Magufuli na Ndulu, Kikwete na Idrissa...

Mimi siamini kama Ndulu ni Gavana Bora...Chukulia kipindi cha Kikwete kila siku shilingi yetu ilikuwa inaporomoka, mimi natamani yule waliyesema kafia marekani angerudishwa apewe hicho cheo cha Ndulu yule jamaa kwangu ndo gavana bora kupita wote ambao wamesimamia BOT, uchumi kipindi cha Mkapa ulitengemaa kwelikweli, au wizara ya Fedha apewe Basil Pesambili Mramba.

Naomba kusahihisha, hakuna siku toka uhuru uchumi wa Tanzania uliwahi kuwa imara.
 
Sijasema Ndulu ni malaika
ninachosema ni mtaalam wa uchumi wa kumsikiliza kuliko Mpango na kuliko Magufuli

kuhusu wizi BOT usisahau wizi ukiwa umepangwa kitaalam
hakuna gavana wa kuuzuia...hasa kama hadi wizara zimeshiriki
Escrow ilipangwa wizarani hadi kwa mwanasheria mkuu
kumbuka BOT wao waliomba tu barua ya mwanasheria mkuu kama ushahidi ndo wakaruhusu hela zitoke

kuhusu kushuka kwa shilingi....ni mambo tele yanahusika sio tu BOT..
Ndulu naweza kusema amesaidia 'hali isiwe mbaya zaidi'
angalau inflation iko single digit miaka yote yupo hapo
mambo yangeweza kuwa mabaya kuliko hapo....

amepunguza damages za maamuzi mabaya ya wajuu wake
yeye hana mamlaka kamili ya kila kitu

Mkuu while I have huge respect for you kama mchangiaji mkongwe kwenye hili jukwaa...hebu naomba pitia tena hili bandiko usome ulivyonijibu!

My question was very simple and precise.

What have we got to show as a nation from what Prof. Ndullu has done to our country as BoT Governor for the past decade (almost?)

Nimetoa mfano: Aliingia BoT shilling ikiwa 1250 kwa 1USD....anakaribia kumaliza muhula wake.....tuko 2185-1USD.

So for what achievement should we applaud him?
 
Nilifikiri ndo furaha yenu Raisi Magufuli na Serikali yake kushindwa sasa kelele za nini tena kama mna uhakika kwamba anashindwa? Kwa nini mnahangaika kumpa mtu ushauri ambaye lengo na furaha yenu ni kuona anashindwa? Mbona mnakuwa kama Wanawake ambao wana sifa ya kutokujua wanataka nini?
Watu hawampingi Magufuli kwa sababu eti kuanguka kwake ndio furaha yetu anapingwa kwa sababu wanao umia yeye akifanya madudu ni sisi na hicho ndio kinafanya wenye kuona mbali wapinge baadhi ya maamuzi yake
 
Pengo la Dr. Likwelile linaonekana alikuwa ni mtu muhimu Wizara ya Fedha na alishirikiana vizuri na Prof. Ndulu.
 
Mkuu while I have huge respect for you kama mchangiaji mkongwe kwenye hili jukwaa...hebu naomba pitia tena hili bandiko usome ulivyonijibu!

My question was very simple and precise.

What have we got to show as a nation from what Prof. Ndullu has done to our country as BoT Governor for the past decade (almost?)

Nimetoa mfano: Aliingia BoT shilling ikiwa 1250 kwa 1USD....anakaribia kumaliza muhula wake.....tuko 2185-1USD.

So for what achievement should we applaud him?

Nimekujibu na nakujibu tena
thamani ya pesa ya nchi haiamuliwi na maamuzi ya BOT peke yake
yapo maamuzi nje ya BOT yanaweza kupelekea shilingi ikashuka au kupanda
mfano export na import...
uzalishaji.....ugaidi ....matetemeko na kadhalika

kuna factors nyingi sana
hivyo siwezi mbebesha lawama Ndulu kwa hilo
 
Kwa takwimu yako broo nimekupata ila swali langu ni kwamb hizo fixed account wakati Wa kikwete zilikuwepo?na kama ndio au hapn wakati wanapiga kodi yangu rais kikwete alikua hajui?
 
Watu hawampingi Magufuli kwa sababu eti kuanguka kwake ndio furaha yetu anapingwa kwa sababu wanao umia yeye akifanya madudu ni sisi na hicho ndio kinafanya wenye kuona mbali wapinge baadhi ya maamuzi yake


Lakini si ndicho mnachokipigania, sasa kelele za nini? Si muache aanguke ili muinuke?
 
Sifa moja ya 'watalaam wanaoujua na wanajua kwamba wanajua' ni kuwa hawapendi kujipendekeza na hawaogopi kufukuzwa.

Wao hupenda kushauri kwa sauti ndogo tu ukiamua kuwasikiliza haya ukiwadharau hasara ni kwako.

Kikwete alipokuwa Rais alifanya kosa moja lillilogharibu Taifa mabilioni baadae

Kikwete aliamua kuwasikiliza Ngeleja na Adam Malima ambao walikuwa waziri na naibu waziri na kuacha kumsikiliza Mtaalam Idrissa Rashid aliekuwa CEO wa Tanesco.

Idrissa Rashid alipoteuliwa CEO wa Tanesco alikuta nchi ina mgao wa umeme na hali ya shirika hoi na wanasiasa wanaingilia maamuzi ya kitaalam.

Akapiga marufuku wanasiasa kuingilia maamuzi kwa miaka minne ya Uongozi wa Idrissa Tanesco hakuna mwanasiasa aliezungumza kitu na mgao ukaisha na shirika likaanza kusimama Idrisa alikuwa anawajua vizuri kina Ngeleja na Malima

Malima alianza kazi BOT Idrissa akiwa gavana..

Ngeleja alipokuwa Vodacom Idrissa alikuwa kwenye Management, wangemueleza nini? aliamua tu 'kutowasikiliza.

Idrissa alivyoondolewa tu Tanesco kilichofuata ni ziara za Waziri Ngeleja Tanesco na 'mgao wa dharura ukaanza' the rest is history. Zaidi ya bilioni 500 zilikwenda. Kikwete alikosea kuwasikiliza kina Ngeleja na Malima asimsikilize Idrissa.

Magufuli anaelekea kurudia kosa hilo hilo anapaswa kumsikiliza Benno Ndulu mtaalam aliemfundisha uchumi Philipo Mpango na naamini Ndulu akisema leo ataje his best students Mpango sidhani atakuwemo.

But Magufuli anaonekana kumsikiliza zaidi Dk. Mpango ambae hata VAT tu haoeneshi kuijua vizuri hadi Ndulu alipojitokeza 'kutoa ufafanuzi.

Siku Ndulu akiondoka hapo ndo tutajua hasara kiasi gani kama taifa tutaingia.

Time will tell.

Yaani wewe unajua kuwa Dr. Mpango hajui VAT?

Maajabu hayataisha dunia hii.
 
Japo ni nje kidogo ya Mada..

Kuna jamaa mmoja ni raia wa Botswana..professionally ni Mhasibu.Alistuka sana aliposikia siku ile Rais ameenda BOT kwa ziara ya kustukiza...!!

Akaniambia anaendaje kwenye institution kubwa kama BOT kwa kustukiza...??!!
Akasema Central Bank ya Nchi ndio ROHO ya Nchi. Pale ndio ilipo HAZINA ya Taifa.

Ni mahali panapotakiwa papewe heshima na staha yake..

Kuvamia namna ile ni kuishushia hadhi BOT

Akasema lolote analotaka Rais anaweza kupewa majibu hata kwa simu tu ndani ya dakika tu.

Akasema... I doubt if your President has advisors or he has them but he doesn't listen.

Sasa nimeuona ukweli.
 
Jaman barbosa broo tatz in letu ni njia ipi ssa ya kuweza kuweka mambo sawa me najua ipo cku mamb yatakaa saw
 
Japo ni nje kidogo ya Mada..

Kuna jamaa mmoja ni raia wa Botswana..professionally ni Mhasibu.Alistuka sana aliposikia siku ile Rais ameenda BOT kwa ziara ya kustukiza...!!

Akaniambia anaendaje kwenye institution kubwa kama BOT kwa kustukiza...??!!
Akasema Central Bank ya Nchi ndio ROHO ya Nchi. Pale ndio ilipo HAZINA ya Taifa.

Ni mahali panapotakiwa papewe heshima na staha yake..

Kuvamia namna ile ni kuishushia hadhi BOT

Akasema lolote analotaka Rais anaweza kupewa majibu hata kwa simu tu ndani ya dakika tu.

Akasema... I doubt if your President has advisors or he has them but he doesn't listen.

Sasa nimeuona ukweli.


Au washauri anawashauri yeye....
 
Sina mashaka na elimu ya Prof. Ndulu (I respect his school-NU-Evanston Chicago- where he wrote his PhD).

Lakini hebu Mkuu tufafanulie tangu Huyu bwana ashike usukani pale BoT (2008?) what have we achieved as a nation in monetary perspective?? Maana in my memory colossal sum of money has been stolen from BoT under his watch. (countless number of scandals-hata yeye mwenyewe kutumia billions za walipa kodi kujijengea nyumba ya Gavana!)

Prof. Ndullu ameingia BoT...... 1USD=1250Tshs.

Leo after almost a decade while still at the top of the BoT the shilling is at 2185 kwa 1USD.

Please enlighten us. Labda kuna vitu sisi hatujui Kuhusu hawa wasomi wetu waliotukuka.

Masanja
Hili Swali gumu Sana kwa The Boss
 
Mimi ningekua kiongozi wa nchi hi, the Boss ningekua nakutazama kama miongoni mwa Wazalendo wa nchi hi; you have nailed it, umefanya summary vizuri but hope and I'm sure the king hua anapitaga humu, atausoma ushauri wako na ninamwomba Mungu aufanyie kazi. GAvana wa fedha ni mtu muhimu sana nchini mwetu, hata kama humpendi but mawazo yake yachukue hata kama ni kwa tahadhari.
Kama kuna kitu ambacho hata mimi ningeweza kumshauri the king ni hiki; kwasasa anao mawaziri na watendaji wengine wengi tu wanao mwogopa and they are there kufanya chochote anachokitaka, hi ni hatari sana, sasa hivi anatakiwa awe anawapigia simu hata kwa siri kuwaomba ushauri watu ambao hawamwopi, hawa watamwambia ukweli, hawawezi kumwambia tu kile anacho taka kukisikia. Benno ni miongoni mwao.
 
Yaani wewe unajua kuwa Dr. Mpango hajui VAT?

Maajabu hayataisha dunia hii.
Unapo bisha au kukubali kitu, jifunze pia kutunza kumbukumbu; the boss ame refer issue hiyo mara baada ya bunge la bajeti lililokaa mwezi May hadi July, walipendekeza katika bajeti kwamba miamala ya simu na ATM ianze kutozwa VAT, makampuni ya simu pamoja na mabenki yakaongeza bills za utoaji wa pesa and then wizara ikaomba BOT/Gavana akae na mabenki ili wasiongeze bei za huduma kwetu watumiaji, unakumbuka jibu alilotoa Benno? Kama unakumbuka basi ndio kiini cha maneno ya The Boss na la kama hukumbuki, basi usiwe unabisha usicho kijua. Baada ya majibu yale ya Benno hakuna aliye thubutu kusema chochote, gharama zilipanda na maisha yanaendelea so in other words, Benno aliendelea kumfundisha mwanafunzi wake hata nje ya darasa.
 
Back
Top Bottom