Unaendelea kuonyesha upumbavu wako wa hali ya juu. Uliandika kwamba mimi nilisimama barabarani kuwapigia debe hao mafisadi wawili nimekwambia weka ushahidi unabaki kung'aa macho. Kama huo si uzushi na upumbavu hebu niambie wewe ni kitu gani.
Nchi yetu ni tajiri sana lakini Watanzania hatuoni manufaa yoyote ya utajiri huo kwa zaidi ya miaka 56 ya uhuru sasa.
Hili limesababishwa na viongozi wa roho wa kujilimbikizia mali za nchi kwa njia za haramu. Kuanzia fisadi Mkapa fisadi Kikwete na fisadi na dikteta uchwara Magufuli.
Ufisadi wa EPA, Meremeta, Kigoda, KCM, Rada, ukwapuzi wa nyumba za Serikali, ununuzi wa ndege ya Rais, Richmond/Dowans, IPTL, ununuzi wa ndege, MV UOZO, ESCROW, etc.
Ufisadi huu umewafanya hawa wahuni wajikusanyie mabilioni ya pesa za walipa kodi huku nchi ikikosa maendeleo ya kweli.
Kila kitu chetu ni shakalabaghala hakuna hata kimoja tunachoweza kusema hiki kina ahueni, lakini mpumbavu wewe bado unaendelea kuwaunga mkono hao wahuni na mafisadi na si ajabu kuimba ule wimbo wenu wa kitaahira wataisoma namba kama vile nchi inapokosa maendeleo ya kweli, huduma muhimu zote ni hovyo, elimu hovyo, matibabu hovyo, miundo mbinu hovyo nyinyi wapumbavu hamuathiriki kwa namna yoyote ile!
Muasisi wa CCM Baba wa Taifa wakati ule hali ya CCM haijawa mbaya kama ilivyo sasa alitamka hadharani kwamba "CCM si mama yangu" kutokana na kutoridhika na mwelekeo wa CCM lakini mpumbavu wewe hata Baba wa Taifa hukubaliani naye bado unafuata hao wahuni na mafisadi kama bendera inavyofuata upepo. Hizi ni dalili za upumbavu uliokithiri. Kwa yeyote yule mwenye akili sawa hawezi kuwa support hao ambao wewe unawa support kila kukicha.
Eti Magufuli ni mchapa kazi! Pamoja na kuandikwa mara tatu katika ripoti ya CAG kuhusu kushiriki kwenye wizi wa nyumba za Serikali, kulidanganya Bunge kuhusu upotevu wa billions of shillings za ujenzi, pia ununuzi wa kivuko uozo. Ndani ya mwaka tu ameuathiri kwa kiwango cha juu sana uchumi wa nchi kwa sera za za kukurupuka na kutotaka ushauri. Amelidharau Bunge na katiba ya nchi. Na Watanzania kila kona ya nchi wanalalamika kuhusu maisha kuwa magumu sana ndani ya mwaka tu wa utawala wake. Pesa kupotea mtaani, bei za vyakula kupanda, ukosefu wa ajira pia nyongeza ya mishahara. Wana CCM ambao waliwahi kushika nafasi za juu Serikalini akiwemo Mwinyi, Kinana, Butiku na Warioba kumtuhumu huyu kwa uongozi wake "Nchi inaendeshwa kama gari bovu" "Nchi imepoteza mwelekeo" "Rais anayejiona yeye ni tembo hatufai Watanzania" lakini taahira wewe haya yote hayakustui ukatafakari KULIKONI mpaka hawa waliowahi kushika nafasi za juu nchini ndani ya CCM na Serikali kuyasema haya!? Bado unaendelea kuimba wimbo wako wa kipumbavu "Magufuli ni mchapa kazi" hebu tuambie kazi ipi anaiyoichapa kwa manufaa ya Tanzania na Watanzania!?
Unajua kuhusu Magufuli kuwapa rushwa Wabunge wa MACCM ya milioni 10 kila mmoja ili wapitishe muswaada uchwara wa kuminya uhuru wa habari nchini!? Bila shaka kwako wewe huu pia ni uchapaji kazi wa Magufuli.
Nasubiri kusikia huo uchapa kazi wa Magufuli. Huyo Magufuli anatukana Watanzania kwa kuwaita vilaza, kutaka waishi kama mashetani lakini sijawahi kukuona ukiandika humu kulalamika kuhusu matusi yake. Na kama unaonyesha akili ya kipumbavu unataka uitwe genius!? Warioba Mwinyi Butiku Kinana wanalalamika kuhusu utendaji wa fisadi na dikteta uchwara iweje
wewe usiyaone na kuyafahamu wayasemayo na hivyo kuendelea kuimba Magufuli ni mchapa kazi?
Tia akili kichwani achana na uzuzu wa bendera hufuata upepo wa kuendelea kuunga mkono utendaji mbovu uliokithiri kila kona na kila sekta nchini.
Mpumbavu!!...
Kwa sababu tu natofautiana na wewe nimekuwa mpumbavu...Lol..
Sijajiunga JF leo, nina zaidi ya miaka 10 humu (na unalijua hilo) yet unasema sina uwezo wa kuandika...
Waungwana hutumia lugha za staha wanapotufautiana kwa hoja..Na si matusi ama dhihaka, kuniita mimi mpumbavu ama Liar hakuondoi ukweli wa nilichoandika.Na haiondoi ukweli kwamba Lowassa na Sumaye walikuwa ni Wabunge waandamizi wa CCM na Mawaziri wakuu wastaafu ambao walishiriki katika kila maamuzi ya serikali tangu enzi za Mwinyi mpaka Mkapa na Kikwete..
Hiyo rekodi mbovu ya utendaji unaiona wewe, lakini watanzania wengi wanajua Magufuli ni mchapa kazi tangu akiwa Waziri wa Ujenzi, Mifugo na Uvuvi, Adhi na baadae tena Ujenzi..Rekodi zinaonekana na wala hazijifichi..Ila siwezi kupingana na mtazamo/maoni yako..Nauheshimu.
Mwisho, tujadiliane kwa hoja Chifu, sio kwa matusi, dhihaka wala maneno ya kuudhi..Tuheshimane pale tunapotofautiana hoja/mutazamo..Kuniita mpumbavu kisa tu natofautiana nawe sidhani kama ni busara..Ingawa nami nina uwezo wa kukuita vyovyote nitakavyo lakini busara na dhamira vinanizuia kufanya hivyo..
Mwisho kabisa; Hongera sana kwa ushindi wa jana wa FA cup (tunatofautiana kimitazamo lakini Arsenal inatuunganisha...Cheers)
Jumapili njema mkuu.
Bala.