Magufuli na Ndulu, Kikwete na Idrissa...

Unapo bisha au kukubali kitu, jifunze pia kutunza kumbukumbu; the boss ame refer issue hiyo mara baada ya bunge la bajeti lililokaa mwezi May hadi July, walipendekeza katika bajeti kwamba miamala ya simu na ATM ianze kutozwa VAT, makampuni ya simu pamoja na mabenki yakaongeza bills za utoaji wa pesa and then wizara ikaomba BOT/Gavana akae na mabenki ili wasiongeze bei za huduma kwetu watumiaji, unakumbuka jibu alilotoa Benno? Kama unakumbuka basi ndio kiini cha maneno ya The Boss na la kama hukumbuki, basi usiwe unabisha usicho kijua. Baada ya majibu yale ya Benno hakuna aliye thubutu kusema chochote, gharama zilipanda na maisha yanaendelea so in other words, Benno aliendelea kumfundisha mwanafunzi wake hata nje ya darasa.
Hujanielewa. Yaani huyo The Boss anajua kuwa Dr. Mpango hajui value added tax ni nini?
 
Nilifikiri ndo furaha yenu Raisi Magufuli na Serikali yake kushindwa sasa kelele za nini tena kama mna uhakika kwamba anashindwa? Kwa nini mnahangaika kumpa mtu ushauri ambaye lengo na furaha yenu ni kuona anashindwa? Mbona mnakuwa kama Wanawake ambao wana sifa ya kutokujua wanataka nini?
Kuwa na adabu acha kudharau wanawake ambapo mmoja ni mzazi wako
Ushamba mzigo
 
BoT boss sio lulu is just another liability.
On his watch tumeshudia haya_:
1.Escrow scandal.
2.Thamani ya sh ikipoteza hadhi yake zaidi ya 200%
3.Economic stagnation
4.Dynamic hyper inflation
5.Massive un employment
6.Money laundering
 
Mimi siamini kama Ndulu ni Gavana Bora...Chukulia kipindi cha Kikwete kila siku shilingi yetu ilikuwa inaporomoka, mimi natamani yule waliyesema kafia marekani angerudishwa apewe hicho cheo cha Ndulu yule jamaa kwangu ndo gavana bora kupita wote ambao wamesimamia BOT, uchumi kipindi cha Mkapa ulitengemaa kwelikweli, au wizara ya Fedha apewe Basil Pesambili Mramba.
Mkuu Mwisenge 1993 uko sahihi kabisa. Mfano Kipindi cha Gavana Ballali (RIP) bei ya Petroli na vyakula ilibaki ile ile for 10 years na nchi ilikuwa na akiba ya takriban miezi 6. Kwa kumbukumbu zangu rekodi hii haijavunjwa.
 
Mimi siamini kama Ndulu ni Gavana Bora...Chukulia kipindi cha Kikwete kila siku shilingi yetu ilikuwa inaporomoka, mimi natamani yule waliyesema kafia marekani angerudishwa apewe hicho cheo cha Ndulu yule jamaa kwangu ndo gavana bora kupita wote ambao wamesimamia BOT, uchumi kipindi cha Mkapa ulitengemaa kwelikweli, au wizara ya Fedha apewe Basil Pesambili Mramba.

Mramba awepo WIZARA YA FEDHA???
 
Mkuu Mwisenge 1993 uko sahihi kabisa. Mfano Kipindi cha Gavana Ballali (RIP) bei ya Petroli na vyakula ilibaki ile ile for 10 years na nchi ilikuwa na akiba ya takriban meiazi 6. Kwa kumbukumbu zangu rekodi hii haijavunjwa.
Mimi huyu Ndulu hakuna chochote anachofanya, hivi si walisema Balali yupo haibasi arudishwe tu aje asaidie uchumi wetu, hawa maprofesa ni mabingwa wa kukariri tu definition
 
Mramba awepo WIZARA YA FEDHA???
Yes Mramba awepo wizara ya fedha atusaidie maana uchumi wa hii nchi unaitaji mtu anayeweza kuiba na kuwarushia wananchi makombo kidogo lakini hii stahili ya Magu ya kubana hali inakuwa tete.
Halafu Mramba ni rahisi kumpigia simu Mkapa na kumwambia huyu kijana wako ananibishia nachomuelekeza kwenye mambo ya Uchumi, Magu lazima amuogope.
 
Sifa moja ya 'watalaam wanaoujua na wanajua kwamba wanajua' ni kuwa hawapendi kujipendekeza na hawaogopi kufukuzwa.

Wao hupenda kushauri kwa sauti ndogo tu ukiamua kuwasikiliza haya ukiwadharau hasara ni kwako.

Kikwete alipokuwa Rais alifanya kosa moja lillilogharibu Taifa mabilioni baadae

Kikwete aliamua kuwasikiliza Ngeleja na Adam Malima ambao walikuwa waziri na naibu waziri na kuacha kumsikiliza Mtaalam Idrissa Rashid aliekuwa CEO wa Tanesco.

Idrissa Rashid alipoteuliwa CEO wa Tanesco alikuta nchi ina mgao wa umeme na hali ya shirika hoi na wanasiasa wanaingilia maamuzi ya kitaalam.

Akapiga marufuku wanasiasa kuingilia maamuzi kwa miaka minne ya Uongozi wa Idrissa Tanesco hakuna mwanasiasa aliezungumza kitu na mgao ukaisha na shirika likaanza kusimama Idrisa alikuwa anawajua vizuri kina Ngeleja na Malima

Malima alianza kazi BOT Idrissa akiwa gavana..

Ngeleja alipokuwa Vodacom Idrissa alikuwa kwenye Management, wangemueleza nini? aliamua tu 'kutowasikiliza.

Idrissa alivyoondolewa tu Tanesco kilichofuata ni ziara za Waziri Ngeleja Tanesco na 'mgao wa dharura ukaanza' the rest is history. Zaidi ya bilioni 500 zilikwenda. Kikwete alikosea kuwasikiliza kina Ngeleja na Malima asimsikilize Idrissa.

Magufuli anaelekea kurudia kosa hilo hilo anapaswa kumsikiliza Benno Ndulu mtaalam aliemfundisha uchumi Philipo Mpango na naamini Ndulu akisema leo ataje his best students Mpango sidhani atakuwemo.

But Magufuli anaonekana kumsikiliza zaidi Dk. Mpango ambae hata VAT tu haoeneshi kuijua vizuri hadi Ndulu alipojitokeza 'kutoa ufafanuzi.

Siku Ndulu akiondoka hapo ndo tutajua hasara kiasi gani kama taifa tutaingia.

Time will tell.
safi mkuu,imekaa kama inavyotakiwa,kudos
 
Nimesoma Thread Yako Hofu Imetanda Sana Kwa Haraka Kuna Umuhimu MkubwA Mkulu Kutoa Nafasi Kwa Hao Wataalam Hasa Ndulu Kufanya Kazi.

Halafu Tuone Je? Mwakani Tutatua Vema Ama Tutakuwa Na Shida. Nchi Hii Huyu Mpango Alikuwa Na Kikwete Kwenye Uongozi Wake.

Ukiangalia Nchi Imejaa Viongozi Wenye Elimu Professor,Doctors, Masters, Bachelor ,Na Elimu Mbalimbali Lakini Mambo Ndiyo Magumu Sana

Kazi Yao Kutamka Kwenye Magazine, Tv
Ila Kumshauri Kiongozi Hali Mbaya Wanaogopa
 
Pale department ya uchumi chuo kikuu cha dar es salaam kuna vichwa vimetulia lakini naona hata wanasiasa hawavitumii.
 
Back
Top Bottom