Magufuli lazima aende Addis Ababa

Magufuli lazima aende Addis Ababa

Mbona kama unamlazimisha y
WAKUU wa Nchi za Afrika wanatarajiwa kukutana katika mkutano wa kawaida wa kila mwaka mwishoni mwa mwezi huu jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Mkutano huu ni sehemu muhimu ya uwepo wa Umoja wa Afrika (AU). Wakati viongozi wa awali wa bara hili walipofikiria namna ya kuileta Afrika pamoja, mojawapo ya mambo ilikuwa ni kuwa na chombo kitakachowakutanisha viongozi wa nchi zote ili kujadili mambo ya msingi yanayohusu bara hili.
Tanzania ilikuwa ni mojawapo ya nchi waasisi wa AU wakati ilipoanzishwa kama Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) mnamo mwaka 1963.

Tanzania ni mojawapo ya nchi muhimu kwenye AU. Imewahi kuwa Mwenyekiti wa OAU na AU. Imewahi kuwa Makao Makuu ya Kamati ya Ukombozi ya Nchi za Kusini mwa Afrika.

Mwanadiplomasia wa Tanzania, Dk. Salim Ahmed Salim, ndiye mtu aliyewahi kuwa Katibu Mkuu (Mtendaji Mkuu) wa OAU kwa muda mrefu kuliko mtu (raia) mwingine wa nchi yoyote barani Afrika !

Hii haikuwa bahati mbaya. Ilitokana na mchango wetu mkubwa kwenye uanzishwaji wa AU na pia namna wenzetu wanavyotuheshimu na kutuona wa maana.

Ni imani yangu kuwa Rais John Pombe Magufuli atafanya ziara yake ya kwanza ughaibuni wakati wa Mkutano huo wa Addis. Hii ni kwa sababu, nchi yetu inahitaji aende huko.

Kuna dhana inajengeka sasa kwamba kusafiri nje ya nchi kwa viongozi wetu ni dhambi. Nakubali kwamba kuna matatizo kwenye utaratibu wa safari za viongozi ambao unatakiwa kuangaliwa upya lakini sikubali kwamba safari za nje ni mbaya.

Kuna suala la umuhimu wa mikutano husika, idadi ya wanaotakiwa kwenda, kiwango cha malipo kinacholipwa na suala zima la gharama nyingine. Haya ni mambo ya kuangaliwa lakini si kusema kwamba safari ni mbaya.
Mkutano wa Viongozi wa AU ni muhimu kutokana na historia yetu kwenye umoja huo. Kama Magufuli atakwenda Addis, hiyo itakuwa ni fursa kwake ya kukutana na wenzake na kufahamiana nao.

Hii ni fursa ambayo Magufuli anaihitaji. Kwa sababu ya historia yake ya nyuma na ukweli kwamba hana mizizi kwenye dunia ya kidiplomasia, mikutano ya namna hii inampa fursa adhimu ya kujiongeza hapa na pale.
Inafahamika kwamba kwenye mkutano kama huu wa mwezi Januari, viongozi wa AU hutumia nafasi hiyo kumtambulisha kiongozi mpya na kwa kawaida hupewa nafasi ya walau kuwahutubia wenzake.
Hii ni nafasi ambayo Magufuli anaihitaji.

Kwenye mkutano kama huo wa Addis, Magufuli anaweza kukaa kwa siku mbili tu. Na wala hahitaji kwenda na msafara mkubwa. Ipo ndege ya Rais ambayo ilinunuliwa na serikali kwa sababu ya majukumu ya namna hii.
Ni kweli kwamba Magufuli anahitajika zaidi hapa kwetu. Lakini, sisi ni Tanzania. Sisi si mojawapo ya nchi ndogo barani Afrika ambazo hazina historia yoyote kwenye ukombozi wa bara letu.

Mwenyekiti wa AU, Robert Mugabe, ataangalia ilipo Tanzania na kutazama kama Magufuli amekuja. Jacob Zuma wa Afrika Kusini atafanya hivyo pia. Wawakilishi kutoka Sahara Magharibi, Comorro, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Msumbiji nao watatazama.

Magufuli kuhudhuria mkutano wa AU, hakutaongeza mishahara kwa wafanyakazi wa Tanzania, hakutaboresha elimu yetu, hakutaondoa maradhi na hakutaongeza ajira kwa vijana.

Lakini, bado ni mkutano muhimu kwetu kuhudhuria. Ni muhimu kwa Rais wetu kujitambulisha kwa wenzake wote kwa wakati mmoja. Kuzungumza nao na kutoa mwelekeo wa wapi Tanzania inataka kwenda na inatarajia nini kutoka kwa wenzake barani Afrika.

Kuna mambo au maamuzi ambayo nchi inatakiwa kusimamia hata kama hayaonekani kuwa na faida yoyote. Uhusiano wetu na Israel kwa mfano, tungetaka, tungeendelea nao lakini tukabaki na Wapalestina kwa sababu ya msimamo wetu.

Tanzania inasimamia misingi ya Umajumui wa Afrika. AU ndicho chombo pekee kikubwa ambacho walau kinasimamia ndoto hiyo hata kama kwa mapungufu mengi. Pasipo AU, ndoto ya siku moja kuwa na Afrika iliyoungana itakuwa imekufa kabisa.

Taifa au mwanadamu asiye na ndoto ni sawa na kitu mfu. Utaifa ni ndoto. Kwamba watu hawa wa nchi moja wameamua kuwa pamoja ili kutimiza malengo fulanifulani. Kwetu sisi Watanzania, ndoto ya kuwa na Afrika moja imara na yenye maendeleo ni ya kudumu.

Ndiyo maana, naamini kuwa, Rais Magufuli atahudhuria mkutano huu wa Addis. Atahudhuria kwa sababu Watanzania walimchagua ili kusimamia kile ambacho sisi kama taifa tumeamua kusimamia.

Nafahamu mazingira ambayo serikali ya Magufuli na nchi yetu inapita kwa sasa. Wakati mwingine ni mazingira ambayo si rafiki sana kwa mambo yanayohitaji kufanywa kwa kuzingatia tafakuri na lojiki.

Lakini, itakuwa siku mbaya katika historia ya nchi yetu endapo Rais John Pombe Magufuli atakacha kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika mwishoni mwa mwezi huu.
tena unasema atumie ndege ya Rais? Kulikoni? Hatuna imani na ninyi watumbuliwa majipu. Anyway ataenda FM.
 
Ni vyema ukafanyika utafiti kujua ni kwanini Magu ni kama ana 'alergy' na safari za anga.

Asije na yeye akawa kama yule mchezaji wa zamani wa Arsenal Dennis Bergkemp ambaye enzi zile wakati wote timu yake ilipokuwa ikisafiri kwenda kucheza mechi za nje ya uwanja wa kwao kwa ndege yeye alikuwa akisafiri kwa treni au basi.

Iwapo timu yake ilikuwa ikisafiri kwenda mahali ambapo yeye asingeweza kusafiri kwa treni au basi, mchezaji huyo alikuwa akizikosa hizo mechi!

Isije ikawa Magu naye akawa na alergy na usafiri wa anga?
Ungesema allergy na safari za nje na si anga, juzi alikwenda Arusha na kurudi kwa anga kupitia KIA, Zanzibar kwenye sherehe za mapinduzi alikwenda kwa anga.
 
WAKUU wa Nchi za Afrika wanatarajiwa kukutana katika mkutano wa kawaida wa kila mwaka mwishoni mwa mwezi huu jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Mkutano huu ni sehemu muhimu ya uwepo wa Umoja wa Afrika (AU). Wakati viongozi wa awali wa bara hili walipofikiria namna ya kuileta Afrika pamoja, mojawapo ya mambo ilikuwa ni kuwa na chombo kitakachowakutanisha viongozi wa nchi zote ili kujadili mambo ya msingi yanayohusu bara hili.
Tanzania ilikuwa ni mojawapo ya nchi waasisi wa AU wakati ilipoanzishwa kama Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) mnamo mwaka 1963.

Tanzania ni mojawapo ya nchi muhimu kwenye AU. Imewahi kuwa Mwenyekiti wa OAU na AU. Imewahi kuwa Makao Makuu ya Kamati ya Ukombozi ya Nchi za Kusini mwa Afrika.

Mwanadiplomasia wa Tanzania, Dk. Salim Ahmed Salim, ndiye mtu aliyewahi kuwa Katibu Mkuu (Mtendaji Mkuu) wa OAU kwa muda mrefu kuliko mtu (raia) mwingine wa nchi yoyote barani Afrika !

Hii haikuwa bahati mbaya. Ilitokana na mchango wetu mkubwa kwenye uanzishwaji wa AU na pia namna wenzetu wanavyotuheshimu na kutuona wa maana.

Ni imani yangu kuwa Rais John Pombe Magufuli atafanya ziara yake ya kwanza ughaibuni wakati wa Mkutano huo wa Addis. Hii ni kwa sababu, nchi yetu inahitaji aende huko.

Kuna dhana inajengeka sasa kwamba kusafiri nje ya nchi kwa viongozi wetu ni dhambi. Nakubali kwamba kuna matatizo kwenye utaratibu wa safari za viongozi ambao unatakiwa kuangaliwa upya lakini sikubali kwamba safari za nje ni mbaya.

Kuna suala la umuhimu wa mikutano husika, idadi ya wanaotakiwa kwenda, kiwango cha malipo kinacholipwa na suala zima la gharama nyingine. Haya ni mambo ya kuangaliwa lakini si kusema kwamba safari ni mbaya.
Mkutano wa Viongozi wa AU ni muhimu kutokana na historia yetu kwenye umoja huo. Kama Magufuli atakwenda Addis, hiyo itakuwa ni fursa kwake ya kukutana na wenzake na kufahamiana nao.

Hii ni fursa ambayo Magufuli anaihitaji. Kwa sababu ya historia yake ya nyuma na ukweli kwamba hana mizizi kwenye dunia ya kidiplomasia, mikutano ya namna hii inampa fursa adhimu ya kujiongeza hapa na pale.
Inafahamika kwamba kwenye mkutano kama huu wa mwezi Januari, viongozi wa AU hutumia nafasi hiyo kumtambulisha kiongozi mpya na kwa kawaida hupewa nafasi ya walau kuwahutubia wenzake.
Hii ni nafasi ambayo Magufuli anaihitaji.

Kwenye mkutano kama huo wa Addis, Magufuli anaweza kukaa kwa siku mbili tu. Na wala hahitaji kwenda na msafara mkubwa. Ipo ndege ya Rais ambayo ilinunuliwa na serikali kwa sababu ya majukumu ya namna hii.
Ni kweli kwamba Magufuli anahitajika zaidi hapa kwetu. Lakini, sisi ni Tanzania. Sisi si mojawapo ya nchi ndogo barani Afrika ambazo hazina historia yoyote kwenye ukombozi wa bara letu.

Mwenyekiti wa AU, Robert Mugabe, ataangalia ilipo Tanzania na kutazama kama Magufuli amekuja. Jacob Zuma wa Afrika Kusini atafanya hivyo pia. Wawakilishi kutoka Sahara Magharibi, Comorro, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Msumbiji nao watatazama.

Magufuli kuhudhuria mkutano wa AU, hakutaongeza mishahara kwa wafanyakazi wa Tanzania, hakutaboresha elimu yetu, hakutaondoa maradhi na hakutaongeza ajira kwa vijana.

Lakini, bado ni mkutano muhimu kwetu kuhudhuria. Ni muhimu kwa Rais wetu kujitambulisha kwa wenzake wote kwa wakati mmoja. Kuzungumza nao na kutoa mwelekeo wa wapi Tanzania inataka kwenda na inatarajia nini kutoka kwa wenzake barani Afrika.

Kuna mambo au maamuzi ambayo nchi inatakiwa kusimamia hata kama hayaonekani kuwa na faida yoyote. Uhusiano wetu na Israel kwa mfano, tungetaka, tungeendelea nao lakini tukabaki na Wapalestina kwa sababu ya msimamo wetu.

Tanzania inasimamia misingi ya Umajumui wa Afrika. AU ndicho chombo pekee kikubwa ambacho walau kinasimamia ndoto hiyo hata kama kwa mapungufu mengi. Pasipo AU, ndoto ya siku moja kuwa na Afrika iliyoungana itakuwa imekufa kabisa.

Taifa au mwanadamu asiye na ndoto ni sawa na kitu mfu. Utaifa ni ndoto. Kwamba watu hawa wa nchi moja wameamua kuwa pamoja ili kutimiza malengo fulanifulani. Kwetu sisi Watanzania, ndoto ya kuwa na Afrika moja imara na yenye maendeleo ni ya kudumu.

Ndiyo maana, naamini kuwa, Rais Magufuli atahudhuria mkutano huu wa Addis. Atahudhuria kwa sababu Watanzania walimchagua ili kusimamia kile ambacho sisi kama taifa tumeamua kusimamia.

Nafahamu mazingira ambayo serikali ya Magufuli na nchi yetu inapita kwa sasa. Wakati mwingine ni mazingira ambayo si rafiki sana kwa mambo yanayohitaji kufanywa kwa kuzingatia tafakuri na lojiki.

Lakini, itakuwa siku mbaya katika historia ya nchi yetu endapo Rais John Pombe Magufuli atakacha kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika mwishoni mwa mwezi huu.

Sio lazima JPM aende, anaweza kutuma mwakilishi.
 
JK atamuwakilia Rais wetu anabaki kutumbua majipu mnataka aende huku nyuma mnabaki kuficha ushahidi wa makandokando yenu
 
YAANI UNAMLAZIMISHA RAIS ASAFIRI KWANI MAKAMU WA RAIS AKIENDA KUMEPUNGUA NINI? SAFARI NI HIYARI SIYO LAZIMA AKITAKA ATAKWENDA NA ASIPOTAKA HAENDI USIWE KAMA MGANGA WA KIENYEJI ETI LAZIMA AENDE.
Makamu wa rais ni lazima aongozane na JK...na JK huwa hakubali kusafiri na begi la mgingoni peke yake, ni lazima aende na msafala na msafala wake ndiyo kama unavyoujua tena..!
 
Tangu upuuzi wa OAU na AU viwepo wamefanya nn cha maana sana sana kucreate dictators
 
Hah jamaa ajaenda?sasa hizi sifa na yeye kazidi.ni muhimu kwenda akumbuke yeye ni rais wa nchi gani hapa afrika na mchango wa nchi yake katika OAU/AU
 
Inaonekana uko really pan-africanist. Hata hivyo naamini mheshimiwa rais anayajua yote haya. Kama hataenda lazima atakuwa na sababu ya Msingi ya kutofanya hivyo.
 
Hujatoa faida na tija kwa wananchi wa Tanzania iwapo Magufuli atahudhuria!
 
Sidhani km hilo lipo kichwani mwake, kwani bado yuko anapata upepo wa bahari
 
Asee naona kamtanguliza waziri wake wa mambo ya nje,hopeful ataenda.
Sidhani Kama ataenda mkuu. Delegation ya Rais bajeti yake inatisha kidogo, na kwa tunavyomjua Mh Rais anavyochukia kufuja pesa sioni Kama atahudhuria. Au ataenda siku ya mwisho.
 
ataongea nini huko? anaogopa kuchanganya mambo kama wazili wake wa michezo alivyo changanya kilefu cha tff bungeni, na kule sio kama bungeni unaweza kuingia na kulala, kila kiongozi ana zamu yake huko
 
Hapo Le Chinese Professeri Roho inamuumaje!! Ha ha ha. Hapo enzi zile utasikia katokea USA, kapitia kuwapa pole Pakistani kwa mlipuko wa Bomu kwenye moja ya vyuo vikuu kisha kaunga ADDIS ABABA
 
Back
Top Bottom