Magufuli "Nchale!" - Usiteme, Usimeze wala Usimumunye!

Magufuli "Nchale!" - Usiteme, Usimeze wala Usimumunye!

Kuna jambo linanitatiza sana, nadhani ni tatizo binafsi.

Watu wanasema hatua zilizochukuliwa ni nzuri, tusiogope kushtakiwa n.k.
Sababu wanazotoa ni kuibiwa

Ninauliza, hivi tunatakiwa tuunge mkono tu hatua zozote bila kujiuliza!
Mikataba inayoonyesha tumeibiwa nani amefanikiwa kuiona?

Kama mikataba ipo, yaani miaka 16+ hakuna aliyeisoma na kuona tatizo licha ya kelele zinapigwa!

Walioingia mikataba wapo wapi ku 'rally' umma kwa kuibiwa wakitufahamisha mikataba ilisemaje?

Namuomba mwenyezi anijalie niwe mwepesi wa kubebwa na mikumbo kama wenzangu! amin
 
Funga migodi yote acacia warudi kwao huu wizi wa mchana kweupe wa makaratasi yalitengenezwa na Change na genge lake hauvumiliki.

Sekta ya madini hainufaishi ktk Taifa la Tanzania zaidi ya matumbo ya viongozi wa wachache kwahiyo Hata tukisitisha uzalishaji wa madini na kutumia wawekezaji wa migodi yote ni sawa.madini hayaozi.
Madini hayaozi yanini yanini miswada kujadiliwa kwa hati za dharura?
 
Una akili fupi ndiyo sababu unashangaa. Kwenye nchi za utawala wa sheria madudu aliyoshiriki huyu kuanzia ukwapuzi wa nyumba za Serikali, ununuzi wa MV Uozo, kulidanganya bunge kuhusu upotevu wa billions pale ujenzi etc vyote hivi vilistahili kumpandisha huyu kizimbani na hatimaye kupatikana na hatia na hivyo kwenda kifungoni. Kwenye nchi zenye utawala wa sheria huyu asingestahili kuwa Rais lakini huu wehu uliokithiri nchini wa hawa wahuni na mafisadi kulindana ndiyo umetufikisha hapa tulipo na hivyo kuendelea kuligharimu Taifa.

Kwa wenye akili finyu kama wewe bado mnataka kumpigia makofi huyu pamoja na rekodi yake kuonyesha maamuzi yake mbali mbali kuligharimu Taifa mabilioni ya shilingi.

Watu mnashangaza sana..

Kwa sababu tu Magufuli ni Rais leo ndo mnasema ajiuzulu kwa sababu alishiriki mikataba!!!...Alishiriki mikataba kwa sababu tu alikuwa Mbunge/Waziri...

Mbona Fredrick Sumaye (aliyekuwa Mbunge na Waziri Mkuu kuanzia 1995 hadi 2005) na Edward Lowassa (Waliyekuwa Mbunge, Waziri na Waziri Mkuu) hamuwagusi kwenye hili sakata, au kwa sababu wako CHADEMA?..

Kwa hiyo mlitaka Rais Magufuli akae kimya na kulifumbia mdomo suala hili kwa sababu tu alikuwa Mbunge na alishawahi kuwa Waziri kwenye serikali ambayo hakuwa na sauti/mamlaka nayo?...Nilitegemea tutamuunga mkono Mhe. Rais katika hili lakini badala yake watu mnalichukulia kisiasa..Eti awajibike kwa sababu alikuwa Mbunge na Waziri...
 
"Balantanda, post: 21339127, member: 11305"]Mbona Fredrick Sumaye (aliyekuwa Mbunge na Waziri Mkuu kuanzia 1995 hadi 2005) na Edward Lowassa (Waliyekuwa Mbunge, Waziri na Waziri Mkuu) hamuwagusi kwenye hili sakata, au kwa sababu wako CHADEMA?..
point! na hii ndiyo hoja yangu mabandiko mengi. Kwamba, kwanini waliotufikisha hapa hawasemwi? Hakuna cha vyama, iwe wanasheria, wanasiasa wanatakiwa waanikwe wakati tunatibu maradhi ya uzembe na ujinga

Utaona hakuna kutajana kwasababu ni 'syndicate' nani amfunge paka kengele.
Inasemwa Yesu aliwaambia 'anayedhani kuwa ni msafi miongoni mwenu aanze kutupa jiwe''
Kwa hiyo mlitaka Rais Magufuli akae kimya na kulifumbia mdomo suala hili kwa sababu tu alikuwa Mbunge na alishawahi kuwa Waziri kwenye serikali ambayo hakuwa na sauti/mamlaka
Wabunge wa upinzani walikuwa na sauti na mamlaka kutoka wapi?
Nilitegemea tutamuunga mkono Mhe. Rais katika hili lakini badala yake watu mnalichukulia kisiasa..Eti awajibike kwa sababu alikuwa Mbunge na Waziri...
Huwezi kulitenga hili jambo na siasa. Walio na madaraka ni wanasiasa. Waliotenda waliteuliwa na wanasiasa. Maamuzi yalikamilika kupitia mikono ya wanasiasa. Hata Katibu mwenezi ambaye ni mwanasiasa ameomba radhi kwa niaba ya CCM iliyopo madarakani miaka yote kwa njia za siasa na kutenda siasa.

Balantanda wananchi wameunga mkono maazimio mengi sana ya nchi hii. Kila baada ya miaka 10 wakiangalia nyuma wanagundua ilikuwa miradi ya watu na si yao

Lazima kuwa na 'ground' za kuunga mkono. Miaka 50 ya uhuru ni Taifa 'matured' linalohitaji kufikiri na si kuimba TANU yajenga nchi.

Huu si muda wa kuhamasishana ni muda wa mkakati na kuelezana ukweli.

Miaka 10 iliyopita tuliongelea mchanga na Karamagi. Leo unataka watu wajimwae mwae uwanjani, wababa na bakro zao na manyanga, akina mama na vibebwe wakisherehekea kutimiza miaka 10 ya mchanga! real
 
Una akili fupi ndiyo sababu unashangaa. Kwenye nchi za utawala wa sheria madudu aliyoshiriki huyu kuanzia ukwapuzi wa nyumba za Serikali, ununuzi wa MV Uozo, kulidanganya bunge kuhusu upotevu wa billions pale ujenzi etc vyote hivi vilistahili kumpandisha huyu kizimbani na hatimaye kupatikana na hatia na hivyo kwenda kifungoni. Kwenye nchi zenye utawala wa sheria huyu asingestahili kuwa Rais lakini huu wehu uliokithiri nchini wa hawa wahuni na mafisadi kulindana ndiyo umetufikisha hapa tulipo na hivyo kuendelea kuligharimu Taifa.

Kwa wenye akili finyu kama wewe bado mnataka kumpigia makofi huyu pamoja na rekodi yake kuonyesha maamuzi yake mbali mbali kuligharimu Taifa mabilioni ya shilingi.
Ufupi na urefu ni nadharia tu...Vyote ni vipimo...Mwenye akili fupi na mwenye akili ndefu wote huwa na uwezo wa kutoa mawazo, japo hutofautiana..

Bado unaelea kulekule pamoja na akili zako ndefu...

Kati ya hayo uliyoyataja hapo juu ni wapi huyo Rais wenu Lowassa hakushiriki?, ni wapi Sumaye hakushiriki?..

Hivi unategemea kitu kinachopitishwa na Baraza la Mawaziri au Bunge, Mbunge ama Waziri ana uwezo wa kupinga msimamo wa Rais wake ama Waziri Mkuu?, unaelewa kwamba Rais Kikwete amewahi kumzuia Magufuli kutekeleza zoezi la bomoaboma mbele ya hadhara?...Kwa akili yako ndefu unategeme Magufuli alikuwa anatekelez yote hayo uliyoyataja hapo juu kwa utashi wake mwenyewe pasipo maelekezo/ufahamu wa Mamlaka zake za juu (ma Rais na Mawaziri wakuu wake)?..

Sasa wewe unayewahail Lowassa na Sumaye leo na mimi nani anaonekana ana akili finyu?...Wewe tangu 2006 enzi za Jambo Forum na baadae Jamii Forum umekuwa ukiwatuhumu Lowassa na Sumaye Mafisadi na kuwatupia kila aina ya laana, leo unakaa barabarani kuwadekia barabara na kumnadi Urais...Pathetic
 
Ajiuzulu kwa sababu yeye pia alishiriki katika mikataba mbali mbali ambayo imeliingiza Taifa hasara kubwa sana.
Alafu tumuweke Lowasa, sababu Lowasa ni Chadema, na hajawai kuwa CCM, pia ni mzalendo alietukuka, Lowasa ni malaika
 
Ila siku hizi huyu Mzee Mwanakjiji amekuwa boys Sana.
Huyu jamaa alikuwa anasema nchi haiwezi kwenda mbele bila kufuata utawala wa sheria.

Leo mjomba yake kawa rais kasahau utawala wa sheria, anaona udikteta na uongo ni sawa tu.

Shida sana
 
Hakika wafuasi wa Magufuli ( siyo wafuasi wa utawala wa sheria ) mko wengi sana !
kamwe sisi wakurya hatuwezi kuishi kwa amani kwenye nchi ya wanaume wanaoishi uvunguni, (waoga) wanao jiandaa kushindwa hata kabla ya vita,vigeugeu,wanafki na wasoma nyota. Nilipozunguka uwani niligundua si kweli kuwa mnawatetea Acacia lahasha vitisho vyenu ni kuwanusuru wale jamaa zetu waliohusika, ambao kamanda mkuu amesema washughurikiwe.
 
point! na hii ndiyo hoja yangu mabandiko mengi. Kwamba, kwanini waliotufikisha hapa hawasemwi? Hakuna cha vyama, iwe wanasheria, wanasiasa wanatakiwa waanikwe wakati tunatibu maradhi ya uzembe na ujinga

Utaona hakuna kutajana kwasababu ni 'syndicate' nani amfunge paka kengele.
Inasemwa Yesu aliwaambia 'anayedhani kuwa ni msafi miongoni mwenu aanze kutupa jiwe''
Wabunge wa upinzani walikuwa na sauti na mamlaka kutoka wapi?
Huwezi kulitenga hili jambo na siasa. Walio na madaraka ni wanasiasa. Waliotenda waliteuliwa na wanasiasa. Maamuzi yalikamilika kupitia mikono ya wanasiasa. Hata Katibu mwenezi ambaye ni mwanasiasa ameomba radhi kwa niaba ya CCM iliyopo madarakani miaka yote kwa njia za siasa na kutenda siasa.

Balantanda wananchi wameunga mkono maazimio mengi sana ya nchi hii. Kila baada ya miaka 10 wakiangalia nyuma wanagundua ilikuwa miradi ya watu na si yao

Lazima kuwa na 'ground' za kuunga mkono. Miaka 50 ya uhuru ni Taifa 'matured' linalohitaji kufikiri na si kuimba TANU yajenga nchi.

Huu si muda wa kuhamasishana ni muda wa mkakati na kuelezana ukweli.

Miaka 10 iliyopita tuliongelea mchanga na Karamagi. Leo unataka watu wajimwae mwae uwanjani, wababa na bakro zao na manyanga, akina mama na vibebwe wakisherehekea kutimiza miaka 10 ya mchanga! real
Hakuna sehemu nimelitenga hili suala na wanasiasa...Wanasiasa hawakwepeki katika hili...

Hoja yangu ni moja tu..Kwamba tumuunge mkono Rais kwa hatua aliyoichukua badala ya kuanza kudhihaki na kukosoa kwamba alishiriki kuingia hiyo mikataba akiwa Mbunge/Waziri (angekuwa amewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini sawa)..

Kwa desturi ya siasa zetu za kiafrika na mfumo wa uendeshaji wa vyama vyetu ni ngumu sana kuona mtu anapingana na chama/msimamo wa chama..Ndio maana hauwezi kukuta wabunge wa CCM au upinzani wanaenda tofauti na caucas za vyama vyao..

Maamuzi mengi hufanywa na Baraza la Mawaziri, usitegemee Rais Magufuli (akiw Waziri) angepingana na maamuzi ya Baraza la Mawaziri au angesimama kupingana na hiyo mikataba ya Madini (ambayo sidhani kama inasainiwa bungeni)...Na kwa vile vikao na maamuzi ya Baraza la Mawaziri ni siri hatujui nini na nani aliongea nini kwenye hivyo vikao...

Yes, ni muda wa kuelezana ukweli..Lakini vipi kuhusu kuunga mkono hatua zilizochukuliwa na Rais JPM..Watu walitaka asichukue hatua kwa sababu tu 'alikuwa' sehemu ya waliofanya maamuzi/kuingia mikataba au kwa sababu ni mwana CCM...Kwa mtazamo wangu hili sio sahihi..Tunatakiwa kumuunga mkono kwanza...Hayo ya nani wametuingiza hapo yanajulikana...

Sorry for the typos...
 
Tuache kuangalia issues kwa jicho la kisiasa kila wakati. Watanzania someni hotuba ya Prof Mruma na Mh Rais ili msipotoshwe....narudia someni zile hotuba kwa umakini sana ....waliofukuzwa sababu zimetolewa ...anayepinga uhalali wa sababu zile aende kwenye hotuba zile anukuu na kuzileta hapa na kuzipangua hoja kwa hoja ....wanaotaka kutumia takwimu kupinga ripoti ni vizuri wakatenda haki ....wachukue kila findings za tume na kuzipinga kwa hoja .....tuache kufanya siasa kwenye mambo ya msingi ....kwenye hili Watanzania watawapigia msumari wa mwisho wa unafiki wa wanasiasa wetu ....Bora Zitto aliyekiri TAFITI hupingwa kwa TAFITI ....Issues za mikataba imegusiwa kwenye ripoti ya tume lakini watu wanakomaa na spinning kupotosha umma ....shame on you ...
 
Siasa sasa hivi imekuwa kama Muziki Chifu...Kick
 
Ajiuzulu kwa sababu yeye pia alishiriki katika mikataba mbali mbali ambayo imeliingiza Taifa hasara kubwa sana.
Huu ushauri ungeanza kumpa Lowasa, Sumaye na wenzao.
 
Na ukichukua hatua hizi na wawekezaji wakubwa wakigoma au wakitushtaki na tukashindwa?

Sidhani kama kuna mnunuzi anayeweza kumshtaki muuzaji kwa kukataa kuuza.
You do not have any power in any negotiation if you are not prepared to walk away.

Hiyo mikataba tuliyosaini tayari tulifanya makosa, cha kufanya ni kuiweka wazi kwanza bungeni, ili serikali ipate support ya wawakilishi wa wananchi kwa kuchukua maamuzi ya kutoka kwenye negotiation na wawekezaji wapya.

Itasaidia wananchi kujua ni vipengele vipi ni suicide, ili siku tukifikuta kwenye mkataba mwengine tupaze sauti.

Mwisho kabisa itautangazia wawekezaji wote ulimwenguni kuwa we mean business. Njoo tanzania kama uko tayati kuwa transparent and fair. You will be supprsed wawekezaji wangapi wanasubiri hiyo nafasi.

Tunakimbiza wawekezaji wazuri tunabaki na crooks kwa sababu hatuko tayari kuwa transparent.
 
Ndiyo akili fupi niliyosema hiyo ya kuandika uzushi ambao hakuna ushahidi wa kuthibitisha ulichoandika. Hebu niwekee ushahidi wa mimi kupigia debe upigaji wa deki kwa ajili ya Lowassa na Sumaye au hata kuwaunga mkono.

Wapumbavu kama wewe ndiyo tatizo kubwa nchi hii. Mtu ana rekodi mbovu kwenye utendaji miaka nenda miaka rudi lakini bado anafikia kuja kuwa Rais wa nchi! Only in Tanzania! Nchi nyingine huyu angekuwa lupango.

Kama huna uwezo wa kuandika ukweli cheza mbali na jukwaa hili badala ya kuandika uongo wa kupindukia eti mimi nimesimama barabarani kuwapigia deki hao mafisadi wawili.

SHAME ON YOU LIAR!

Ufupi na urefu ni nadharia tu...Vyote ni vipimo...Mwenye akili fupi na mwenye akili ndefu wote huwa na uwezo wa kutoa mawazo, japo hutofautiana..

Bado unaelea kulekule pamoja na akili zako ndefu...

Kati ya hayo uliyoyataja hapo juu ni wapi huyo Rais wenu Lowassa hakushiriki?, ni wapi Sumaye hakushiriki?..

Hivi unategemea kitu kinachopitishwa na Baraza la Mawaziri au Bunge, Mbunge ama Waziri ana uwezo wa kupinga msimamo wa Rais wake ama Waziri Mkuu?, unaelewa kwamba Rais Kikwete amewahi kumzuia Magufuli kutekeleza zoezi la bomoaboma mbele ya hadhara?...Kwa akili yako ndefu unategeme Magufuli alikuwa anatekelez yote hayo uliyoyataja hapo juu kwa utashi wake mwenyewe pasipo maelekezo/ufahamu wa Mamlaka zake za juu (ma Rais na Mawaziri wakuu wake)?..

Sasa wewe unayewahail Lowassa na Sumaye leo na mimi nani anaonekana ana akili finyu?...Wewe tangu 2006 enzi za Jambo Forum na baadae Jamii Forum umekuwa ukiwatuhumu Lowassa na Sumaye Mafisadi na kuwatupia kila aina ya laana, leo unakaa barabarani kuwadekia barabara na kumnadi Urais...Pathetic
 
Na hili litakuridhisha? akivunja mkataba kwa njia za kisheria (una maana aende mahakamani na kujaribu kujitoa) akishindwa alipe na gharama za kesi au atalaumiwa kwa kushindwa kesi nyingine?
Hiyo ndio njia pekee ya halali ya kuondoa utata , haitawezekana mtu mmoja kuvunja sheria zote , za Tanzania ambazo tayari kazisigina na za kimataifa kwa kisingizio chochote kile , utawala wa sheria uko hivyo , na wewe hili unalijua bali unasukumwa na ukabila na wala si uzalendo.
 
Ndiyo akili fupi niliyosema hiyo ya kuandika uzushi ambao hakuna ushahidi wa kuthibitisha ulichoandika. Hebu niwekee ushahidi wa mimi kupigia debe upigaji wa deki kwa ajili ya Lowassa na Sumaye au hata kuwaunga mkono.

Wapumbavu kama wewe ndiyo tatizo kubwa nchi hii. Mtu ana rekodi mbovu kwenye utendaji miaka nenda miaka rudi lakini bado anafikia kuja kuwa Rais wa nchi! Only in Tanzania! Nchi nyingine huyu angekuwa lupango.

Kama huna uwezo wa kuandika ukweli cheza mbali na jukwaa hili badala ya kuandika uongo wa kupindukia eti mimi nimesimama barabarani kuwapigia deki hao mafisadi wawili.

SHAME ON YOU LIAR!
Mpumbavu!!...

Kwa sababu tu natofautiana na wewe nimekuwa mpumbavu...Lol..

Sijajiunga JF leo, nina zaidi ya miaka 10 humu (na unalijua hilo) yet unasema sina uwezo wa kuandika...

Waungwana hutumia lugha za staha wanapotufautiana kwa hoja..Na si matusi ama dhihaka, kuniita mimi mpumbavu ama Liar hakuondoi ukweli wa nilichoandika.Na haiondoi ukweli kwamba Lowassa na Sumaye walikuwa ni Wabunge waandamizi wa CCM na Mawaziri wakuu wastaafu ambao walishiriki katika kila maamuzi ya serikali tangu enzi za Mwinyi mpaka Mkapa na Kikwete..

Hiyo rekodi mbovu ya utendaji unaiona wewe, lakini watanzania wengi wanajua Magufuli ni mchapa kazi tangu akiwa Waziri wa Ujenzi, Mifugo na Uvuvi, Adhi na baadae tena Ujenzi..Rekodi zinaonekana na wala hazijifichi..Ila siwezi kupingana na mtazamo/maoni yako..Nauheshimu.

Mwisho, tujadiliane kwa hoja Chifu, sio kwa matusi, dhihaka wala maneno ya kuudhi..Tuheshimane pale tunapotofautiana hoja/mutazamo..Kuniita mpumbavu kisa tu natofautiana nawe sidhani kama ni busara..Ingawa nami nina uwezo wa kukuita vyovyote nitakavyo lakini busara na dhamira vinanizuia kufanya hivyo..

Mwisho kabisa; Hongera sana kwa ushindi wa jana wa FA cup (tunatofautiana kimitazamo lakini Arsenal inatuunganisha...Cheers)

Jumapili njema mkuu.

Bala.
 
Back
Top Bottom