Magufuli ni mnafiki kama Kikwete

TL. Marandu

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
3,625
5,810
Kabla ya Kuzungumza dhumuni Kubwa La Post Hii Napenda Niweke wazi Kuwa, Kwa Miaka Mingi, Kuwashinda hata wengi wa wanaCCM, Nilitambua Uwezo Mkubwa wa Magufuli wa Kufanya Kazi. Nilikuwa na Shukurani Kubwa sana Kwa Magufuli kwa Upendo wake kwa Tanzania na Watanzania. Nilimpenda zaidi Kwa Tabia yake ya Kutokumwogopa yeyote.

Bahaati Mbaya sana Magufuli Ameruhusu tabia Moja mbaya, Ni Mnafiki, sio Mkweli Kama anavyosema "Msemakweli ni Mpenzi wa Mungu" Inapofikia Katika Maswala ya Siasa Magufuli sio mkweli wala mwenye haki, inayofanana na Magufuli wa Ujenzi wa Taifa na Huduma za Jamii.

Unafiki wa wazi ni Pale aliposisitiza Kuwa ati Majaji walimwambia Kuwa Hawana haja ya Kuonekana Live, akiwa anaweka dhana Kuwa Majaji wanamuunga Mkono kwa Kuingilia Utendaji wa Bunge. Swala la Kukatisha matangazo ya TBC ilikuwa ni kwa Lengo na Mpango Mahususi wa CCM Kuubana Upinzani Bungeni na Kuruhusu Uonevu. Kusema Vinginevyo Ni Unafiki,

Swala Lingine Lilikuwa Ni swala la Zanzibar, Magufuli anajua wazi, Kikwete na Mkapa, walishinikiza Jecha Kufuta matokeo kwa Maslahi ya CCM, Magufuli anajua kuwa NEC, na ZEC sio Tume Huru. Magufuli anajua Uhuni Uliotendeka Zanzibar, Kwa yeye Kujifanya Jecha alifanya maamuzi yake Kikatiba Ni Unafiki.

Watu wanasahau Kuwa Sio Madictator wote Ni wa Aina ya Mobutu, Wengine walikuwa Madictator wa Kuchaguliwa na Watu waoliwaabudu, Madictator hao walikuwa Tayari kutoa damu yao Kuwapa watu wao Wainywe kama wana Kiu. Lakini kwenye Ukubwa wangemtoa yeyote Roho. Mfano halisi alikuwa ni Adolf Hitler. I hope Magufuli Ataukataa Unafiki When it comes to Politics.

Mnamjua Mpanju yule Jamaa wa Bunge la Katiba, sasa Hivi kapewa Ukubwa Kwenye Wizara ya Sheria na Katiba.
Mnamkumbuka Makonda na siasa zake za maji taka, Naye Pia alikuwa Kwenye Bunge la Katiba, Magufuli sasa anampa Chapuo
Naaamini hata Bi Asha Bakari asingefariki, angepewa Madaraka Makubwa Kwa Kumtukana Jusa Bungeni! Huyo Ndiye Magufuli Mwanasiasa!

Inatia Uchungu sana, Kwani Katika Viongozi wote waliotokea Kuongoza Nchi za Afrika Kama akiwa makini, Magufuli anaweza Kuwa The great Leader na Atakayekumbukwa Karne Kadhaa Zijazo. Ari yake, Na Moyo wake wa Kusaidia Kujenga Nchi na Kusaodia wananchi Hauna Mfano.

Lakini, Labda Kwa Kile Kilichonifanya Kwa Moyo mzito sana nisimpigie Debe wakati Ule ingawa alikuwa My Best of the best, Unafiki, Na hamu ya Kubebwa bebwa kwa wana-CCM, Hali hiyo Imemblind upande mmoja. AnataKiwa awe ni mtu wa 1)Hapa Kazi Tu? 2) Hapa Haki tu, 3) Habebwi Mtu, Kubebwa bebwa kwa CCM, Kubweteka kwao Kuwa hata wakifanya Madudu gani wataendelea Kutawala tu. Ndiko Kulikosababisha Uwepo wa Uozo na Madudu aliyoyakuta. Sasa Kwanini aendelee Kulea Siasa hizi?

Sikiliza Maneno Yake Katika Sherehe za CCM, Msikilize Mpka Mwisho, Kuna Mahali aliropoka Ukweli, Kuonyesha Zanzibar ilikuwa Ni "Kukataa Kutawaliwa"

Unafiki wake Mwingine:

SIKU YA KUHUTUBIA BUNGE:
Suala La Zanzibar tutalishughulikia na
tutalimaliza haraka.....

SIKU YA XMAS:
Kama nilivyoahidi bungeni
suala la Zanzibar tutalimaliza
karibuni

SIKU YA WAZEE WA MKOA
WA DAR:
Suala la Zanzibar hatuwezi
kuliingilia kwasababu tume
huru na haiwezi kuingiliwa na
chombo chochote...
 
Mtazungumza maneno mengi na vijembe vingi lakini ukweli ni kwamba Rais hana mamlaka kisheria kuingilia maamuzi ya tume ya Uchaguzi, iwe NEC au ZEC. Tume hizi zina mamlaka huru yasiyohojiwa na rais yeyote. Iwe zimefanya maamuzi mabovu au zimefanya maamuzi manzuri rais hawezi kuizingilia kisheria.
 
Unafiki wake Mwingine:

SIKU YA KUHUTUBIA BUNGE:
Suala La Zanzibar tutalishughulikia na
tutalimaliza haraka.....

SIKU YA XMAS:
Kama nilivyoahidi bungeni
suala la Zanzibar tutalimaliza
karibuni

SIKU YA WAZEE WA MKOA
WA DAR:
Suala la Zanzibar hatuwezi
kuliingilia kwasababu tume
huru na haiwezi kuingiliwa na
chombo chochote...
Umalizwaji wa suala la Zanzibar ni kwa kurudia uchaguzi na wala si kwa rais kuvunja katiba na kuingilia mamlaka ya tume.
 
Ila anamamlaka ya Kumlinda Jecha Kama Vile amekuwa ni Mfalme Abdullah. To Me Mtu Mnafiki hata Kama Akijito ngozi yake Nivae wakati wa Baridi, Simhitaji. Hata Magufuli Mwnyewe alishasema, Bora Mchawi anayekuloga Unakufa Kuliko Mnafiki. MAGUFULI NI MNAFI IT IS SAD! Magufuli anania mbili zisizoendana, Kama Vile Mtu anayemtupia Kuku Mahindi Ili amkamate na Kumchinja wala haoni aibu mahindi yake Bado yako shingoni. Kama Magufuli Unamjali Mtanzania,

Jali Uhuru wake, Maamuzi Yake
Amani Yake
Afya Yake
Elimu Yake
Jali Kila Kitu

Hili La Kukataza Habari Hata Nyerere alikatalia Television, Huku yeye akiwa na TV ya Ungo Ikulu na Msasani. Ni Rahisi sana Kumtawala asiyeona Kinaachoendelea.
 
Lol!....naona umeuweka unafiki pembeni kabisa na umeamua kumpa za uso wazi wazi na kumwita "MNAFIKI"

Ni kweli ni mnafiki na kila kinachofanyika ni cha kinafiki tu hata tumbua majipu ni unafiki kwa kwenda mbele

Kwa sababu huyu jamaa angekuwa si mnafiki kweli, angeshatumbua jipu kubwa la Tegeta Escrow Account na angeweza kusababisha ktk eneo hilo tu kupata zaidi Tshs bilion mia moja na ushee na wahusika kuanza kunyea madebe Segerea au Ukonga!

Eti kwa unafiki wake, anajivunia kuokoa 7bn kwenye sherehe za uhuru, ukimwi na kuzuia safari. Hivi 320bn (za Escrow scandal) na hii 7bn ni wapi na wapi kama si unafiki tu?
 
WAPINZANI/ WATUMBULIWA MAJIPU MNAHANGAIKA KUMCHAFUA MAGUFULI KILA KUKICHA MNAHANGAIKA SANA

YAANI NAWAFANANISHA NA MWANAMKE ANAYEFIKA MSHINDO WAKE ANAVYOHANGAIKA NDIO SAWA NA NYIE
 
Unafiki wake Mwingine:

SIKU YA KUHUTUBIA BUNGE:
Suala La Zanzibar tutalishughulikia na
tutalimaliza haraka.....

SIKU YA XMAS:
Kama nilivyoahidi bungeni
suala la Zanzibar tutalimaliza
karibuni

SIKU YA WAZEE WA MKOA
WA DAR:
Suala la Zanzibar hatuwezi
kuliingilia kwasababu tume
huru na haiwezi kuingiliwa na
chombo chochote...

Unaweza ukawa sahihi kulingana na kauli zake, lakini vyema ukajiongeza Zaidi, yeye ana maoni yake katika mgogoro wa Zanzibar, lakini pia kuna watangulizi wake kina jk na bwm na vyombo vya akili pamoja na msimamo wa chama chake! Ukizingatia yeye sio mwenyekiti wa chama chake.....!

Hivyo kauli na misimamo ya woote hao, kwnda kwake kwa nyakati tofauti, lazima utakuwa humwelewi!
 
Kwa unafiki wake hata ameshindwa kumkamata Edward Lowassa na kumfikisha kwenye "mahakama ya mafisadi ya kule Chato"

Kwa unafiki wake ameshindwa hata kutumbua jibu la Bunge la Katiba lililokuwa chini ya mzee "Six" na kuchakachua maoni ya wananchi huku wakitumia mabilioni ya shilingi ambazo zingetumika kwenye "Bure Elimu".....
 
Umalizwaji wa suala la Zanzibar ni kwa kurudia uchaguzi na wala si kwa rais kuvunja katiba na kuingilia mamlaka ya tume.

Vipi Kama CCM Ingekuwa Imeshinda halafu Uchaguzi Ukaombwa Urudiwe, CCM Mngesemaje, Najua Jibu hebu sikiliza Mwaka 2000, Tofauti ilidaiwa CCM ndiyo iliyoshinda.

Hata hivyo Magufuli kimsingi si mwanasiasa na yeye hapendi hilo eneo ila hakuna njia. Sisi watanzania tutamsamehe kwa hilo. Tunachohitaji kwake aendelee kuisafisha na hatimaye aikomboe Tanzania.
 
Ila anamamlaka ya Kumlinda Jecha Kama Vile amekuwa ni Mfalme Abdullah. To Me Mtu Mnafiki hata Kama Akijito ngozi yake Nivae wakati wa Baridi, Simhitaji. Hata Magufuli Mwnyewe alishasema, Bora Mchawi anayekuloga Unakufa Kuliko Mnafiki. MAGUFULI NI MNAFI IT IS SAD! Magufuli anania mbili zisizoendana, Kama Vile Mtu anayemtupia Kuku Mahindi Ili amkamate na Kumchinja wala haoni aibu mahindi yake Bado yako shingoni. Kama Magufuli Unamjali Mtanzania,

Jali Uhuru wake, Maamuzi Yake
Amani Yake
Afya Yake
Elimu Yake
Jali Kila Kitu

Hili La Kukataza Habari Hata Nyerere alikatalia Television, Huku yeye akiwa na TV ya Ungo Ikulu na Msasani. Ni Rahisi sana Kumtawala asiyeona Kinaachoendelea.
Siyo Jecha pekee hata wewe ana mamlaka ya kukulinda kama hujaleta fyokofyoko lakini hata ukileta fyokofyoko ukapalekwa gerezani, Rais ana mamlaka pia ya kukulinda ukiwa gerezani.

Kwani kwa sasa mgogoro wa Zanzibar haumalizwi? Au unadhani ataumaliza kwa kutumia fikra zako?

By the way, unafahamu muundo wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar?

Unafahamu ni kina nani waliopendekeza huo muundo wa Tume ya Uchaguzi (ZEC)?

Fanya kwanza utafiti kabla hujaleta hoja ambazo hazina misingi ya hoja
 
Lol!....naona umeuweka unafiki pembeni kabisa na umeamua kumpa za uso wazi wazi na kumwita "MNAFIKI"

Ni kweli ni mnafiki na kila kinachofanyika ni cha kinafiki tu hata tumbua majipu ni unafiki kwa kwenda mbele

Kwa sababu huyu jamaa angekuwa si mnafiki kweli, angeshatumbua jipu kubwa la Tegeta Escrow Account na angeweza kusababisha ktk eneo hilo tu kupata zaidi Tshs bilion mia moja na ushee na wahusika kuanza kunyea madebe Segerea au Ukonga!

Eti kwa unafiki wake, anajivunia kuokoa 7bn kwenye sherehe za uhuru, ukimwi na kuzuia safari. Hivi 320bn (za Escrow scandal) na hii 7bn ni wapi na wapi kama si unafiki tu?
Mkuu naona tayali lakini nashauri ununue ndimu tu halafu usichelewe kuchukua kipima na vipimo vingine.
 
Vipi Kama CCM Ingekuwa Imeshinda halafu Uchaguzi Ukaombwa Urudiwe, CCM Mngesemaje, Najua Jibu hebu sikiliza Mwaka 2000, Tofauti ilidaiwa CCM ndiyo iliyoshinda.

Mkuu jifunze kutofautisha kati ya vyama na katiba ya nchi. Mie nazungumzia katiba ya nchi na si mambo ya vyama hapa. NEC na ZEC zimewekwa na katiba ya nchi na si vyama.
 
Ni danganya toto ya hali ya juu kuona bilioni 4 kwa mwaka kugharamia matangazo ya Bunge ni gharama wakati uko kimya kabisa kuhusu malipo ya bilioni 70(kwa mujibu wa Nipashe) kuliipia sitting allowance za wabunge.

Mbunge mh.Elibariki Kingu anaweza kuwa mzalendo kuliko hata Magu na mwaziri wake wenye jukumu la kusimamia matumizi ya serikali.
 
Hata hivyo Magufuli kimsingi si mwanasiasa na yeye hapendi hilo eneo ila hakuna njia. Sisi watanzania tutamsamehe kwa hilo. Tunachohitaji kwake aendelee kuisafisha na hatimaye aikomboe Tanzania.
Ben Mkapa Alisema anayezungumziia ukombozi mpumbavu
 
Hakuna wanafiki kama chadema.
Mtu walietuaminisha kuwa ni fisadi kwa miaka nane,ndani ya mwezi tu kawa mgombea wao wa urais!
 
Back
Top Bottom