Ilikuwaje kipindi cha J Kikwete, Mtera haikuwa inazalisha hata MW 1 ya umeme lakini kipindi cha Magufuli lilifanya kazi kwa muda wote?

Mpinzire

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
4,334
2,000
Naam!

Kipindi cha awamu ya nne bwawa la mtera lilifungwa kabisa kwani lilikuwa halizalishi ata unit moja ya umeme na haya aliyasema mwenyewe katika hotuba yake clip hipo chini hapo.

Awamu ya ya 5 kwa muda wote bwawa lilitumika kufua umeme kama kawaida mpaka sasa tunapoambiwa kuwa bwawa lile tena maji yamepungua sana kiasi kusababisha upungufu wa uzalishaji wa umeme?

Bwawa la Mtera lina uwezo wa kuzalisha Megawati 80 mpaka kufikia February mwaka huu 2021 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Dk Alexander Kyaruzi alisema bwawa la mtera lina maji ya kutosha yakuweza kutumika ndani ya mwaka huu wote 2021 na kutufikisha 2022 bila adha yoyote.


Mwanzoni mwa mwaka huu pia Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) likiwatangazia wanainchi wanaoishi pembezoni mwa bwawa ilo kuwa watafungulia maji kutokana na bwawa ilo kujaa sana kiasi inaweza kuathili uendeshaji wa mitambo na wakafanya hizo.

Dr. Alexander Kyaruzi aliteuliwa na Hayati Rais Magufuli mwaka 2016 kuwa mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Tanesco, Dk Kyaruzi ana PHD ya Electrical Engineering aliyoipata kwenye chuo cha The George Washington University nchini Marekani.

Dr. Alexander Kyaruzi uteuzi wake ulitenguliwa na Mh Samia Suluhu Hassan pia Mh Samia akitengua uteuzi wa Mh Mederd Kalemani ambae pia alichukua Masters of Law in Energy and Minerals, Mh Samia alimteua Bwana Omary Issa kuwa kuwa Mwenyekiti Bodi wa Wakurugenzi Tanesco na pia akamteua January Makamba kuwa Waziri Nishati.

Pia Mh Samia Suluhu Hassan alimteua Maharage Chande kuwa Mkurugenzi Tanesco akichukua nafasi ya Dkt Titto Mwinuka ambae alipata shahada ya Mechanical Engineering kwenye chuo cha Manchester nchini Uingereza.


Swali langu kuu "ilikuwaje kipindi cha Jakaya Mrisho Kikwete bwawa la Mtera lilikauka kabisa?

Bado tuendelee kutafuta majibu juu ya mgao wa umeme?
Screenshot_2021-11-19-23-56-19-18.jpg
Screenshot_2021-11-20-11-01-43-27.jpg
Screenshot_2021-11-20-10-55-06-82.jpg
 

Niza doyi

JF-Expert Member
Dec 10, 2019
2,337
2,000
Hangaya bwana!! anatoa wataalamu waliobobea kwenye field hiyo,anaweka wajanjawajanja.

Hujachelewa Hangaya,hata Kikwete alimtoa JPM kwenye barabara akamuweka mwingine.
Mambo yalipoharibika alimurudisha kwenye barabara.

Usione aibu kuwarudisha Hawa wanaume kuliko huyu kijana anayewatesa watu,vyitu vinaoza majumbani.
 

Karaoke

JF-Expert Member
Nov 22, 2019
205
500
Bwawa la Mtera lilijaa maji kutokana na mvua nyingi zilizonyeesha, matatizo hayo ya kujaa maji pia yalitokea kwenye maziwa makubwa ya Tanganyika na victoria.

Kipindi hiki yamepungua kutokana na ukame na ni sababu hiyohiyo iliyotokea kipindi cha kikwete.

Note: kujaa au kupungua kwa maji hakuangalii nani yupo madarakani bali ni hali ya hewa.

Viongozi uliosema wameondolewa madarakani, hawakuondolewa kwasababu walichaguliwa na Magufuli ni kutokana na uwezo wao na kutengeza timu itakayo fanya kazi kwa pamoja.

Kuwa na elimu kubwa kwenye nyanja fulani hakumaanishi una uwezo mkubwa wa kiuongozi kwenye eneo hilo.
 

Mpinzire

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
4,334
2,000
Bwawa la Mtera lilijaa maji kutokana na mvua nyingi zilizonyeesha, matatizo hayo ya kujaa maji pia yalitokea kwenye maziwa makubwa ya Tanganyika na victoria.

Kipindi hiki yamepungua kutokana na ukame na ni sababu hiyohiyo iliyotokea kipindi cha kikwete.

Note: kujaa au kupungua kwa maji hakuangalii nani yupo madarakani bali ni hali ya hewa.

Viongozi uliosema wameondolewa madarakani, hawakuondolewa kwasababu walichaguliwa na Magufuli ni kutokana na uwezo wao na kutengeza timu itakayo fanya kazi kwa pamoja.

Kuwa na elimu kubwa kwenye nyanja fulani hakumaanishi una uwezo mkubwa wa kiuongozi kwenye eneo hilo.
Sawa Multchoice

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Karaoke

JF-Expert Member
Nov 22, 2019
205
500
Tutumie janga hili la umeme km fursa ya kubuni vyanzo vingi zaidi
Ni kweli, hata kwenye ilani ya chama tulichokipa madaraka 2015 walisema kipaombele kitakua umeme unaotokana na gesi, lakini wakaanzisha mradi mpya wa rufiji ambao haukuwepo kwenye ilani yao.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom