Magufuli lazima aende Addis Ababa

bukoba boy

JF-Expert Member
Jan 15, 2015
5,370
3,959
WAKUU wa Nchi za Afrika wanatarajiwa kukutana katika mkutano wa kawaida wa kila mwaka mwishoni mwa mwezi huu jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Mkutano huu ni sehemu muhimu ya uwepo wa Umoja wa Afrika (AU). Wakati viongozi wa awali wa bara hili walipofikiria namna ya kuileta Afrika pamoja, mojawapo ya mambo ilikuwa ni kuwa na chombo kitakachowakutanisha viongozi wa nchi zote ili kujadili mambo ya msingi yanayohusu bara hili.
Tanzania ilikuwa ni mojawapo ya nchi waasisi wa AU wakati ilipoanzishwa kama Umoja wa Nchi Huru za Afrika (OAU) mnamo mwaka 1963.

Tanzania ni mojawapo ya nchi muhimu kwenye AU. Imewahi kuwa Mwenyekiti wa OAU na AU. Imewahi kuwa Makao Makuu ya Kamati ya Ukombozi ya Nchi za Kusini mwa Afrika.

Mwanadiplomasia wa Tanzania, Dk. Salim Ahmed Salim, ndiye mtu aliyewahi kuwa Katibu Mkuu (Mtendaji Mkuu) wa OAU kwa muda mrefu kuliko mtu (raia) mwingine wa nchi yoyote barani Afrika !

Hii haikuwa bahati mbaya. Ilitokana na mchango wetu mkubwa kwenye uanzishwaji wa AU na pia namna wenzetu wanavyotuheshimu na kutuona wa maana.

Ni imani yangu kuwa Rais John Pombe Magufuli atafanya ziara yake ya kwanza ughaibuni wakati wa Mkutano huo wa Addis. Hii ni kwa sababu, nchi yetu inahitaji aende huko.

Kuna dhana inajengeka sasa kwamba kusafiri nje ya nchi kwa viongozi wetu ni dhambi. Nakubali kwamba kuna matatizo kwenye utaratibu wa safari za viongozi ambao unatakiwa kuangaliwa upya lakini sikubali kwamba safari za nje ni mbaya.

Kuna suala la umuhimu wa mikutano husika, idadi ya wanaotakiwa kwenda, kiwango cha malipo kinacholipwa na suala zima la gharama nyingine. Haya ni mambo ya kuangaliwa lakini si kusema kwamba safari ni mbaya.
Mkutano wa Viongozi wa AU ni muhimu kutokana na historia yetu kwenye umoja huo. Kama Magufuli atakwenda Addis, hiyo itakuwa ni fursa kwake ya kukutana na wenzake na kufahamiana nao.

Hii ni fursa ambayo Magufuli anaihitaji. Kwa sababu ya historia yake ya nyuma na ukweli kwamba hana mizizi kwenye dunia ya kidiplomasia, mikutano ya namna hii inampa fursa adhimu ya kujiongeza hapa na pale.
Inafahamika kwamba kwenye mkutano kama huu wa mwezi Januari, viongozi wa AU hutumia nafasi hiyo kumtambulisha kiongozi mpya na kwa kawaida hupewa nafasi ya walau kuwahutubia wenzake.
Hii ni nafasi ambayo Magufuli anaihitaji.

Kwenye mkutano kama huo wa Addis, Magufuli anaweza kukaa kwa siku mbili tu. Na wala hahitaji kwenda na msafara mkubwa. Ipo ndege ya Rais ambayo ilinunuliwa na serikali kwa sababu ya majukumu ya namna hii.
Ni kweli kwamba Magufuli anahitajika zaidi hapa kwetu. Lakini, sisi ni Tanzania. Sisi si mojawapo ya nchi ndogo barani Afrika ambazo hazina historia yoyote kwenye ukombozi wa bara letu.

Mwenyekiti wa AU, Robert Mugabe, ataangalia ilipo Tanzania na kutazama kama Magufuli amekuja. Jacob Zuma wa Afrika Kusini atafanya hivyo pia. Wawakilishi kutoka Sahara Magharibi, Comorro, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na Msumbiji nao watatazama.

Magufuli kuhudhuria mkutano wa AU, hakutaongeza mishahara kwa wafanyakazi wa Tanzania, hakutaboresha elimu yetu, hakutaondoa maradhi na hakutaongeza ajira kwa vijana.

Lakini, bado ni mkutano muhimu kwetu kuhudhuria. Ni muhimu kwa Rais wetu kujitambulisha kwa wenzake wote kwa wakati mmoja. Kuzungumza nao na kutoa mwelekeo wa wapi Tanzania inataka kwenda na inatarajia nini kutoka kwa wenzake barani Afrika.

Kuna mambo au maamuzi ambayo nchi inatakiwa kusimamia hata kama hayaonekani kuwa na faida yoyote. Uhusiano wetu na Israel kwa mfano, tungetaka, tungeendelea nao lakini tukabaki na Wapalestina kwa sababu ya msimamo wetu.

Tanzania inasimamia misingi ya Umajumui wa Afrika. AU ndicho chombo pekee kikubwa ambacho walau kinasimamia ndoto hiyo hata kama kwa mapungufu mengi. Pasipo AU, ndoto ya siku moja kuwa na Afrika iliyoungana itakuwa imekufa kabisa.

Taifa au mwanadamu asiye na ndoto ni sawa na kitu mfu. Utaifa ni ndoto. Kwamba watu hawa wa nchi moja wameamua kuwa pamoja ili kutimiza malengo fulanifulani. Kwetu sisi Watanzania, ndoto ya kuwa na Afrika moja imara na yenye maendeleo ni ya kudumu.

Ndiyo maana, naamini kuwa, Rais Magufuli atahudhuria mkutano huu wa Addis. Atahudhuria kwa sababu Watanzania walimchagua ili kusimamia kile ambacho sisi kama taifa tumeamua kusimamia.

Nafahamu mazingira ambayo serikali ya Magufuli na nchi yetu inapita kwa sasa. Wakati mwingine ni mazingira ambayo si rafiki sana kwa mambo yanayohitaji kufanywa kwa kuzingatia tafakuri na lojiki.

Lakini, itakuwa siku mbaya katika historia ya nchi yetu endapo Rais John Pombe Magufuli atakacha kuhudhuria mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika mwishoni mwa mwezi huu.
 
Ni vyema ukafanyika utafiti kujua ni kwanini Magu ni kama ana 'alergy' na safari za anga.

Asije na yeye akawa kama yule mchezaji wa zamani wa Arsenal Dennis Bergkemp ambaye enzi zile wakati wote timu yake ilipokuwa ikisafiri kwenda kucheza mechi za nje ya uwanja wa kwao kwa ndege yeye alikuwa akisafiri kwa treni au basi.

Iwapo timu yake ilikuwa ikisafiri kwenda mahali ambapo yeye asingeweza kusafiri kwa treni au basi, mchezaji huyo alikuwa akizikosa hizo mechi!

Isije ikawa Magu naye akawa na alergy na usafiri wa anga?
 
YAANI UNAMLAZIMISHA RAIS ASAFIRI KWANI MAKAMU WA RAIS AKIENDA KUMEPUNGUA NINI? SAFARI NI HIYARI SIYO LAZIMA AKITAKA ATAKWENDA NA ASIPOTAKA HAENDI USIWE KAMA MGANGA WA KIENYEJI ETI LAZIMA AENDE.
 
Kwa kuwa Ethiopia ipo karibu na Eritrea, bila shaka ataichangamkia fursa hii. Chezea Eritrea!
 
Ni vyema ukafanyika utafiti kujua ni kwanini Magu ni kama ana 'alergy' na safari za anga.

Asije na yeye akawa kama yule mchezaji wa zamani wa Arsenal Dennis Bergkemp ambaye enzi zile wakati wote timu yake ilipokuwa ikisafiri kwenda kucheza mechi za nje ya uwanja wa kwao kwa ndege yeye alikuwa akisafiri kwa treni au basi.

Iwapo timu yake ilikuwa ikisafiri kwenda mahali ambapo yeye asingeweza kusafiri kwa treni au basi, mchezaji huyo alikuwa akizikosa hizo mechi!

Isije ikawa Magu naye akawa na alergy na usafiri wa anga?
Huenda bado hawaamini watu fulani fulani kuwaachia nchi mapema hii.
 
Wewe ni muumini wa Uvasco Da Gama wa Msoga! Hizo ni safari zisizo na tija, OAU na AU ni coffee bars tupu, kebehi na mipasho tu, AU baada ya kizazi cha Nyerere imewahi kufanya nini?! Bora tujiunge na Ecowas wanafanya mambo yanaonekana!
 
Ni vyema ukafanyika utafiti kujua ni kwanini Magu ni kama ana 'alergy' na safari za anga.

Asije na yeye akawa kama yule mchezaji wa zamani wa Arsenal Dennis Bergkemp ambaye enzi zile wakati wote timu yake ilipokuwa ikisafiri kwenda kucheza mechi za nje ya uwanja wa kwao kwa ndege yeye alikuwa akisafiri kwa treni au basi.

Iwapo timu yake ilikuwa ikisafiri kwenda mahali ambapo yeye asingeweza kusafiri kwa treni au basi, mchezaji huyo alikuwa akizikosa hizo mechi!

Isije ikawa Magu naye akawa na alergy na usafiri wa anga?
Mbona Arusha na Zanzibar alienda kwa ndege? Au hukuona?
 
Ingawa ni kweli kuwa Arusha alienda kwa ndege, lakini tunachosema ni kuwa anasafiri kwa nadra sana kwa njia ya anga, je kulikoni???

Hata wakati wa ufunguzi wa Bunge hili la 11 kule Dodoma mwezi Novemba alisafiri kwa barabara badala ya kutumia anga.

Kwa hiyo Magu ni tofauti sana na mtangulizi wake, mzee wa Msoga, ambaye kwake yeye ilikuwa favourite 'hobby' yake ilikuwa kupaa angani kwenda 'kutalii' ughaibuni.
 
BukobaBoy,
Kumbuka vikao vya AU viongozi wa Afrika sana sana watazungumzia jinsi ya kufanya kampeni kuzuia korti ya kimataifa ya The Hague ICC isiwabane na kutoa hotuba zisizo na mashiko kwa mwafrika wa kawaida mfano kuondoa umasikini, elimu/afya bure n.k

Vikao vya AU ni vya ''kuuza sura'' kuwa na ''mimi nilikuwepo'' na zisizo za maslahi kwa taifa.

Hivyo lazima Mh. Rais Dk. John Pombe Joseph Magufuli na yeye pia abanwe na taratibu zile zile (bila kubagua) zinazowabana wafanyakazi wa umma kuzuiwa kwenda safari za nje ambazo kwa kweli hazitaleta tija katika kauli mbiu yake ya ''hapa kazi tu''.

Ama sivyo wananchi wakiona amekwea pipa kwenda Addis Ababa, Ethiopia wataanza kuuliza kama kweli ana nia ya kuokoa fedha ziende kwenye maeneo muhimu kama elimu bure, afya na miundo mbinu.
 
Sioni faida ya hiyo mikutano wakati wanashindwa kusuluhisha migogoro ya AFRIKA mfano Burundi, Somalia, Sudan, DRC na n. K
 
Kuna jipu moja limebaki na tayari limeshaiva akilitumbua hili anaweza kwenda sasa tena Kwa amani
 
Wewe ni muumini wa Uvasco Da Gama wa Msoga! Hizo ni safari zisizo na tija, OAU na AU ni coffee bars tupu, kebehi na mipasho tu, AU baada ya kizazi cha Nyerere imewahi kufanya nini?! Bora tujiunge na Ecowas wanafanya mambo yanaonekana!
 
Ni vyema ukafanyika utafiti kujua ni kwanini Magu ni kama ana 'alergy' na safari za anga.

Asije na yeye akawa kama yule mchezaji wa zamani wa Arsenal Dennis Bergkemp ambaye enzi zile wakati wote timu yake ilipokuwa ikisafiri kwenda kucheza mechi za nje ya uwanja wa kwao kwa ndege yeye alikuwa akisafiri kwa treni au basi.

Iwapo timu yake ilikuwa ikisafiri kwenda mahali ambapo yeye asingeweza kusafiri kwa treni au basi, mchezaji huyo alikuwa akizikosa hizo mechi!

Isije ikawa Magu naye akawa na alergy na usafiri wa anga?
Anaweza akawa na ile phobia ya height..
 
Naunga mkono hoja. Magufuli afike Addis Ababa akatoe salaam za Tanzania kwa Umoja wa Afrika!
 
Back
Top Bottom