Magufuli ni mnafiki kama Kikwete

Magufuli ni mnafiki kama Kikwete

Nishasema sana jpm ni mnafiki sans inapofika issue za wanasiasa na chama na huo utumbuaji ni usanii tuuu
 
Umalizwaji wa suala la Zanzibar ni kwa kurudia uchaguzi na wala si kwa rais kuvunja katiba na kuingilia mamlaka ya tume.

Kurudia uchaguzi wote (Rais, wabunge, madiwani..) katika majimbo yote hata Unguja ambapo hakuna "faulo" yoyote iliyoripotiwa?
 
Hakuna wanafiki kama chadema.
Mtu walietuaminisha kuwa ni fisadi kwa miaka nane,ndani ya mwezi tu kawa mgombea wao wa urais!
Unafiki wa CHADEMA ni baada ya kujua watanzania hata ukihubiri ufisadi kwao si issue na ushahidi ni kura alizopata Lowassa na kurudi Bungeni kwa Chenge,Ngeleja na Tibaijuka na sasa Chenge ndio mwenyekiti mmojawapo wa Bunge.

Pia usisahau ni wana-CCM ndio walioimba tuna imani na Lowassa mbele ya Jk na mpaka leo hii hao walioimba huwa wimbo ni viongozi wa ngazi mbalimbali ndani ya CCM.
 
Siyo Jecha pekee hata wewe ana mamlaka ya kukulinda kama hujaleta fyokofyoko lakini hata ukileta fyokofyoko ukapalekwa gerezani, Rais ana mamlaka pia ya kukulinda ukiwa gerezani.

Kwani kwa sasa mgogoro wa Zanzibar haumalizwi? Au unadhani ataumaliza kwa kutumia fikra zako?

By the way, unafahamu muundo wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar?

Unafahamu ni kina nani waliopendekeza huo muundo wa Tume ya Uchaguzi (ZEC)?

Fanya kwanza utafiti kabla hujaleta hoja ambazo hazina misingi ya hoja

Magufuli hana Uwezo wa Kunipeleka Gerezani Kwa Mambo ya Kijinga. Magufuli Ni Mnafiki Ndicho Nilichosema, Yeye anajua, Wenye akili wanajua, sasa Kama wewe hutaki Ukweli Hiyo ni Shida yako am Busy Sibishani na Kisiki, Upo!
 
Mkuu jifunze kutofautisha kati ya vyama na katiba ya nchi. Mie nazungumzia katiba ya nchi na si mambo ya vyama hapa. NEC na ZEC zimewekwa na katiba ya nchi na si vyama.

Usipende Kujibujibu Kubishana Mambo yalio wazi Magufuli Ni Mnafiki, CCM Ni wanafiki, anajua na wanajua. Don't waste your time. What I said its settled! Naujua Ukweli Ushahidi ni mwingi umepewa baadhi unabishana nini.
 
Sijakueleqa
Kabla ya Kuzungumza dhumuni Kubwa La Post Hii Napenda Niweke wazi Kuwa, Kwa Miaka Mingi, Kuwashinda hata wengi wa wanaCCM, Nilitambua Uwezo Mkubwa wa Magufuli wa Kufanya Kazi. Nilikuwa na Shukurani Kubwa sana Kwa Magufuli kwa Upendo wake kwa Watanzania na Watanzania. Nilimpenda zaidi Kwa Tabia yake ya Kutokumwogopa yeyote.

Bahaati Mbaya sana Magufuli anatabia Moja mbaya, Ni Mnafiki, sio Mkweli Kama anavyosema "Msemakweli ni Mpenzi wa Mungu" Inapofikia Katika Maswala ya Siasa Magufuli sio mkweli wala mwenye haki, inayofanana na Magufuli wa Ujenzi wa Taifa na Huduma za Jamii.

Unafiki wa wazi ni Pale aliposisitiza Kuwa ati Majaji walimwambia Kuwa Hawana haja ya Kuonekana Live, akiwa anaweka dhana Kuwa Majaji wanamuunga Mkono kwa Kuingilia Utendaji wa Bunge. Swala la Kukatisha matangazo ya TBC ilikuwa ni kwa Lengo la Kuubana Upinzani Bungeni na Kuruhusu Uonevu. Kusema Vinginevyo Ni Unafiki,

Swala Lingine Lilikuwa Ni swala la Zanzibar, Magufuli anajua wazi, Kikwete na Mkapa, walishinikiza Jecha Kufuta matokeo kwa Maslahi ya CCM, Magufuli anajua kuwa NEC, na ZEC sio Tume Huru. Magufuli anajua Uhuni Uliotendeka Zanzibar, Kwa yeye Kujifanya Jecha alifanya maamuzi yake Kikatiba Ni Unafiki.

Watu wanasahau Kuwa Sio Madictator wote Ni wa Aina ya Mobutu, Wengine walikuwa Madictator wa Kuchaguliwa na Watu waoliwaabudu, Madictator hao walikuwa Tayari kutoa damu yao Kuwapa watu wao Wainywe kama wana Kiu. Lakini kwenye Ukubwa wangemtoa yeyote Roho. Mfano halisi alikuwa ni Adolf Hitler. I hope Magufuli Ataacha Unafiki When it comes to Politic.

Mnamjua Mpanju yule Jamaa wa Bunge la Katiba, sasa Hivi kapewa Ukubwa Kwenye Wizara ya Sheria na Katiba.
Mnamkumbuka Makonda na siasa zake za maji taka, Naye Pia alikuwa Kwenye Bunge la Katiba, Magufuli sasa anampa Chapuo
Naaamini hata Bi Asha Bakari asingefariki, angepewa Madaraka Makubwa Kwa Kumtukana Jusa Bungeni! Huyo Ndiye Magufuli Mwanasiasa!

Sikiliza Maneno Yake Katika Sherehe za CCM, Msikilize Mpka Mwisho, Kuna Mahali aliropoka Ukweli, Kuonyesha Zanzibar ilikuwa Ni "Kukataa Kutawaliwa"

[/QUOTE
Sijakuelewa una maanisha nn hivi tofauti za kimamlaka kati ya taasisi moja na nyingine huzijui
 
Kurudia uchaguzi wote (Rais, wabunge, madiwani..) katika majimbo yote hata Unguja ambapo hakuna "faulo" yoyote iliyoripotiwa?
Bosi ipo hivi, maumuzi ya tume hayaingiliwi na mtu yoyote. Rais hana mamlaka hayo. Hivyo hata tume wakifanya maamuzi ya kipuuzi rais hawezi kuingilia. Ndivyo katiba invyosema.
 
Iv kati ya magufuli na chadema nan mnafik? Kama walimkandia lowasa kuwa fisadi kisha wakamsimamisha kugombea uraic, achen siasa zenu za maji taka
 
Unafiki wake Mwingine:


SIKU YA KUHUTUBIA BUNGE:
Suala La Zanzibar tutalishughulikia na
tutalimaliza haraka.....


SIKU YA XMAS:
Kama nilivyoahidi bungeni
suala la Zanzibar tutalimaliza
karibuni


SIKU YA WAZEE WA MKOA
WA DAR:
Suala la Zanzibar hatuwezi
kuliingilia kwasababu tume
huru na haiwezi kuingiliwa na
chombo chochote...

TL.Marandu huna hoja labda umekaa ukaamua kupoteza muda eti unajifanya Administrative analysist go back to school
 
Majipu yenu hata yaamie mikononi atayatumbua tuuuuuuu...Mh. Magufuli ni raisi hata mfanyaje kashasema kashasema...inabidi hasira mkatolee katika kujisafisha na kuumia kwenu hakuna kuiba tena muende mkalime sio kukaa kulalamika au kamvuteni shati Jecha atoke kwani hamumuelewi?
 
Magufuli hana Uwezo wa Kunipeleka Gerezani Kwa Mambo ya Kijinga. Magufuli Ni Mnafiki Ndicho Nilichosema, Yeye anajua, Wenye akili wanajua, sasa Kama wewe hutaki Ukweli Hiyo ni Shida yako am Busy Sibishani na Kisiki, Upo!
Nani amekuambia ninabishana na wewe?

Nani amekuambia Rais Magufuli atakupeleka gerezani. Watakaokupeleka gerezani baada ya kuleta fyoko fyoko ni Maaskari Magereza.
 
Anasema wateule wote walioteuliwa na rais lazima wawe CCM hivyo Jaji mkuu, mwenyekiti wa NEC wote ccm shame
 
Ila anamamlaka ya Kumlinda Jecha Kama Vile amekuwa ni Mfalme Abdullah. To Me Mtu Mnafiki hata Kama Akijito ngozi yake Nivae wakati wa Baridi, Simhitaji. Hata Magufuli Mwnyewe alishasema, Bora Mchawi anayekuloga Unakufa Kuliko Mnafiki. MAGUFULI NI MNAFI IT IS SAD! Magufuli anania mbili zisizoendana, Kama Vile Mtu anayemtupia Kuku Mahindi Ili amkamate na Kumchinja wala haoni aibu mahindi yake Bado yako shingoni. Kama Magufuli Unamjali Mtanzania,

Jali Uhuru wake, Maamuzi Yake
Amani Yake
Afya Yake
Elimu Yake
Jali Kila Kitu

Hili La Kukataza Habari Hata Nyerere alikatalia Television, Huku yeye akiwa na TV ya Ungo Ikulu na Msasani. Ni Rahisi sana Kumtawala asiyeona Kinaachoendelea.
Asante sana!
 
Mtazungumza maneno mengi na vijembe vingi lakini ukweli ni kwamba Rais hana mamlaka kisheria kuingilia maamuzi ya tume ya Uchaguzi, iwe NEC au ZEC. Tume hizi zina mamlaka huru yasiyohojiwa na rais yeyote. Iwe zimefanya maamuzi mabovu au zimefanya maamuzi manzuri rais hawezi kuizingilia kisheria.
Tofautisha kati ya maamuzi ya ZEC na Jecha.
 
TL nakubaliàna na wewe kweli ni mnafiki kama alie muweka Tanzania ulikua inachungwa kwa muda mrefu sasa wamejiingiza wenyewe katika mtego kiburi chà magufuli na ujinga wa kuropokwa ishaiharimu tz hizo trilion anazo sema za hewe hazitoisaidia kitu kama hakuna kutembeza bakuli kwa wakubwa
 
Siasa zetu jinsi zilivyo wakati mwingine lazima usimamie uongo ili mambo yaende,mfano chadema na gia za hewani! Walimtukana lowasa matusi lukuki baadae walipompata wakamgeuza mkombozi.
Kwa nionavyo ccm kuiachia Zanzibar kwa Cuf hii ni sawa na kuvunja muungano. Pia kuikubali katiba ya warioba ni kuimaliza ccm.Japo kwa ukweli ni haki pia Cuf kutawala na katiba ya warioba kupitishwa.
 
Back
Top Bottom