mungu.
 
Kiongozi hujajibu swali langu. Kuna sehemu au wakati wowote Pope alishakiri "MUNGU YUPO"?

Zingatio hilo liwepo kwenye kukiri Mungu yupo au Kuamini uwepo wa Mungu.
Ndiyo, wakristo wote, Papa akiwamo, wanasema imani ya mitume.

Apostles Creed (Imani ya Mitume) inasema kuamini imani ya kuwepo Mungu.

Hilo halimaanishi wote wanaamini.

Wengine wanasema kama fashion tu.
 
Tutafika tu,

Ivi kwanin kila mara mnazungumzia democracy? Ukweli toka moyoni mwangu si muumini wa neno hili DEMOKRASIA, ni mipango michafu sana za mataifa ya magharibi kuendelea kuzitawala nchi nchi nyingi za Kiafrika kwa kutumia makundi kinzani na serikali zilizowekwa na pendekezwa na wananchi wake kuliongoza taifa lake kwa misingi yake na tamaduni zake, hapo sasa ndipo mataifa ya magharibi kutumia vikundi kinzani au vyama pinzani kuvuruga hali ya kiusalama ndani ya taifa kwa kile kinachoitwa serikali haifuati DEMOKRASIA,
Hakika naamini kabisa kuwa hata wao kabla hawajapata maendeleo waliyo nayo sasa hawakuwa na huyu MDUDU DEMOCRASIA, lakini baada ya kupata maendeleo na kutaka kuendelea kumtawala mtu mweusi na mali yake ni kumletea hiki kitu DEMOCRASIA ili atengeneze makundi mawili yenye kutaka kuongoza taifa lakini akiwa na lake jambo kwa kuutumia upande wa pili kuleta vurugu kwa aliyefanikiwa kukaa kwenye kiti cha uongozi wa juu na hasa akionekana akukinzana na malengo yao mabeberu,

Mifano halisi tu ni huko Libya baada ya kumuondoa Gaddaf kwa kile walichokiita hakuongoza KIDEMOKRIA, angalia sasa walichokifanya kwa muweka utawala wao wenyewe kwa manufaa yao, Libya siibya ile ya Gaddafi lwa sasa,
Algeria, hali ni mbaya kwa neno lilelile DEMOKRASIA,
DRC Congo, hali ni ile ile, kila kukicha Congo ni sawa na jalala la kuleta kila aina ya uchafu wa wamagharibi huku wakifaidika na utajiri wa nchi ile,

Najiuliza maswali kwanini hili neno DEMOKRASIA ni Africa tu?
Mbona wasizungumzie na mataifa ya ASIA? ambayo hayafuati tawala wazitakazo hawa WAMAGHARIBI?
Na mbona chumi za mataifa haya(ASIA) unazidi kupaa tu ili hali hamna Demokrasia?
Mifano ya mataifa ya mashariki ya mbali yasiyokuwa muumini wa demokrasia ni kama CHINA, KOREA KAS NA KUSI, URUSI, na mengine yenye mifumo ya kifalme,
Mbona sisi tu Afrika ndio tumekuwa wenda wazimu kiasi hiki kukubali mfumo ambao hata enzi za mababu zetu hawakuwahi kuzitumia na walienzi hasa mifumo yao ya kitawala kichifu kujiletea maendeleo katika maeneo na himaya zao?
Au mnataka mnambie eti tumestarabika?
Tusitarabike kwa mengine ila si kwa kila kitu hasa tamaduni na mifumo iliyokuwapo kiutalawa, kiongozi akiwa anania ya kulijenga taifa tumwache na tumuunge mkono kufika pale aliponuia kutufikisha,
Taifa ni mshikamano na si utengano hasa katika maslahi mapana ya vizazi vijavyo,
Maisha ni kupita na vizazi vitapita,
JPM anania njema na tumwache atimize lile aliloliona kuwa ndio dira ya taifa,
Hakuna kiongozi yeyote aliyepewa dhamana na kuaminiwa na wananchi wake akataka kuwakomoa,
Tusikubali kugawanywa makundi hasa kipindi hiki kijacho cha uchaguzi. Beberu amepatarget sana kuona tunatofautiana ili aingize kucha lake kuchota mali tuliyo nayo, tukawa kama wenzetu Libya, na anaiona sana nafasi kuutumia upinzani kuleta sintofahamu ndani ya taifa,.
Hii ni kwa sababu ya Kiongozi wetu mwenye mlengo wa kushoto na matakwa ya WAMAGHARIBI,

JPM nakuombea sana MUNGU akupe maisha marefu kuliongoza taifa langu Tanzania.

Povu ruksa
Kwa hiyo wewe ktk mawazo yako unaamini kuwa maendeleo ya nchi yanaletwa kwa kufuata mawazo ya mtu mmoja? Je pale wanapojitokeza wenye mawazo tofauti tena yenye tija basi watekwe na kupotezwa ama wamiminiwe risasi kwakuwa wanatumiwa na mabeberu?

Taifa kubwa kama la Tanz lenye watu zaidi ya milioni 55 halitaweza kuendelea kwa kutegemea kichwa cha mtu mmoja na siyo DIRA ya Maendeleo ya Taifa. Hutaweza kuendeleza nchi kwa kuyachukia na kubagua mawazo ya wenzako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huko North mara kumetapika watu 110 wanarudi mtaani kuuanza mwaka mpya kwa staili mpya. Wakaribisheni kitaa muwape semina elekezi
 
Back
Top Bottom