hawezi pekee, matatizo ya umeme yamenzia ikulu, unless makuguli awe raisHabari zenu wadau, Sijui kwanini natamani sana kuona wizara ya Nishati na Madini, angepewa John Magufuli hata kwa muda mchache tu.
Najiuliza sana sijui ingekuaje au angefanya nini, au ndo angeanza kwa kutimua maelfu ya watu,
au mpaka sasa umeume ungekua umesharudi ndani ya wiki moja, natamani kuona.
Kuna mtu mwenye wazo kama langu? sorry kama nimewakwaza.
Wakuu wanaogopa kumuweka hapo maana yule hana simile, atawaanika wooote! Na hapa ndio dhamira ya serikali inakuwa na mashaka maana haiingii akilini hata kidogo wizara nyeti kama ya Nishati na Madini inaongozwa na huyu joker Ngeleja na fresher Malima. Wawili hawa wana utaalam gani au creativity gani kwenye nishati na madini?
On the other hand wakimtoa Magufuli kwenye barabara bei ya ujenzi zita-shoot kama wakati wa Shukuru Kawambwa. Sasa hivi angalia samaki na ufugaji alikokuwa Magufuli, Dr Mathayo ni kama hayupo, makokoro yamerudi, shamba la bibi limechanua tena.
Nionavyo mimi siri ya mafinikio ya Magufuli sio tu kusimamia sheria bali pia kutuoogopa kuwambua 'wakubwa' hata kama ni CCM yenyewe na hapa ndio wanapata kigugumizi maana wengi wao wamewekeza kwenye nishati na madini.
Wanasema Maghufuli angalau anafanya maamuzi na kuyasimamia hata kama ni mabaya kama hili la nyumba za serikali! Lakini mbele ya JK Maghufuli hatafurukuta tena baada ya sakata lile la bomoabomoa.kwani huko aliko kishafanya nini hadi sasa? zaidi ya kumulikwa tu na kamera za wanahabari? alikopitia je, alifaya nini, mmesahau alichoifanyia tanzania na nyumba za serikali? kweli watanzania tunasahu kirahisi sana, hata haya ya ngereja na jairo tutasahau pia.
mi nionavyo huyo naye ni walewale, kama alishindwa kuzilinda nyumba za serikali na leo taifa litapata gharama za kutisha kuwaweka maafisa wa serikali mahotelini kwa ajili yake, hata huko naye atatafuta madili mapya na kutengeneza pesa tu kama wenzake, mi kwa kweli sioni utofauti wake na waheshimiwa wengine! samahani kwa nitakaowakwaza
kwani huko aliko kishafanya nini hadi sasa? zaidi ya kumulikwa tu na kamera za wanahabari? alikopitia je, alifaya nini, mmesahau alichoifanyia tanzania na nyumba za serikali? kweli watanzania tunasahu kirahisi sana, hata haya ya ngereja na jairo tutasahau pia.
mi nionavyo huyo naye ni walewale, kama alishindwa kuzilinda nyumba za serikali na leo taifa litapata gharama za kutisha kuwaweka maafisa wa serikali mahotelini kwa ajili yake, hata huko naye atatafuta madili mapya na kutengeneza pesa tu kama wenzake, mi kwa kweli sioni utofauti wake na waheshimiwa wengine! samahani kwa nitakaowakwaza
Tatizo la Wizara ya Nishati ni kutopewa kimbaumbele na Wizara ya Fedha. Mimi naona tatizo ni Mustafa Mkullo, wakimwondoa Mkullo na kumweka mtu mwenye upeo wa kuangalia matatizo ya taifa na kupanga vipaumbele sahihi nchi itaenda mbele kimaendeleo
Mkullo ni 'ultimate Security' ya Magogoni. Sioni akiondoka hapo langoni kabla ya 2015. Kwa umachinoo wake kamaliza akiba yote hazina na sasa wanakopa kwenye bank za ndani. Sasa hivi serikali ndio mkopaji mkuu kwenye mabenki yetu!