Magufuli: Nilikupa angalizo lakini...

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
24,477
34,519
Katika post yangu ya tarehe24/11/2015 Magufuli kuwa makini na hawa watu... nilijaribu kuelezea namna ambavyo yawezekana rais akaingia mtegoni kwa ustadi wa wanaomzunguka.

Narejea tena kumweleza rais wangu Magufuli kwamba azidi kutumia busara na dhamira safi kuwatumikia Watanzania kwani hadi sasa wananchi wameshatambua nini walichokikosa kwa muda mrefu na matumaini ya kweli chini ya uongozi wa JPM.

Ni aina ile ile ya watendaji ambao wamo katika serikali ndiyo waliokuwepo tangu enzi za Mkapa hadi sasa. Ili tupate mabadiliko ya kweli ni budi ikafanyika sensa ya kujua tija za hawa watendaji ili kupitia humo uweze kupata timu bora yenye kukusaidia kufikia malengo.

Katika kampeni zako ulituambia sisi watu wa chini kwamba utapambana na wakepaji kodi wakubwa na sisi watu wa hali ya chini utatupatia unafuu wa kodi. Sasa najiuliza kuwa leo wauza karanga huku mtaani wanauliziwa TIN number , ndiyo ulichokiagiza au wasaidizi wako wamefululiza? Kwa nini Halmashauri za wilaya wasipange utaratibu wa kukusanya kodi hizi ndogondogo badala ya TRA?

Kamatakamata ya Bodaboda katikati ya Jiji la Dar ni kwa mantiki gani haswa? Polisi wanasema hizo tuktuk zinatumiwa sana na majambazi halafu mamlaka zilizopo zinaamka ahsubuhi na kusema hakuna boda kuingia mjini. Wamewekewa sharti la kibali halafu wakabadilishiwa namba za kutoka T hadi MC pia bodaboda za biashara zinatambulika kwa weupe wa plate yake. Wakishapata hiko kibali wakifika mjini hawaruhusiwi kupakia abiria. Sijui hii ni sheria ya wapi hii. Kuhusu ujambazi ni wazi kwamba polisi inazembea kutimiza wajibu wake. Polisi ya zamani walikuwa wanaweza hata kufichua mipango ya kijambazi na kudhibiti ila polisi ya leo kutwa kuchwa wapo njiapanda wakipambana na madereva wa magari ya mizigo wakipokea rushwa na kusaka magari yasiyo na bima badala ya kazi hiyo kuwaachia trafiki.
Iangalie safu yako, iangalie polisi huku ukiihurumia jamii.

Napenda kutoa pendekezo kwa mamlaka husika. wasaidieni vijana wa bodaboda kufanya shughuli zao kwa urasmi. Ili waweze kuingiza kipato halali na kuondokana na hatari ya kuingia kwenye uhalifu. Tengenezeni kadi maalumu ambayo kila muendesha bodaboda atawajibika kuifunga ktk chombochake ambapo kadi hiyo itolewe kwa mjumuiko wa Polisi na TRA yenye kuonyesha yafuatayo
  1. kadi iwe ukubwa wa A5
  2. picha ya dereva ukubwa wa nusu ya size ya kadi
  3. jina kamili na jina la mmiliki
  4. namba ya pikipiki
  5. namba ya kadi
  6. manispaa anapotoka
  7. detail yoyote muhimu ya kumtambua
Itakapobainika kuwa dereva wa bodaboda siye yule aliyepo kwenye kadi ya chombo basi ukamataji ufanyike. Hii itasaidia kupunguza wimbi la ujambazi ama matumizi ya bodaboda kwenye ujambazi

Narejea kwenye suala la ubomoaji nyumba za mabondeni na upatikanaji wa viwanja vilivyopimwa. Kumbuka kwamba kule kuna serikali za mitaa, Kata na hata miundombinu ambayo wakazi wale wamekuwa wakilipia bili. Hivyo wasaidizi wako walipaswa kuweka utaratibu wa kuwaondoa wakazi wale kistaarabu kwa utaratibu wa kupitia serikali za mitaa na Kata ili hatua ya ubomoaji ije baada ya hatua za awali kugonga mwamba. Pia kumbuka kwamba serikali yako inauza viwanja vya kupima kwa bei ghali sana hivyo Mtanzania wa hali ya chini hawezi kumudu kulipia gharama za kiwanja na hata ufuatiliaji wake, hivyo kupelekea watumishi wachache wa Wizara ya ardhi na watanzania wachache kuhodhi viwanja vingi ambavyo hata kuviendeleza vinawashinda. Kuna baadhi ya hisia kuwa mkurupuko uliofanywa katika zoezi la ubomoaji ni uratibu wa kukufarakanisha kwa wananchi ili ionekane kwamba serikali yako haizingatii haki za binadamu....

Usibague katika kuwashughulikia mafisadi walioipukutisha nchi hadi hapa tulipo, wengi wa MAFISI hayo wapo ndani ya chama chako na wachache walitoroka kutoka humo. Ni vigumu sana mtu wa kawaida kuweza kuifisadi nchi bila ya msaada wa aliyeko madarakani au kwenye nafasi nyeti. Angalia Wakurugenzi wa Wilaya, Wachumi wa halmashauri za wilaya na wakurugenzi kwenye vitengo vya wizara vyenye miradi. Hao ndiyo mchwa wetu ambao tangu uhuru hadi sasa wapo huru kujitwalia mapande ya keki ya taifa bila bugudha. CAG akague mafungu yaliyopelekwa TAMISEMI hasa miradi ya maendeleo kama kuna kilichofanyika. Ofisi za Watendaji Kata ni vichaka vya wakurugenzi wasio waaminifu. Vikao vya Ward Councils vingi huwa ni vya kufoji, Madiwani wengi ni ceremonials tu kwenye kata zao, inaelekea labda hawatambui wajibu wao au makusudi.

USHAURI KWAKO RAIS
  1. Ukusanyaji wa mapato ya serikali na Halmashauri zote nchini usipitie kwa mawakala. Serikali yako iboreshe nyenzo za kukusanya mapato hayo kwani yanapopitia kwa mawakala ni dhahiri kuna fedha inayopotea along the way.
  2. Tafakari upya nafasi za wakuu wa mikoa, kwa kuwa tunao wakuu wa Wilaya, basi uwekwe utaratibu wa wateuliwa hao kumchagua mmoja wao awe mkuu wa mkoa ambapo ataendelea kulipwa mafao na masurufu ya ukuu wa wilaya huku akiongezewa mshahara wake hivyo tutakuwa tumeondoa urasimu wa utitiri wa wakuu wamikoa ambao kimsingi kazi zao zinafanywa na wakuu wa wilaya. Kama ushauri huu utakuwa mgumu basi kazi za mkuu wa Mkoa zifanywe na Afisa Tawala Mkoa
  3. Taarifa za mali za viongozi zisiwe siri. Taarifa ziwekwe wazi kwa umma ili kusaidia kuthibitisha na uhakiki wa mali hizo
  4. weka utaratibu wa kuwafikia watu wa chini ili kujua uhalisia wa mambo unayoelezwa ama kushauriwa.
  5. Hamia Dodoma
Nimetimiza wajibu kwa kusema yaliyomo moyoni mwangu
Ni rahisi sana kwa jinsi teknolojia ilivyo kwa sasa!. Lakini ukiacha teknolojia ni suala la kuweka utaratibu wa leseni maalumu ambayo inakuwa imeunganishwa na Kadi ya Pikipiki kwa pamoja na muda wote anayeendesha Bodaboda hiyo mjini lazima awe nayo na siyo vinginevyo!.
Baada ya kukamilisha utaratibu huo masharti mengine yanafuatia.
Mfano.
Namba ya ubavuni.
Rangi ya Wilaya inakotoka-kiufupi kama Tax ilivyo.

Uuzuri halmashauri zitajiongezea Kodi-kupitia kutoa vibali na TRA kuweza kufuatilia Mapato kwa wenye Pikipiki maana zitakuwa za Biashara. Hata ukisema 1% anacholipa mteja itakuwa kodi ni sawa na ukiangalia idadi ya Boda boda inayofanya Biashara kodi yake itakuwa siyo haba!
Hoja hii ya VAT kuwa ya viwango tofauti Mh.Zungu alilizungumza lakini naamini Serikali itaifanyia kazi mapema.
Hakuna ugumu hata kidogo ni suala la kujipanga.
 
  3. jina kamili
  4. namba ya pikipiki
  5. namba ya kadi
  6. manispaa anapotoka
  7. detail yeyote muhimu ya kumtambua

mkuu, sijakusoma mpaka mwisho lakini umeongea mambo ya msingi sana ambayo kama yakizingatiwa jamii itaishi kwa amani kuliko sasa hivi bodaboda na mamantilie wanavyowindwa kama mbarbaig anavyosaka digidigi porini. haiwezekani watu wadogo waonewe hivi wakati wahalifu wakubwa akina mramba na yona walioitia hasara nchi kwa bilioni 111 wakiachiwa huru huku wafungwa waliohukumiwa vifungo kwa sababu ya kuiba vitu vidogo kama kiberiti, sindano, piece moja ya sigara, na simu wakiendelea kusota magerzani. ndio maana mimi huwa nasema kwamba CCM ni ileile na mambo yake ni yaleyale.

tunaomba rais magufuli aache kuwaonea wananchi alioapa kuwatetea kwa nguvu zake zote....aache kuyumbishwa na CCM...kama akiona CCM hawampi mazingira mujarab ya kufanyia kazi kwa ufasaha, ni ruhusa kuhamia UKAWA.

tazama jinsi mama ntilie wanavyokufa njaa kwa kuzuiwa kuuza chakula kwa kisingizio kwamba CHAKULA HUSABABISHA KIPINDUPINDU! jamani embu tuache unafiki.....tangu lini chakula kikasababisha kipindupindu? UCHAFU ndio huleta kipindupindu sio CHAKULA. ambacho walitakiwa kufanya ni kuwaelimisha mama lishe kuzingatia usafi wa vifaa na mazingira ya kufanyia kazi badala ya kuwazuia huku wakijua fika kwamba wengi wa hawa akina mama wana mikopo SACCOS na kwenye VICOBA. sasa wanapozuiwa kuuza chakula watalipaje mikopo? Tafakari, chukua hatua!
 
Nakuunga mkono.
kwa uhalisia wa yanayojiri huku chini ni kama wananchi wanaadhibiwa kwa kosa wasilolijua.
Endapo hawa wajasiriamali wadogo wakawekewa mazingira mazuri na sheria za kudhibiti huduma zao zikidhi vigezo huku wakilipa kodi ndogo kwa manispaa husika ni wazi tutakuwa tumeitengeneza jamii yenye kutumia fursa zilizopo kihalali. Mara nyingi tukishapata dhamana huwa tunajisahau sana. Tunasahau kuwa ninani haswa tunapaswa kutimiza wajibu wetu kwake. tunasahau nani anapaswa kufaidika na maamuzi yetu.

Naamini bado Magufuli anaweza kutuvusha katika hili maana mangimeza walewale wanajiita wazee wa HAPA KAZI TU huku tukijua kwamba wapo pale kukwamisha juhudi za wananchi kujikwamua kiuchumi
 
Katika post yangu ya tarehe24/11/2015 Magufuli kuwa makini na hawa watu... nilijaribu kuelezea namna ambavyo yawezekana rais akaingia mtegoni kwa ustadi wa wanaomzunguka.

Narejea tena kumweleza rais wangu Magufuli kwamba azidi kutumia busara na dhamira safi kuwatumikia Watanzania kwani hadi sasa wananchi wameshatambua nini walichokikosa kwa muda mrefu na matumaini ya kweli chini ya uongozi wa JPM.

Ni aina ile ile ya watendaji ambao wamo katika serikali ndiyo waliokuwepo tangu enzi za Mkapa hadi sasa. Ili tupate mabadiliko ya kweli ni budi ikafanyika sensa ya kujua tija za hawa watendaji ili kupitia humo uweze kupata timu bora yenye kukusaidia kufikia malengo.

Katika kampeni zako ulituambia sisi watu wa chini kwamba utapambana na wakepaji kodi wakubwa na sisi watu wa hali ya chini utatupatia unafuu wa kodi. Sasa najiuliza kuwa leo wauza karanga huku mtaani wanauliziwa TIN number , ndiyo ulichokiagiza au wasaidizi wako wamefululiza? Kwa nini Halmashauri za wilaya wasipange utaratibu wa kukusanya kodi hizi ndogondogo badala ya TRA?

Kamatakamata ya Bodaboda katikati ya Jiji la Dar ni kwa mantiki gani haswa? Polisi wanasema hizo tuktuk zinatumiwa sana na majambazi halafu mamlaka zilizopo zinaamka ahsubuhi na kusema hakuna boda kuingia mjini. Wamewekewa sharti la kibali halafu wakabadilishiwa namba za kutoka T hadi MC pia bodaboda za biashara zinatambulika kwa weupe wa plate yake. Wakishapata hiko kibali wakifika mjini hawaruhusiwi kupakia abiria. Sijui hii ni sheria ya wapi hii. Kuhusu ujambazi ni wazi kwamba polisi inazembea kutimiza wajibu wake. Polisi ya zamani walikuwa wanaweza hata kufichua mipango ya kijambazi na kudhibiti ila polisi ya leo kutwa kuchwa wapo njiapanda wakipambana na madereva wa magari ya mizigo wakipokea rushwa na kusaka magari yasiyo na bima badala ya kazi hiyo kuwaachia trafiki.
Iangalie safu yako, iangalie polisi huku ukiihurumia jamii.

Napenda kutoa pendekezo kwa mamlaka husika. wasaidieni vijana wa bodaboda kufanya shughuli zao kwa urasmi. Ili waweze kuingiza kipato halali na kuondokana na hatari ya kuingia kwenye uhalifu. Tengenezeni kadi maalumu ambayo kila muendesha bodaboda atawajibika kuifunga ktk chombochake ambapo kadi hiyo itolewe kwa mjumuiko wa Polisi na TRA yenye kuonyesha yafuatayo
  1. kadi iwe ukubwa wa A5
  2. picha ya dereva ukubwa wa nusu ya size ya kadi
  3. jina kamili
  4. namba ya pikipiki
  5. namba ya kadi
  6. manispaa anapotoka
  7. detail yeyote muhimu ya kumtambua
Itakapobainika kuwa dereva wa bodaboda siye yule aliyepo kwenye kadi ya chombo basi ukamataji ufanyike. Hii itasaidia kupunguza wimbi la ujambazi ama matumizi ya bodaboda kwenye ujambazi

Narejea kwenye suala la ubomoaji nyumba za mabondeni na upatikanaji wa viwanja vilivyopimwa. Kumbuka kwamba kule kuna serikali za mitaa, Kata na hata miundombinu ambayo wakazi wale wamekuwa wakilipia bili. Hivyo wasaidizi wako walipaswa kuweka utaratibu wa kuwaondoa wakazi wale kistaarabu kwa utaratibu wa kupitia serikali za mitaa na Kata ili hatua ya ubomoaji ije baada ya hatua za awali kugonga mwamba. Pia kumbuka kwamba serikali yako inauza viwanja vya kupima kwa bei ghali sana hivyo Mtanzania wa hali ya chini hawezi kumudu kulipia gharama za kiwanja na hata ufuatiliaji wake, hivyo kupelekea watumishi wachache wa Wizara ya ardhi na watanzania wachache kuhodhi viwanja vingi ambavyo hata kuviendeleza vinawashinda. Kuna baadhi ya hisia kuwa mkurupuko uliofanywa katika zoezi la ubomoaji ni uratibu wa kukufarakanisha kwa wananchi ili ionekane kwamba serikali yako haizingatii haki za binadamu....

Usibague katika kuwashughulikia mafisadi walioipukutisha nchi hadi hapa tulipo, wengi wa MAFISI hayo wapo ndani ya chama chako na wachache walitoroka kutoka humo. Ni vigumu sana mtu wa kawaida kuweza kuifisadi nchi bila ya msaada wa aliyeko madarakani au kwenye nafasi nyeti. Angalia Wakurugenzi wa Wilaya, Wachumi wa halmashauri za wilaya na wakurugenzi kwenye vitengo vya wizara vyenye miradi. Hao ndiyo mchwa wetu ambao tangu uhuru hadi sasa wapo huru kujitwalia mapande ya keki ya taifa bila bugudha. CAG akague mafungu yaliyopelekwa TAMISEMI hasa miradi ya maendeleo kama kuna kilichofanyika. Ofisi za Watendaji Kata ni vichaka vya wakurugenzi wasio waaminifu. Vikao vya Ward Councils vingi huwa ni vya kufoji, Madiwani wengi ni ceremonials tu kwenye kata zao, inaelekea labda hawatambui wajibu wao au makusudi.

USHAURI KWAKO RAIS
  1. Ukusanyaji wa mapato ya serikali na Halmashauri zote nchini usipitie kwa mawakala. Serikali yako iboreshe nyenzo za kukusanya mapato hayo kwani yanapopitia kwa mawakala ni dhahiri kuna fedha inayopotea along the way.
  2. Tafakari upya nafasi za wakuu wa mikoa, kwa kuwa tunao wakuu wa Wilaya, basi uwekwe utaratibu wa wateuliwa hao kumchagua mmoja wao awe mkuu wa mkoa ambapo ataendelea kulipwa mafao na masurufu ya ukuu wa wilaya huku akiongezewa mshahara wake hivyo tutakuwa tumeondoa urasimu wa utitiri wa wakuu wamikoa ambao kimsingi kazi zao zinafanywa na wakuu wa wilaya. Kama ushauri huu utakuwa mgumu basi kazi za mkuu wa Mkoa zifanywe na Afisa Tawala Mkoa
  3. Taarifa za mali za viongozi zisiwe siri. Taarifa ziwekwe wazi kwa umma ili kusaidia kuthibitisha na uhakiki wa mali hizo
  4. weka utaratibu wa kuwafikia watu wa chini ili kujua uhalisia wa mambo unayoelezwa ama kushauriwa.
  5. Hamia Dodoma
Nimetimiza wajibu kwa kusema yaliyomo moyoni mwangu

Duh! Sasa WataZania milioni 25 wote tukitaka kumshauri Raisi afanye vile tunavyoona inafaa na wote tuseme usiposikiliza ushauri shauri yako nimekupa angalizo huyo Raisi atakua na kazi nyingine kweli ya kufanya?
Acheni kuwa wabinanfsi namna hiyo kwa kujiona kwamba nyie ndiyo muhimu klk wengine Raisi yuko mwacheni aongoze yeye anavyoona inafaa na ndiyo maana ya Uchaguzi, yaani tunachagua Kiongozi na siyo mtu wa kuongozwa na maoni ya kila takataka hapa nchini!
 
Katika kampeni zako ulituambia sisi watu wa chini kwamba utapambana na wakepaji kodi wakubwa na sisi watu wa hali ya chini utatupatia unafuu wa kodi. Sasa najiuliza kuwa leo wauza karanga huku mtaani wanauliziwa TIN number , ndiyo ulichokiagiza au wasaidizi wako wamefululiza? Kwa nini Halmashauri za wilaya wasipange utaratibu wa kukusanya kodi hizi ndogondogo badala ya TRA?

Mkuu hiyo ni mipango B baada ya mpango A ya utunguaji majipu! Unataka wakala kwa nani?
Unajua walikuwa wamejihakikishia kwenda nazo nyumba kwa siku kiasi gani?. Kila mtu hula ofisini kwake!
 
Duh! Sasa WataZania milioni 25 wote tukitaka kumshauri Raisi afanye vile tunavyoona inafaa na wote tuseme usiposikiliza ushauri shauri yako nimekupa angalizo huyo Raisi atakua na kazi nyingine kweli ya kufanya?
Acheni kuwa wabinanfsi namna hiyo kwa kujiona kwamba nyie ndiyo muhimu klk wengine Raisi yuko mwacheni aongoze yeye anavyoona inafaa na ndiyo maana ya Uchaguzi, yaani tunachagua Kiongozi na siyo mtu wa kuongozwa na maoni ya kila takataka hapa nchini!
Mkuu unakosea tena unakosea sana tu.
Ibara ya 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Tanzania inapingana na mtazamo wako. Inawezekana ushauri ukawa mbaya na usiwe mbaya lakini ni muhimu kuheshimu maoni ya wengine mkuu wangu...

Labda uniambie kuwa takataka nilizoeleza huko juu zimekugusa
 
Nakumbuka alisema kwenye serikali yake Mgambo watatafuta kazi za zingine za kufanya na si ugambo wa kukamata wamachinga na mama Ntilie, cha ajabu Mgambo wameshika kasi sana tofauti na serikali ya Awamu ya Nne wamachinga na mama Ntilie wamefurumushwa maeneo yote ya mjini huku mkoani kwetu.
 
Magufuli anataka watendaji wa serikali wa~stretch mind zao wafikiri kwa upeo wa juu na kupata suluhu ya matatizo ya wananchi....

Katika mazingira ya sheria na kanuni nyingi za halmashauri zina mapungufu makubwa na baadhi zipo kimaslahi tatizo linakuja kwenye utekelezaji kuunganisha highly stretched mind na poorly maded by~laws
 
Tengenezeni kadi maalumu ambayo kila muendesha bodaboda atawajibika kuifunga ktk chombochake ambapo kadi hiyo itolewe kwa mjumuiko wa Polisi na TRA yenye kuonyesha yafuatayo
  1. kadi iwe ukubwa wa A5
  2. picha ya dereva ukubwa wa nusu ya size ya kadi
  3. jina kamili na jina la mmiliki
  4. namba ya pikipiki
  5. namba ya kadi
  6. manispaa anapotoka
  7. detail yeyote muhimu ya kumtambua

Ni rahisi sana kwa jinsi teknolojia ilivyo kwa sasa!. Lakini ukiacha teknolojia ni suala la kuweka utaratibu wa leseni maalumu ambayo inakuwa imeunganishwa na Kadi ya Pikipiki kwa pamoja na muda wote anayeendesha Bodaboda hiyo mjini lazima awe nayo na siyo vinginevyo!.
Baada ya kukamilisha utaratibu huo masharti mengine yanafuatia.
Mfano.
Namba ya ubavuni.
Rangi ya Wilaya inakotoka-kiufupi kama Tax ilivyo.

Uuzuri halmashauri zitajiongezea Kodi-kupitia kutoa vibali na TRA kuweza kufuatilia Mapato kwa wenye Pikipiki maana zitakuwa za Biashara. Hata ukisema 1% anacholipa mteja itakuwa kodi ni sawa na ukiangalia idadi ya Boda boda inayofanya Biashara kodi yake itakuwa siyo haba!
Hoja hii ya VAT kuwa ya viwango tofauti Mh.Zungu alilizungumza lakini naamini Serikali itaifanyia kazi mapema.
Hakuna ugumu hata kidogo ni suala la kujipanga.
 
Ni rahisi sana kwa jinsi teknolojia ilivyo kwa sasa!. Lakini ukiacha teknolojia ni suala la kuweka utaratibu wa leseni maalumu ambayo inakuwa imeunganishwa na Kadi ya Pikipiki kwa pamoja na muda wote anayeendesha Bodaboda hiyo mjini lazima awe nayo na siyo vinginevyo!.
Baada ya kukamilisha utaratibu huo masharti mengine yanafuatia.
Mfano.
Namba ya ubavuni.
Rangi ya Wilaya inakotoka-kiufupi kama Tax ilivyo.

Uuzuri halmashauri zitajiongezea Kodi-kupitia kutoa vibali na TRA kuweza kufuatilia Mapato kwa wenye Pikipiki maana zitakuwa za Biashara. Hata ukisema 1% anacholipa mteja itakuwa kodi ni sawa na ukiangalia idadi ya Boda boda inayofanya Biashara kodi yake itakuwa siyo haba!
Hoja hii ya VAT kuwa ya viwango tofauti Mh.Zungu alilizungumza lakini naamini Serikali itaifanyia kazi mapema.
Hakuna ugumu hata kidogo ni suala la kujipanga.
Mkuu umeiweka vizuri sana hiyo.
Mapato yataongezeka na sheria zitafuatwa
 
bodaboda na mamantilie wanavyowindwa kama mbarbaig anavyosaka digidigi porini. haiwezekani watu wadogo waonewe hivi wakati wahalifu wakubwa akina mramba na yona walioitia hasara nchi kwa bilioni 111 wakiachiwa huru
Wakati wa kampeni alisema mamantilie watakuwa rafiki zake mgambo watafute kazi zingine sasa hivi imekuwa kinyume chake.
 
Back
Top Bottom