Magufuli na mawaziri zake na ziara zao za Dar tu kwenye media

Last emperor

JF-Expert Member
Mar 22, 2015
10,352
9,810
Imekuwa ni fashion sasa kwa serikali ya magufuli na mawaziri wake kufanya ziara za '' kushtukiza '' Dar tu kwenye media ambapo watapata coverage ya kutosha, ina maana matatizo ya watanzania yapo Dar tu? Alianza Magufuli kwenda bandarini, muhimbili, akafuata majaliwa bandarini, akaja kigwangallah kwa Dr Mwaka, Ummy mwalimu amekosa nitoke vipi na yeye ameamua arudi muhimbili. Hivi hakuna hospital zingine za rufaa Tanzania? Kwanini hawaendi mikoa mingine ambako kuna shida na matatizo mengi zaidi? Au Tanzania ni Dar tu? Utakuja kuona kinachoendelea mpaka sasa hivi ni usanii tu wa kutaka waonekane wanafanya kazi sana kumbe hamna kitu, Ni kuuza sura tu kwenye media kana kwamba matatizo yote ya Tanzania yapo Dar. Msituchoshe!
 
wanahitaji waandishi wa kuwauzisha sura,
sasa wakifanya ziara ya kustukiza huko Namtumbo nani atawaona.
 
Deep down utagundua hii nchi viongozi wengi ni empty
yaani Magufuli akikosea na mawaziri wake wanamfuata huko huko kwenye makosa
 
Usanii usanii tu. Wanazunguka hapa hapa tu. Tena kwa watu ambao hawakuwachagua, kwanini wasiende huko Rukwa chama Chao kilipopata kura nyingi, hata kuwashukuru kwa vitendo?
 
mimi nathani tusitegeme jipya kwa magufuli.Nimeshaona serikali yake ikionea wanyonge huku ikijifanya ni mtetezi wa wanyonge lakni hama kitu.Mawaziri hao pia hawana dira mpya wala mustakabali mpya kwenye fani zao.Wao wanataka kuendelea na mambo yale yale ya mwaka sabini na saba.
ingekuwa mimi ni dr hamisi na wazir wake,ningekaa chini na kuangalia ni vipi tuboreshe huduma za afya,madawa na upatikanaji wake,sera ya kuwa na hospitali kubwa kila mkoa na zahanati ndogo kila wilaya,huduma kwa wagonjwa,maslahi ya madaktari na manesi,na vile vile kuimarisha au kubadilisha mfumo wa utoaji huduma za afya kuwa wa kisasa zaidi kama dunia ya kwanza,kuunganisha huduma ya afya kwa njia ya mtandao (faili la mgonjwa linaweza kuwa online madaktari wanaweza kusharea na kuangalia historia nk)
kuimarisha vitendea kazi,vifaaa,na hata sheria na mambo mbalimbali ya kisasa ikiwa pamoja na insurance za afya kwa wote nk.
mimi sioni sababu ya kuzunguka huko na huko maana tatizo la viongozi wa tanzania wamefikia kikomo kwenye ufikiri.
nishaona serikali ya magufuli ikifeli na kuchukiwa vibaya sana kulko hata mkwere...time will tell..
 
Dogo kutambua..nikitu bora..ujamuona Prof Muhongo kafika mtera,pangani huko sio mikoani..

ujamuona Mwiguru Morogoro

ujamuona Jafu na Simbachawene Dodoma

jaribu kutumia akili mda mwingine
 
Lakini Magufuli alishawaambia waende vijijini kwenye matatizo ya wananchi..
Yani wengi wao tayari wameshakuwa majipu kabla hata hawajaanza kazi.
 
Tena tu kwa vile ameacha kupiga pushup mbona wangekuwa wanapiga sana ukasuku tuliupata awamu ya kwanza ya kutaifisha, ujamaa, operation maduka na Universal Primary Education na tulitikisika tu hatukutoka
 
mwigulu yupo kwenye korosho huko lindi....na ameshatoa tamko bila chombo cha habari......tuwape muda yan hata wiki hawana jaman mbona mnakuwa nakiimuhemuhe......mnyonge mnyongeni ila haki yake mpeni
 
Muhongo na mwigulu wameshatembea nje ya dar, tatizo bila media mtajuaje kuwa kuna agizo fulani?
 
Saloon zitapata dili sana kuwanyoa na scrub wave black dahh watapendeza vipiii
 
Imekuwa ni fashion sasa kwa serikali ya magufuli na mawaziri wake kufanya ziara za '' kushtukiza '' Dar tu kwenye media ambapo watapata coverage ya kutosha, ina maana matatizo ya watanzania yapo Dar tu? Alianza Magufuli kwenda bandarini, muhimbili, akafuata majaliwa bandarini, akaja kigwangallah kwa Dr Mwaka, Ummy mwalimu amekosa nitoke vipi na yeye ameamua arudi muhimbili. Hivi hakuna hospital zingine za rufaa Tanzania? Kwanini hawaendi mikoa mingine ambako kuna shida na matatizo mengi zaidi? Au Tanzania ni Dar tu? Utakuja kuona kinachoendelea mpaka sasa hivi ni usanii tu wa kutaka waonekane wanafanya kazi sana kumbe hamna kitu, Ni kuuza sura tu kwenye media kana kwamba matatizo yote ya Tanzania yapo Dar. Msituchoshe!

Wala usichoke, kwanza hukumpigia kura pili humtambui tatu katafute rais wa kwako ndo ukampangie ratiba yako itakayokuwa haikuchoshi.
 
Mbona na wabunge wa mikoani wanashitukiza unataka atoke hapa mpaka mwanza kwa Gari akashitukize, hilo haliwezekani hata akienda kwa ndege utakua ni upotezaji wa fedha na hautakua mshtuku Polisi watajaa barabara yote, kila mbunge awajibike kwa kushitukiza wabunge wa ukawa wala hawana habari
 
Imekuwa ni fashion sasa kwa serikali ya magufuli na mawaziri wake kufanya ziara za '' kushtukiza '' Dar tu kwenye media ambapo watapata coverage ya kutosha, ina maana matatizo ya watanzania yapo Dar tu? Alianza Magufuli kwenda bandarini, muhimbili, akafuata majaliwa bandarini, akaja kigwangallah kwa Dr Mwaka, Ummy mwalimu amekosa nitoke vipi na yeye ameamua arudi muhimbili. Hivi hakuna hospital zingine za rufaa Tanzania? Kwanini hawaendi mikoa mingine ambako kuna shida na matatizo mengi zaidi? Au Tanzania ni Dar tu? Utakuja kuona kinachoendelea mpaka sasa hivi ni usanii tu wa kutaka waonekane wanafanya kazi sana kumbe hamna kitu, Ni kuuza sura tu kwenye media kana kwamba matatizo yote ya Tanzania yapo Dar. Msituchoshe!

Nimemuona mwigulu pwani na morogoro hivi na huko ni dar
 
Back
Top Bottom