Magufuli na Trump wanavyofanana

Magufuli na Trump wanavyofanana

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Posts
49,320
Reaction score
117,613
1. Wote hupenda kutupia lawama Kwa waliowatangulia Ikulu.
Kikwete na Obama.

2. Wote walijitapa kujiandaa na janga la Corona..vizuri na matokeo ni kinyume..

3. Wote waliudharau ugonjwa Kwa kuuita ni mafua tu..

4. Wote hawapendi lockdown..Trump hadi anabishana na Magavana wake

5. Wote wanatifautiana na watu wa chini yao jinsi ya kupambana na Corona..

6. Wote wanajali uchumi zaidi kuliko lockdown .

7. Wote Wana face uchaguzi mwaka huu na wote wanahofia hili la Corona kugeuka agenda kwenye uchaguzi..

8....

9...

Kwenye hili la Corona naona Magufuli na Trump Baba mmoja mama mmoja, tofauti ni ukubwa tu wa nchi zao na aina ya freedom of speech kwa kila nchi.
 
Rais ukishaingia madarakani na kuanza lawama kwa wenzio ufai kuwa rais wa nchi Trump sio mvumilivu ana jaziba kama alivyo Magufuli.

Tofauti ni kuwa Marekani taasisi ni imara mno wanazuia mambo mengi machafu ambayo angefanya Trump tofauti na Tz jamaa kaachwa.

Marekani isingekuwa na ubora wa katiba na taasisi imara Trump angetawala kwa mabavu sana kama anavyofanya Magufuli kuitawala Tanzania Kidicteta.
 
1.Wote hupenda kutupia lawama Kwa waliowatangulia IKulu..
Kikwete na Obama.
Trump siyo kwamba anapenda kutupia lawama marais waliomtangulia, sema anapenda kumtupia lawama Obama.
Na ukiangalia kwa jicho la kawaida unagundua ni aina Fulani ya wivu.
Yaani Trump anaona heshima anayopewa Obama ni kubwa wakati yeyeanajiona kama anapuuzwa.Ndiyo maana anapmbana sana kufuta legacy ya Obama lakini bila bila.
In short kivuli cha Obama bado kinamtesa sana Trump.

2.Wote walijitapa kujiandaa na janga la Corona..vizuri na matokeo ni kinyume..
Corona wakati iko China Trump hakuona ni kwa namna gani utafika Marekani na kwa kuwa ana chuki na China akawa anachekelea tu ( Kumbuka mpaka subordinates wake wakawa wanasema CORONA kwao ni fursa ). Magufuli hana uwezo wa kutatua tatizo lolote, likitokea yeye anakaa pembeni labda liishe kwa kudra za Mwenyezi Mungu tu.


3 .Wote waliudharau ugonjwa Kwa kuuita ni mafua tu..
May be

[qute]4.Wote hawapendi lockdown..Trump hadi anabishana na Magavana wake[/quote]Trump hataki Lockdown kwasababu imeua Leacy yake yote aliyokuwa anatamba nayo ya JOBS na Stock market wakati ana uchaguzi mwaka huu.

Wakati Magufuli anategemea jeshi kurudi Ikulu.
Magufuli kakopa kopa weeee mpaka hanaona watu wakikaa lockdown atakosa pesa ya kulipa madeni.

5.Wote wanatifautiana na watu wa chini yao jinsi ya kupambana na Corona..
May be




[/QUOTE]Anyway!!!

At least Trump anajua uchumi na kujali raia wake wakati Magufuli yeye akishia yeye na Makonda inatosha kabisa
 
Ongeza wote wamejaa ego, wapo tayari kuangusha hata nuclear ili mradi tu wasifanye kitu mtu wa upinzani anataka.
 
Kwahiyo sasa unasemaje? Hamia Uganda huko kuna miujiza watu hawafi....wana mapafu ya popo
 
Bado kajifungia? Unajua watu wa huko wana mambo ya ajabu ajabu pengine anafanya yale mambo yao.
 
OP anazungumzia mlinganisho wa marais wawili: Trump na JPM katika kupambana na Covid-19 na sio mlinganisho wa nchi mbili: USA na TZ.

Ni vizuri kustick kwenye mada husika.
Rais ukishaingia madarakani na kuanza lawama kwa wenzio ufai kuwa rais wa nchi Trump sio mvumilivu ana jaziba kama alivyo Magufuli.

Tofauti ni kuwa Marekani taasisi ni imara mno wanazuia mambo mengi machafu ambayo angefanya Trump tofauti na Tz jamaa kaachwa.

Marekani isingekuwa na ubora wa katiba na taasisi imara Trump angetawala kwa mabavu sana kama anavyofanya Magufuli kuitawala Tanzania Kidicteta.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom